arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 08.09.2007

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» The Blood Deal! -45
» MAMA HUYU AENDELEA KUTE ...
» AISHA MADINDA
» Michael Jackson afariki ...
» silent forever! -27
» Nyayo za damu-3
» Dalili za rafiki yako k ...

 

Bibi kizee afanya kufuru beach

risasi jumamosi  
Bibi kizee afanya kufuru beach
Na Mwandishi Wetu
Kudadeki, ama kweli maisha ni ubishi! Huwezi kuamini kile kilichotokea hivi karibuni huko majuu baada ya bibi kizee (hakikuweza kufahamika jina lake) kinachokadiriwa kuwa na miaka 70, kufanya kufuru katika ufukwe (beach).

Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa kwetu mwishoni mwa wiki hii na dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Rachel Kidenda, bibi kizee huyo (pichani mbele) alipigwa picha na mapaparazi katika ufukwe ambao haukuweza kujulikana mara moja kisha picha zake kusambazwa mtandaoni.
.....
    (8 September 2007)
Views: 2463 | Maoni (13) | Soma Zaidi

 

Zitto kufa vibaya?

risasi jumamosi  
Na Tulizo Kilaga
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mhe. Zitto Kabwe huwenda akafa vibaya kutokana na tabia yake ya kufichua mambo na kusema ukweli pasipo woga.

Hali hiyo imebainika, hivi karibuni kutokana na kufuatilia mambo ya serikali na viongozi kwa karibu kiasi cha kutaka kuweka ubovu wao hadharani jambo lililomfanya asimamishwe
kazi.
    (8 September 2007)
Views: 1049 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Ndoa na mabadiliko yake (2)

risasi jumamosi  
Ahlan wasahlan, karibu tena msomaji wangu, kama kawaida yetu tupeane mawili matatu kuhusiana na suala zima la uhusiano. Uwanja wa Mahaba ndiyo jina la safu yetu, ushirikiano baina yangu na wewe ndiyo silaha ya kuidumisha.Tunalazimika kuongea mapenzi kwa sababu yanatuhusu, kila binadamu mwenye utimamu wa akili na afya lazima ayapitie, lakini hutokea kuwasumbua wengi na kuwafanya wengine kuwa ndani ya majuto na ndiyo maana tunaamua kuelekezana.Wiki iliyopita tuliangalia sehemu ya kwanza ya mada hii inayohusu ndoa na mabadiliko yake, naamini ujumbe ulifika kwa sababu nimepokea simu za kutosha na sms ambazo ni uthibitisho kuwa safu hii inasomwa na ndiyo maana naiita ‘Safu Pendwa’.Wengi walipongeza siyo rahisi kuwataja wote ila napenda niwaongelee Jeniffer Gwakisa wa Mpanda na Jelemia Hasnati wa Tabora kwa kitendo chao cha kuchoma masalio yao ya simu na kunipigia kunishauri kuhusu mada hiyo pamoja na muongozo mzima wa kona ya Uwanja wa Mahaba.....[/i]
    (8 September 2007)
Views: 516 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

I am Back from Hell: Nimerudi toka kuzimu 1

risasi jumamosi  
Sauti ya kwanza ya Muadhini ilisikika kila mahali maeneo ya Kinondoni, hiyo ilimaanisha kwamba tayari ilishagonga saa kumi kasorobo ya alfajiri. Watu wengi waumini wa dini ya kiislamu waliamka vitandani mwao na kuanza kujiandaa kwa ajili ya swala ya alfajiri ambayo huanza saa kumi na moja kasoro robo.

Nje ya nyumba bado kulikuwa na giza nene, angani kulikuwa na mawingu mazito na manyunyu ya mvua yalikuwa yakidondoka taratibu, ulikuwa ni mwezi Novemba ambao kwa kawaida huwa na mvua nyingi jijini Dar es Salaam, jiji hili ambalo mara nyingi husifika kwa joto, lilikuwa na hali ya baridi.

    (8 September 2007)
Views: 621 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

THE HIDDEN TRUTH (UKWELI ULIOFICHWA) - 58) Na E.J Shigongo

risasi jumamosi  
Wakili Ishengoma anautaka utajiri wa Samatha kwa gharama yoyote ile. Anaamini akimuua mume wake Nyakutengwa akiwa gerezani, yeye ndiye atakuwa mume wake baada ya hapo hivyo utajiri wote wa marehemu Davis Mosha utaingia mikononi mwake! Katika kulitekeleza jambo hili, ametuma chakula chenye sumu gerezani ambacho kimefanikiwa kumfikia Nyakutengwa lakini kabla hajakila aliitwa ofisini kwa mkuu wa gereza na kumwacha rafiki yake Tobias akila.

Aliporejea dakika ishirini baadae alimkuta Tobias akilalamikia maumivu makali ya tumbo, mara moja anachukuliwa na kupelekwa zahanati ya gereza ambako inagundulika amelishwa sumu na daktari kuamua awahishwe haraka iwezekanavyo hospitali ya Muhimbili na gari linaondoka kwa kasi lakini linakwama lilipofika barabara ya Nyerere ambako magari yote yamezuiliwa sababu viongozi wa SADC wanaingia kutokea uwanja wa ndege.
Je, nini kitaendelea, SONGA NAYO….
    (8 September 2007)
Views: 522 | Maoni (0) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com