Na Waandishi Maalum Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kijana mmoja na mpenzi wake ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, wakazi wa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita walibambwa wakifanya mapenzi ndani ya gari.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na waandishi wetu, lilitokea Jumamosi iliyopita saa nne usiku, karibu na nyumba ya kufikia wageni, iitwayo Mabibo Lodge iliyopo Mabibo jijini.....................................
Na Julius Kihampa BAADA ya kuwepo kwa mtazamo tofauti juu ya asili ya Miss Tanzania 2007 Richa Adhia, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Watanzania wote kwa ujumla ‘kumsapoti’ mrembo huyo badala ya kushutumu juu ya rangi yake.....
Na Joseph Shaluwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, amelizwa na hali ngumu ya maisha waliyonayo watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo yatima.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Hoyce alisema kuwa maisha magumu waliyonayo watoto yatima yanamkosesha raha na kumfanya atokwe na machozi kila anapowakumbuka....
Imelda Mtema na Catherine Kassally Stadi wa Bongo Fleva nchini, Abdul Sykes 'Dully Sykes' kama asipokuwa makini, anaweza kumuuzia penzi lake jimama aliyejulikana kwa jina moja la Kuruthumu ambaye ametenga kitita cha shilingi milioni 10 ili kumpata mwanamuziki huyo....
Na Hamida Hassan. Mnenguaji wa African Stars Band 'Twanga Pepeta' Aisha Madinda, amekuwa wa tano kuaga Shindano la The Ijumaa Sexiest Girl, baada ya kupata 12.6% ya kura zote zilizopigwa na mashabiki....
Mshiriki wa Kenya Jeff katika Jumba la BBA, ambaye aliondolewa ndani ya jumba hilo wiki mbili zilizopita, anatarajiwa kukaribishwa kwa ‘pati’ ya nguvu nchini kwao leo....
Nilipomuuliza alifanya nini alinijibu kwamba alifanya ndumba za kutaka kumuangamiza hivyo atamuonesha yeye alikuwa nani, nilipomuomba asimfanye chochote alisema huwa hachezewi hata siku moja.
Baada ya kuongea na jini huyo kwa muda aliniaga na kutoweka kwa kupitia ukutani, kulipokucha nilimsimulia mama kila kitu ambapo alishangaa....
Laibon, Tina, bibi Khadija na mtoto mdogo Hope ambaye Laibon alimwokota wakati wa mapigano huko Darfur, wapo ndani ya chumba kidogo chenye kiza na hewa nzito kwenye meli iitwayo St. Petersburg Royal Marine inayoelekea Urusi.
Ingawa lengo la safari yao ni kwenda Marekani, wameamua kupanda tu meli hiyo ili waondoke Mogadishu, hawakutaka kabisa kuendelea kuwa Afrika.....
Nikiacha kumshukuru Mungu wangu kutokana na mema anayonifanyia katika maisha yangu, nitakuwa sina busara, hakika ni wajibu wangu kumshukuru kwa kuwa siku zote amekuwa akinipigania katika maisha yangu.
Natamka haya kwa dhati ya moyo wangu, ahsante baba!....