arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 15.09.2007

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Sherehe za kusimikwa ka ...
» NILIFANYA MAPENZI NA MA ...
» Aina 10 ya vyakula vina ...
» Ze Comedy waua!
» SHED NO MORE TEARS GENE ...
» OOOSHI! NITAMU SANA
» Gadner Habash amtosa La ...

 

Waraka wa Shigongo kwa wasomaji wa gazeti la Ijumaa

ijumaa  

Waraka wa Shigongo kwa wasomaji wa gazeti la IjumaaNdugu wasomaji,

Naomba nichukue nafasi hii, kwa niaba ya kampuni, nikiwa Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti pendwa ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Risasi, Amani na The Bongo Sun. Pia kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hii, nachukua fursa kuwaomba radhi ninyi wasomaji kwa kilichotokea katika habari na picha zilizochapishwa kwenye gazeti la Ijumaa la tarehe 14, Septemba, 2007, chini ya kichwa cha habari WABAMBWA!

Asubuhi na mapema siku ya Ijumaa baada ya gazeti hilo kutoka, nilianza kupokea simu kutoka kwa wasomaji wengi wanaotutakia mema wakidai habari hiyo ilikuwa ni ya kweli lakini haikutokea nchini Tanzania kama tulivyoandika, bali nchi jirani na kwamba ziko kwenye mtandao. Simu hizo zilinishtua sana, nikalazimika kulitafuta gazeti hilo ili nisome na kuona kama taarifa nilizopewa zina ukweli wowote.

Baada ya kuziona picha hizo na kuisoma habari husika, nilichofanya ni kumuita mhariri wa gazeti hilo na kutaka atoe maelezo juu ya malalamiko yaliyotolewa na wasomaji wetu. Katika maelezo yake, mhariri alidai habari hiyo ililetwa na chanzo cha habari ambacho siku zote tumekuwa tukifanyanacho kazi na kukiamini. Kwa mujibu wa chanzo hicho, tukio hilo lilitokea maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kikafanikiwa kupiga picha hizo na kuzileta ofisini kwetu na kudai malipo ya shilingi 200,000 (laki mbili) zilizotakiwa kulipwa siku ya Ijumaa baada ya gazeti kutoka.

Kufuatia utata huo, niliagiza chanzo hicho kuhojiwa kwa mara nyingine kama kweli picha hizo zilipigwa Mabibo na yeye ama la, jambo hilo lilifanyika na awali katika maelezo yake, chanzo kilisisitiza kuwa picha hizo alizipiga yeye katika eneo hilo, lakini baadaye alipobanwa kwa maswali mengi ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa picha kama hizo zilizotumwa kwetu kwa njia ya mtandao na msomaji aitwaye Anna, alikiri kudanganya kwa lengo la kujipatia fedha!

Kwa kweli, jambo hili, mimi binafsi pamoja na wenzangu katika Global, limetuumiza sana, kwani kwa muda mrefu yamekuwepo madai kwamba habari tunazoandika siyo za kweli, lakini mara nyingi tumefanikiwa kuwathibishia wasomaji wetu kuwa hatuandiki uongo. Ndani ya miaka kumi tunayokaribia kuimaliza, hata siku moja hatujawahi kupata tatizo la aina hii! Hii ni mara ya kwanza, tunakiri kosa hili na tumeshaelewa tatizo letu, tunaahidi kuwa makini zaidi siku nyingine ili tusiudanganye tena umma wa wasomaji wetu wanaotuheshimu na kununua magazeti yetu kila siku.

Zipo hisia kwamba, chanzo hiki kilikuwa kimetumwa na maadui zetu kwa lengo la kutushushia heshima. Jambo hili bado tunalifanyia kazi, lakini tunachokifahamu ni kwamba mwisho wa vita vilivyopo tutashinda tu kama ninyi mtaendelea kusimama na sisi na kutukosoa pale tunapokwenda vibaya. Kumbukeni “to grow economically you need friends, but to develop economically you need enemies, so enemies are important for us to develop.”

Hatua makini zimechukuliwa kwa chanzo hiki, kisingeweza kuachwa kiondoke huru baada ya kuwa kimetuumiza kiasi hiki. Kinachoendelea wakati tunaandika waraka huu, ni kwamba Bw. Anos Magongo Rugahimkamu (pichani chini)yuko Kituo cha Polisi Msimbazi, alikamatwa siku hiyo hiyo ya Ijumaa na kufikishwa kituoni ambako alifunguliwa kesi namba MS/RB/10757/07 ya kujaribu kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu. Anategemea kufikishwa mahakamani Jumatatu.
Waraka wa Shigongo kwa wasomaji wa gazeti la Ijumaa
Hizi ndizo hatua tulizozichukua, pamoja na yote hayo, hakuna jambo lolote ambalo muungwana anaweza kusema baada ya kukosea zaidi ya kuomba msamaha! Kwa niaba ya wenzangu, tunaomba mtusamehe na tunaahidi kuwa makini sana siku nyingine. Ni matumaini yetu mtakubali kufanya hivyo. Kumbukeni hili ni kosa letu la kwanza na sisi ni ndugu zenu, tumetoka nanyi mbali miaka kumi iliyopita, TUPENI NAFASI NYINGINE.

Mungu awabariki sana.
Ahsanteni
Eric Shigongo James

NB: Hatua makini pia zimechukuliwa dhidi ya Mhariri.
    (15 September 2007)
Views: 4590 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Mpakanjia atoweka

risasi jumamosi  
Mpakanjia atowekaNa Mwandishi Wetu

Mfanyabiashara maarufu Mohamed Mpakanjia au Meddy ametoweka nyumbani kwake tangu atoke hopitalini hivi karibuni, Risasi limedokezwa.

Kutoweka kwa Mpakanjia kumejulikana hivi karibuni baada mwandishi wetu kufika nyumbani kwake ili kutaka kumjulia hali kutokana na tatizo lake la kiafya pia kujua ukweli kuhusu madai kuwa alikuwa amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.........
    (15 September 2007)
Views: 2636 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

I am back to hell (Nimerudi kutoka kuzimu -3)

hadithi za Shigongo  
Kijana mchafu, mwenye nywele zilizojisokota ambazo watu wengi huziita rasta amekutwa kwenye makaburi ya Kinondoni akifukua kaburi la kiongozi wa zamani wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sebastina Masaniwa aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

Walinzi wawili walikuwa wamekufa kando ya kaburi hilo kwa kuchomwa visu vifuani, maaskari waliomkamata wanaamini kijana huyo ni aidha mshirikina aliyekuwa akifatuta viungo vya wanadamu kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za uchawi au mwendawazimu ingawa yeye kijana huyo aitwaye Prosper analikataa kabisa jambo hilo na kudai anajua anachokifanya.

Polisi wanamchukua hadi kituo cha Polisi cha Kati ambako ilipogundulika kuwa kijana huyo ni Prosper Lufungulo kila mtu alishtuka kwani Tanzania nzima ilielewa mtu mwenye jina hilo alikuwa mfungwa kwenye gereza Makerebe lililopo kando ya bahari ya Hindi barabara ya kuelekea Bagamoyo na alikufa kwa kuzama maji yeye na wafungwa wenzake walipokuwa wamekwenda kuteka maji ya kunywa na maiti yake haikuonekana.

Hata hivyo anahojiwa na kuendelea kukiri mauaji ya watu wawilia hakubaliani kabisa na suala la uchawi! Wengi wanaamini ni mtu aliyechanganyikiwa hivyo kumpeleka hospitali ya Muhimbili ambako baada ya uchunguzi ilithibitika hakuwa na tatizo lolote la akili hivyo daktari alishauri afikishwe mahakamani kupambana na mkono wa sheria kwa mauaji ya kinyama aliyoyatenda.

Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (15 September 2007)
Views: 689 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

'The Hidden Truth 60'

hadithi za Shigongo  
Dhamiria ya wakili Dk. Ishengoma ni kuhakikisha Nyakutengwa ambaye ni mume wa Samantha anafia jela ili yeye ampate mke wake na hatimaye utajiri aliourithi.

Akitaka kumuua, anatuma chakula chenye sumu mahabusu ambako Nyakutengwa ananusurika kifo baada ya kuitwa
na Mkuu wa gereza, rafiki yake Thobias ndiye anakula chakula hicho na kufa kwa sumu.Uchunguzi ulipofanyika baadaye, ilibainika mtu aliyekileta chakula alitumwa na Samantha, akakamatwa na kufikishwa polisi. Jambo hili limemuumiza sana Nyakutengwa ambaye anaamini

mke wake alitaka kumuua. Je, nini kinaendelea?
    (15 September 2007)
Views: 736 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Ndoa na mabadiliko (3)

Mahaba  
Tupo ndani ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tuwe na staha katika kipindi hiki cha
ibada ambayo ni moja ya nguzo tano za Dini ya Kiislamu.

Sisi sote ni ndugu, kwahiyo kama wewe si mwislamu, basi ni busara kujua nini ndugu zako
hao wanatakiwa kufanyiwa katika mwezi huu, wasaidie kuepukana na vishawishi, kwa kufanya .............
    (15 September 2007)
Views: 558 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

WABAMBWA KWENYE TENDO!

ijumaa  
Uongozi wa gazeti la ijumaa unatoa taarifa maalumu kuhusiana na habari iliyochapishwa kwenye toleo lake la jana muda mfupi ujao.. tafadhali fuatilia!
    (15 September 2007)
Views: 1492 | Maoni (8) |
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com