Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big brother Africa, linaloendelea nchini Afrika Kusini, Richard Bezuidenhout (24) juzi alitoa kali akiwa katika mahojiano maalum na kiongozi wa jumba hilo, Big brother pale alipouliza kama kuna sehemu ndani ya jumba hilo ambako kamera hazifiki....
Na Mwandishi Wetu Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu kumkabidhi umalkia wa urembo Richa Adhia aliyeibuka kidedea mwaka huu, wadau wa tasnia hiyo wamemkataa....
Richard Bukos na Christopher Lissa Mnenguaji wa kujitegemea Mwajuma Thabiti anayefahamika pia kwa jina la Rose Jimama, hivi karibuni alifanya kufuru la nguvu ukumbini baada ya ‘kubanjuka’ kama anavyoonekana katika picha .....
Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga. Mtoto wa darasa la sita (14) (jina na shule anayosoma kapuni) mkazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kubakwa na kunyongwa na watu wasiofahamika....
Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii maridhawa nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na shughuli zako ya kila siku katika kuyaboresha maisha yako....
Baada ya Jokate au Jack kuamua kuachana na Mchungaji Patrick aliyekuwa akimtumia katika masuala yake ya ngono huku akifahamu wazi kwamba kufanya hivyo ni dhambi, mchungaji huyo sasa ameamua kuhamishia nguvu zake kwa mke wa muumini aitwaye mama Kisambale....
Kwa wasomaji wapya, kijana Salum Mlangwa mkazi wa mtaa wa Maganga uliopo Temeke jijini Dar es Salaam ametokewa kupendwa na jini wa wa kike wa Kiarabu aitwaye Husna ambaye amefanikiwa kuzaa naye mtoto wa kiume baada ya kufanya naye mapenzi chini ya bahari....
Hii ni kali! Mwarabu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, hivi karibuni ametolewa chumbani na changudoa aliyekuwa uchi wa mnyama baada ya kugoma kumlipa fedha walizokubaliana kama ujira wa kufanya naye mapenzi.
Changudoa aliyedaiwa kumkurupua Mwarabu huyo alijulikana kwa jina la Ester Mushi mkazi wa Kipunguni jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea Septemba 1, mwaka huu saa 3.45 asubuhi katika Hoteli ya Holiday Inn, iliyopo eneo la Posta.....
Mdau maarufu wa michezo nchini, Jack Pemba, hivi karibuni alifanya madudu ya aina yake baada ya kumkandamiza ‘midenda’ mfululizo mkewe Anti Ezekiel, mbele ya umati wa watu.
Wakili Dk. Ishengoma akiwa katika tamaa ya mali na kumpata Samantha ili awe mke wake, amefikia uamuzi wa kumuua Nyakutengwa (mume wa Samantha) akiwa mahabusu, anaamini kijana huyo akifa lazima yeye atamuoa Samantha.
Amemtuma kijana aitwaye Chacha, mteja wa dawa za kulevya ambaye huosha magari nje ya jengo la Sukari House, amemvalisha nguo mpya na kumtaka ampelekee Nyakutengwa chakula chenye sumu mahabusu, sumu imewekwa upande mmoja na upande mwingine hakuna sumu, Chacha alipofika gerezani alikionja chakula hicho mbele ya Nyakutengwa na askari jela akidai alikuwa ametumwa na Samantha kwa sababu yeye alikuwa mgonjwa. Nyakutengwa amekipokea chakula na kukipeleka mpaka mahali alipokaa rafiki yake Thobias, wote wawili hawakitilii mashaka yoyote wako tayari kwa kula. Je, nini kitafuata? SONGA NAYO…
Naomba nianze kwa kumshukuru Muumba aliyetupa uzima pamoja na afya njema na kuweza kutukutanisha mimi na wewe katika safu hii tena kwani kunawenzetu ambao walipenda kuiona siku hii ya leo lakini kwa rehma zake Mola hawakuweza kufika wote tuseme asante Mungu.
Kama nilivyokueleza wiki iliyopita kuhusiana na tabia zinazoweza kukuonesha mwanamke aliyekupenda kwa tamaa ama kama mimi nilivyoamua kumuita ni mwanamke asiye na subira na hivyo kutofaa kuwa mwanamke bora wa kutafuta naye maisha. Leo nitamuongelea mwanaume ambaye ana tabia za uchoyo na asiyependa ndugu wa upande mwanamke.