arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for July 2007 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» HATA IKINYESHA VIPI, TU ...
» Utajuaje kama uliyenaye ...
» Nizar sasa Simba
» Tsvangirai atangaza ku ...
» BOBAN AZIDI KUSUSWA
» Ni juju la Richmond au?
» Luhanjo aipongeza Celte ...

 

Hongo Ya Ngono

Amani  
Hongo Ya  NgonoKigogo mmoja wa Benki jijini Dar es Salaam, (jina limehifadhiwa) ameonesha kufuru ya pesa kwa kumhonga Miss Tanzania kiasi cha shilingi milioni 3 (3,000,000/=), sambamba na kumuahidi mrembo huyo kumjenge nyumba na kumnunulia gari la kifahari.

Meseji na baadhi ya vielelezo vilivyotua mezani kwa Amani hivi karibuni vimefichua matumizi hayo makubwa ya fedha yanayodaiwa kufanywa na kigogo huyo kwa ajili ya kupalilia penzi la mlimbwende mwenye heshima ya Miss TZ.

Kwa mujibu wa sms hiyo, kiasi hicho cha pesa alichodaiwa kupewa Miss huyo (jina lake limehifadhiwa) ni mwanzo wa huduma atakazopewa endapo atakubali kukandamiza raha na mheshimiwa huyo.
    (27 July 2007)
Views: 1597 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Wabongo NA Picha za X

risasi mchanganyiko  
Wabongo NA Picha za XWarembo wa Tanzania waliojitambulisha kwa jina moja moja la Amina, Janie na Candy wamepiga picha za utupu (x) na kuzisambaza sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Gazeti hili lilifanikiwa kupata picha za baadhi ya warembo hao hivi karibuni wakiwa katika mitindo mbalimbali ya mahaba. Aidha nyuma ya picha hizo warembo hao wameweka namba zao za simu za mikononi pamoja na mitandao wanayopatikana.

Kufuatia kuwepo kwa mawasiliano ya mabinti hao, gazeti hili liliamua kuwapigia kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kumpata Janie aliyedai yupo Arusha kikazi. Janie alisema kuwa, angerudi jijini baada ya siku tatu na kama kuna mtu anahitaji huduma yake aweke mihadi naye kwa sababu alikuwa na ‘oda’ nyingi jijini Dar es Salaam.
    (24 July 2007)
Views: 3976 | Maoni (21) | Soma Zaidi

 

Kudaadeki Walai!!!!

Amani  
Kudaadeki Walai!!!!Katika hali ya kustaajabisha dada mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu kimoja nchini (jina tunalihifadhi) aliyetajwa kwa jina la Veronica Amos, amejikuta akifanyiwa kitu mbaya na vijana wa kihuni.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni usiku wa saa sita eneo la Ubungo, Maziwa jijini Dar-es-Salaam kwenye kichochoro kimoja cha mtaa, ambapo vijana hao walimvamia dada huyo 'sistaduu' na kumchania nguo kisha kumpora simu.

Shuhuda wetu aliyekuwepo eneo la tukio ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alidai kuwa, dada huyo alikuwa akitokea kuponda starehe ndipo alipopatwa na balaa hilo.

"Yule dada ni mwanafunzi wa chuo kikuu (anataja jina) mara kwa mara amekuwa akipita maeneo ya hapa nyumbani usiku, amepanga nyumba ya tano kutoka ninapoishi, siku hiyo alipita kama kawaida yake, nadhani alikuwa anatoka kustarehe.
    (24 July 2007)
Views: 2059 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

RAY C Mgongo Huo

ijumaa  
RAY C Mgongo HuoMbunge mmoja machachari na mwenye msimamo mkali bungeni, ambaye ni kijana na hana mke, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuona 'mgongo' wa mwanadada Ray C katika gazeti dada, Ijumaa Wikienda ya wiki hii.

Tukio hili la aina yake lilitokea siku hiyo hiyo katika baa maarufu ya Chako ni Chako iliyopo Dodoma mjini ambayo wabunge wengi hukaa jioni baada ya vikao vyao ambako Mbunge huyo na mwenzake kutoka Chama cha Upinzani cha CUF ambaye pia ni kijana walikuwa wameketi wakinywa huku Mheshimiwa akisoma gazeti hilo.

Mwandishi wetu wa Dodoma aliyekuwa pembeni akipata chakula chake, alifanikiwa kuyanasa mazungumzo ya wabunge hao wawili wakiongelea picha hiyo ya Ray C. "Aiseee huyu mtoto anatisha, utafikiri Beyonce, hizo ndizo figa ambazo mimi huwa nazitaka, si unajua. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa mnene, mimi hivi sasa nataka shepu kama hizi, lazima nimpate huyu Ray C hivi nikijifanya kumtafutia tripu ya nje kimuziki atakataa?"
    (24 July 2007)
Views: 1677 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Mkali Wa Bongo Ampachika Mkali wa Kenya Mimba!!

risasi jumamosi  
Mkali Wa Bongo Ampachika Mkali wa Kenya Mimba!!Ama kweli wahenga hawaongopi, kwanini? Walisema mficha uchi hazai, unakumbuka jinsi Amani na AY walivyojitahidi kuzima uvumi wa wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi? Walizani mapenzi yana siriii, sasa limebumbuluka Amani huyo ana mimba.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari (jina tunalihifadhi) ni kuwa mapenzi ya siri baina ya wasanii hao yamefikia kikomo baada ya Amani kuamua kushika mimba ya AY. Chanzo hicho kilidai kuwa licha ya mwanadada huyo kuwa na ujauzito wa AY bado wanataka iwe siri kubwa.
    (24 July 2007)
Views: 1664 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Jedi Kuzeekea Kwenye Muziki

ijumaa wikienda  
Jedi Kuzeekea Kwenye Muziki
Msanii mkongwe katika game ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady Jaydee' (pichani juu) ameiambia Abby Cool & MC George Over The Weekend kuwa kwa upande wake hana mpango wa kuachana na sanaa ya muziki hata akifikisha umri kama alionao mwanamuziki mkongwe wa taarab, Bi. Kidude.

Akipiga stori zaidi na safu hii nyumbani kwake eneo la Hananasif, Kinondoni, Dar es Salaam, Jide a.k.a Komando, alisema kwamba wapo baadhi ya watu ambao huwa wanafikiria ameachana na game ya muziki pindi anapokuwa kimya, kitu ambacho siyo kweli.

'Kimya changu huwa ni kukaa na kufikiria vitu vipya vya kuimba, ndiyo maana huwa natoka na mashairi ambayo yanaigusa jamii, ambayo pia huiteka Afrika Mashariki, alisema.

Akiyazungumzia mabadiliko yake katika muziki, ikiwemo staili ya kwaito ambayo anaitumia hivi sasa, Jide alisema kwamba hiyo ni kutokana na kutembelea nchi mbalimbali kisha kupata mawazo kutoka kwa wanamuziki wengine wakiwemo wale ambao wamefanikiwa kupitia staili hiyo ya kwaito.

Msanii huyo ambaye anamiliki tuzo kumi na moja amesema kuwa nia yake ni kuongeza nyingine zaidi ili ndoto zake za kuwa mwanamuziki anayemiliki tuzo nyingi zitimie.

Hivi sasa Jide anamiliki bendi inayojulikana kama Machozi Band ambayo ina jumla ya wasanii kumi. 'Nina mpango wa kuipeleka Machozi nje ya nchi ili kwenda kujifunza mengi zaidi' alisema.
    (24 July 2007)
Views: 834 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Skendo Ya Ngono

ijumaa wikienda  
Skendo Ya NgonoMtangazaji wa Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV), Irene Kiwia, ameingia katika skendo ya ngono baada ya kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo mmoja ambaye ni mume wa mtu.

Habari toka kwa chanzo chetu cha kuaminika zimedai kuwa kutokana na uhusiano huo, ndoa ya kigogo huyo (jina tunalihifadhi) imetingishika kwa kiasi kikubwa mpaka kukaribia kusambaratika.

Chanzo chetu kilifafanua kwamba ndoa ya mume huyo ambaye ni mdogo wa mmoja wa mawaziri maarufu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, ilitingishika baada ya mke wa kigogo kubaini uwepo wa mapenzi kati ya mumewe na Irene.
    (24 July 2007)
Views: 2198 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Mganga Aliye Weka Kufuli

uwazi  
Mganga wa kienyeji, Bibi Catherine Punde Kadede (70) mkazi wa Msangani Wilaya ya Kibaha ambaye anadaiwa kumuweka kufuli sehemu za siri mwanamke mmoja ili apate mimba hatimaye kuzaa ameanikwa hadharani.

Aliyemuanika hadharani ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Bw. Henry Salewi alipoongea na waandishi wa habari ofisini kwake wiki iliyopita ambapo alisema mganga huyo alikuwa akimtibia mgonjwa wake aitwaye Halima Mohamed ambaye alienda kupata tiba baada ya kuishi kwa miaka miwili na mumewe bila ya kupata mamba.

Mwanamke huyo ni mkulima wa eneo la Jamaika Kwa Mathiasi na alikwenda kwa mganga huyo akitaka apatiwe dawa ili aweze kupata mtoto baada ya kutopata mtoto kwa kipindi hicho alichoishi na mumewe.

    (24 July 2007)
Views: 705 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Sheshe La Ujambazi Bongo!!!

uwazi  
Sheshe La Ujambazi Bongo!!!Mapambano kati ya vyombo vya usalama nchini na majambazi yaliyotokea Arusha wiki iliyopita hayajawahi kutokea. Kauli hiyo ilitolewa na baadhi ya watu walioshuhudia mapambano kati ya polisi, wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Usalama wa Taifa ambapo majambazi mawili yalirushiana risasi na wanausalama hao.

UWAZI ambalo lilikuwa katika eneo la tukio huko Njiro, mjini Arusha lilishuhudia ‘vita’ hiyo ambapo baadhi ya polisi waliozungumza nasi walisema walielekezwa kutoka ngazi za juu ya jeshi la polisi kutowaua watuhumiwa hao wa ujambazi wakati wanashambuliana.
    (24 July 2007)
Views: 980 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mbunge, mumewe sasa matatani

risasi mchanganyiko  
Ndoa ya Mbunge wa Chama cha Wananchi CUF, Meryce Mussa Emmanuel na Maberana Bashinde imeingia matatani baada ya mume wake wa awali Musa John Buganga kufungua kesi kupiga ndoa hiyo na mambo mengine kadhaa.

Buganga amefungulia wanandoa hao kesi ya madai Civil Case Number 37 ya 2007 katika mahakama ya Wilaya ya Ilala (Samora) Julai 16, mwaka huu.

Mwandishi wetu alifanikiwa kuiona hati ya wito (summons) inayokwenda kwa Mbunge Meryce na Bwana Maberana ikiwataka wawili hao kusimama kizimbani Agosti 7, mwaka huu saa 2.30 asubuhi.

Katika hati hiyo ya madai, Buganga anataka mahakama itengue ndoa hiyo kwa vile mwanamke huyo ni mkewe na itangaze kuwa ndoa yake na mkewe imeshavunjwa.
    (24 July 2007)
Views: 579 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Kitchen Party Ya Hoyce Temu Yazua Jambo!!

risasi mchanganyiko  
Kitchen Party Ya Hoyce Temu Yazua Jambo!!
Kitchen Party ya aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu ilikuwa ya aina yake kufuatia watu wa Usalama wa Taifa ‘system’ kuweka ulinzi wa ‘kufa mtu’ huku mwandishi wa gazeti hili akitishiwa bastola.

Shughuli hiyo ambayo ilifanyika Julai 22, mwaka huu katika Ukumbi wa Water Front jijini Dar es Salaam, ilihudhuriwa na watu maarufu lukuki akiwemo mke wa Rais mstaafu, mama Anna Mkapa.

Mwandishi wetu (jina tunalihifadhi) ambaye alifanikiwa kupata mwaliko wa ‘kitchen party’ hiyo akiwa amejikoki kisawasawa, alitinga katika ukumbi huo na kuchagua meza moja iliyopangwa mahususi kwa ajili ya wageni waalikwa.

Alipotulia, mwandishi huyo alianza kusoma mazingira huku akiweka sawa kamera yake ili aweze kuchukua baadhi ya matukio yaliyojiri katika ukumbi huo.
    (24 July 2007)
Views: 2451 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Waliomuua Amina Kazi Kwao!

uwazi  
Waliomuua Amina Kazi Kwao!Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Bw. Jamal Rwambow ametoa msimamo wa jeshi lake kuwa watawakamata na kuwahoji wale wote wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mbunge kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) marehemu Amina Chifupa endapo watapata taarifa yenye ushahidi juu ya kifo hicho.

Akizungumza na mwandishi wetu juzi kwa njia ya simu Kamanda Rwambow alisema kuwa endapo baba wa marehemu atakuwa dira kwa kuwakilisha majina ya watu wanaosadikiwa kuhusika na kifo hicho watayapokea na kuyashughulikia kisheria.

"Sisi polisi mkoa wa Kinondoni hatujapokea malalamiko hayo lakini wanafamilia wakilalamika na kutuletea majina hayo tutayafanyia kazi," alisema Rwambow.
    (22 July 2007)
Views: 1584 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Mbinu Mpya ya Majambazi Tanzania.

---  
Katika hali ya kustaajabisha, watu wamebaki wamejishika tama huku wakijiuliza kulikoni ndani ya serikali hii iliyoingia na falsafa ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Ikumbukwe kwamba falsafa za namna hii zimekuwa kama kichocheo cha uharifu ndani ya jamii zikiwa zimeanzishwa na viongozi wanaoingia madarakani au wanaotaka kuingia madarakani. Ni awamu iliyopita tu ya braza Benny iliingia na "mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe". Na baada ya kitambo kidogo tu wasafiri wa mabasi kupitia Singida walivamiwa na majambazi na kuvuliwa nguo zao zote na kunyang'anywa kila kitu huku wakiimba, "mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe".

Kwa kutafuta staili ya mtoko, JK naye akaona bora aandae falsafa yake ili aamushe hamasa miongoni mwa watanzania.Nakubali kwamba falsafa hizi zinatumiwa na mabwana hawa kwa nia nzuri, lakini watu walalahoi ambao wameona unyanganyi wa mali na roho za watu wasiokuwa na hatia ndiyo njia pekee ya kupambana na maisha ndani ya nchi inayopambana na janga la ukame na njaa.Sasa ni karibia matukio ya ujambazi ishirini yametokea, lakini lilotia fora ni lile la jana la NBC Bank pale karibu na Ubungo Plaza.Unajuwa ni mbinu gani iliyotumika?Ngoja nikusimulie kisa kilivyoanza.
    (20 July 2007)
Views: 331 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mnyama Msumbufu.

champion  
Je, Unamfahamu mnyama msumbufu? Majawabu mbali mbali yaweza kutolewa yupi ni mnyama msumbufu kuliko wote hasa kwa wale wafugwao.Jibu la haraka mtu aweza kusema ni mbuzi kwa wale waliowahi kukaa vijijini wakakumbana na shughuli za kuchunga mnyama huyu wanalifahamu vizuri hilo. Anajulikana kama mbuzi japokuwa ndugu yangu Mwaipopo kwao anajulikana kama mbusi.Kwa wale "maboni tawuni", nasema kumradhi sana kwani mtakuwa hamuelewi purukushani za huyu mnyama isipokuwa mnamfahamu katika mahadhi ya kimapishi hasa kupitia kitoweo chake muruwa.
Kwa upande mwingine binadamu kama kiumbe alipewa uwezo na akili za utashi ni kiumbe msumbufu kuliko vyote.Pamoja na akili yake, kiumbe huyu haridhiki na kila hali aliyonayo.

Nikianzia na mimi nilipokuwa Dar es Salaam nilikuwa nalalamika joto na kulala bila hata kujifunika.Hali hii ilisababisha malalamiko makubwa sana kiasi kwamba hata wakati mwingine nilisahau kwamba mambo haya ni ya asili na kuna mtu aliye na nguvu za kufanya marekebisho na hivyo kukufuru mda wote.Hamadi nikapata hii fursa ya kuja huku Steti kama panavyojulikana kule bongo kwa kupatukuza.Wakaniambia nitakuta baridi kali hadi barafu nikasema itakuwa vizuri manake hili juwa lilikuwa linakaribia kunitowa roho.Nilipotuwa huku tabu ikaanza mwanetu mimi nimeonea wapi barafu nchi kavu!Malalamiko yakaanza.
    (20 July 2007)
Views: 323 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Ni kwa maslahi ya UMMA au maslahi ya NYUMA?

---  
SAKATA la ununuzi wa rada iliyonunuliwa na Serikali ya awamu ya tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika mazingira ya utatanishi mwaka 2002, lingali likichanja mbuga kama moto wa nyikani nyakati za kiangazi. Wengi wetu ambao tulikuwa hatujui kwa undani nini hasa kilikuwa ama kingali kimejificha ndani ya sakata hili, hivi sasa tunayajua, baada ya ukweli wake kuanza kuanikwa hadharani.

Teknolojia imetuwezesha kufunguliwa macho, Teknolojia imeonyesha tena umuhimu wake katika mchakato wa maendeleo, mchakato wa kuleta ukombozi, mchakato wa kupambana na ulafi wa baadhi ya viongozi wetu na uozo uliomo ndani ya baadhi ya serikali zetu, sio tu za kiafrika bali duniani kwa ujumla. Si hata serikali ya Uingereza ilichangia katika hili? unadhani sio uozo huo?

Bunge la Uingereza limejadili suala hili, na kukiri kuwa rushwa ilikuwemo katika manunuzi hayo, Rais wetu, mhe. Jakaya M. Kikwete, kaomba arejeshewe chenchi (cha juu kama wanavyosema vijana wa kizazi cha sasa), kutoka katika mabilioni yaliyokuwa yametolewa kwa ajili ya kununua rada hiyo. Ni kizungumkuti na mshike mshike kila kona kwa ujumla hivi sasa.
    (20 July 2007)
Views: 250 | Maoni (0) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us