Na Christopher Lissa Hili ni soo! Raia wawili wa Visiwa vya Comoro, Abascar Malide (40) na Ibrahim Assioundru (35), jana (Jumatano) walifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar-es-Salaam kwa tuhuma za kukutwa na dawa hatari za kulevya aina ya bangi, zenye thamani ya shilingi milioni 25.....
Na Waandishi Wetu Katika kile kilichodaiwa kuwa ni mishemishe za vunja jungu kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, jiji la Dar es Salaam sasa linanuka ngono kutokana na kuongezeka mara dufu kwa biashara ya ukahaba....
Na Adolf Balingilaki Uchaguzi wa wajumbe na viongozi wa mikoa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), umempa wakati mgumu Rais Jakaya Kikwete wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini wamesema....
Filipo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa akitibiwa baada ya kujikata sehemu za siri na kuziondoa kabisa Septemba 2, mwaka huu wa 2007 katika kijiji cha Inyonga na kumsababishia kutokwa na damu nyingi na maumivu makali....
Mnenguaji na mfundaji maarufu aliyezimika ghalfa, wapenzi wa taarabu ni vilio tupu. Kwa yeyote ambaye ni mdau wa muziki hasa ule wa mwambao, nazungumzia muziki wa taarab jina la Shenazi Salum sio geni masikioni mwake....
Mpenzi msomaji, kila aliye na mpenzi anatamani sana uhusiano wao udumu kwa muda mrefu na ikiwezekana aweze kutimiza ndoto zake mke ama mume. Kitu unachotakiwa kujua ni kwamba, si rahisi sana kulitunza penzi lenu kama hutakuwa makini kwani siku hizi kumekuwepo na vishawishi vingi kiasi kwamba kila siku tunashuhudia wapenzi wamekuwa wakiachana....
Mchungaji Patrick ameachana na Jack, mtoto wa mzee wa kanisa na hivi sasa yuko na mke wa muumini aitwaye mama Kisambale. Mwanamke huyu alikwenda ofisini kwa mchungaji kuelezea matatizo yake ya kutopata mtoto kwa miaka yote kumi aliyoishi kwenye ndoa yake jambo lililopelekea familia ya mume wake waanze kumnyanyapaa na kumkosesha raha ya maisha.....