Na Kulwa Mwaibale Mkali wa Filamu na Michezo ya kuigiza nchini, Vincent Kigosi 'Ray', hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mbaroni na Askari Polisi wa China.
Chanzo chetu cha habari kilichopo nchini humo, kinaeleza kuwa wanausalama hao walifikia hatua hiyo baada ya kumhisi kuwa alikuwa akitaka kufanya ugaidi....
Na Joseph Shaluwa Wakati warembo 26 wanatarajiwa kupanda jukwaani kesho katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaa, kuwania Taji la Miss Tanzania 2007-2008, Mlimbwende wa mwaka huu atakayewakilisha nchi yetu katika Shindano la Dunia 'Miss Word' atapatikana kutoka mikoani, Ijumaa limedokezwa....
Nasir Abdul na Mabure Ibrahim, Tanga Katika kile kinachoonesha kuwa dunia inakaribia kufika mwisho, Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini, Peter Mngazija ameuawa baada ya kufumwa na mke wa mtu....
Richard Bukos na Christopher Lissa Kesi inayowakabili Dereva na kondakta wa Basi la wanafunzi wanaotuhumiwa kumlawiti mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka 8 (Shule na jina lake vinahifadhiwa kwa sababu maalum) ambayo ilikuwa iungurume juzi katika Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Kinondoni imeaharishwa hadi Septemba 5,mwaka huu....
Na Hamida Hassan Miss Tanzania 2006-2007 Wema Sepetu ambaye ni mshiriki namba 03 katika Shindano la The Ijumaa Sexiest Girl, amewafuata Rashida Wanjara na Flaviana Matata, baada ya kutolewa kwa 11.6% ya kura zote zilizopigwa na wasomaji wetu kupitia mtandao unaoendesha mtanange huo....
Laibon hakuwa na matumaini ya kumpata tena Tina, aliamua kukubaliana na ukweli kuwa Tina alikuwa ameshafariki! Aliamua kuukubali ukweli huo ili aweze kuendelea na safari yake kama kawaida. Tina naye anahangaika kumtafuta Laibon kila mahali bila mafanikio!....
Baada ya salamu alinipa pole kwa kuumwa kisha alinieleza kila kitu kuhusu yule bibi aliyenifunga hirizi na kuniambia kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kumfukuza angemtambua.
Maimuna alinionya niache kujihusisha na yule msichana wangu, kwa kuwa nilikuwa nampenda sana binti huyo nilimwambia ingekuwa vigumu kumuacha....
Nakurabisha kwa moyo mkunjufu katika safu hii maridhawa ambayo hukuletea mambo mbalimbali juu ya kutambua mambo ya Uhusiano na Mapenzi. Ninaamini kwa uwezo wa Maamani utakuwa mzima wa afya njema na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku....
Na Richard Bukos Mama mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Cecilia hivi karibuni alijikuta akipata kipondo cha nguvu baada ya kufumwa akila raha na mume wa jirani yake.
Tukio hilo la aibu lilitokea usiku wa manane wa Agosti 28 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Manzese karibu na Uwanja wa Fisi jijini Dar es Salaam....