Na Waandishi Wetu Afisa Elimu wa wilaya moja iliyopo Kanda ya Kusini ( jina lake na wilaya vimehifadhiwa), amepata aibu kubwa baada ya kubambwa akigandamiza raha na dogodogo katika chumba alichopanga na mkewe kwenye hoteli moja kubwa iliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam.....
Na Dotto Mwaibale Wasichana wanne wanaodaiwa kufanya biashara ya ukahaba maarufu kama changudoa, hivi karibuni waligoma kuondoka katika nyumba moja wanayoishi Wachina iliyopo karibu na Hosteli ya Mabibo jijini Dar e s Salaam, wakidai walipwe shilingi 200, 000 kama ujira wao baada ya kufanya mapenzi usiku mzima na raia hao wa kigeni......
Kijana Prosper Lufungulo ameua watu wawili, walinzi wa kaburi la Kiongozi Sebastian Masaniwa lililoko Kinondoni na kuanza kuchimba kaburi hilo mpaka alipolifikia jeneza na kuanza kutupa mabaki ya marehemu nje.
Baadae anakamatwa na polisi na kufikishwa Mahamani ambako amekiri mauaji lakini anakanusha kujihusisha na mambo ya kishirikina na kumuomba jaji kabla hayamhukumu kifo, kwanza asikilize historia ya maisha yake. Je nini kilimfanya kijana huyo awe katili? SONGA NAYO......
Assalam alaikum mpenzi msomaji wangu wa safu hii ya mahaba ,nikitumaini umzima wa afya na ukiwa kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na Swaum ikiwa ndiyo utaratibu wako kwa muda huu hususan kwa ndugu zangu waislam Mungu awape nguvu ili muweze kuvishinda vishawishi vinavyo wazunguka katika maisha yenu ya kila siku....
By The Bongo Sun Investigative Reporters. ANGAZA, the much touted and trusted government HIV testing agency can simply sell a client a clean bill of HIV at 20,000/- without one actually undergoing the blood test, The Bongo Sun can reveal.
This paper has learnt that there is an established network of people in the city involved in forging HIV “negative” certificates for people who may need them for all kinds of needs, ranging from marriage, school admission and foreign travel, and the well-connected culprits are linked with officials of trusted agencies like Angaza, as well as private and government hospitals.
This time The Bong Sun investigative reporter said she wanted the ‘clean’ certificate to facilitate her travel toYemen. “This is a very little problem. I have telephone contacts of two medical doctors. I will give them to you; you will get your certificate this same day” said a link person whom The Bongo Sun had earlier approached after being tipped by trusted sources...........
The retirement of the national team “Taifa Stars” Mecky Mexime has definitely shocked many soccer stakeholders in the country.
This happened few days ago when the calm and strong defender presented his will of quitting playing for Taifa Stars after serving for eight straight years as the team captain, which makes him the longest serving captain in history.....
Following his second escape to go out of BBA, Tanzanians now want their representative, Richard, to come home with the money and not otherwise.
Speaking to The Bongo Sun, the fans who were following the eviction session step by step, said that at first they were worried but the tension has come down when the votes dropped upon Max of Zambia. .....
Na Elvan Stambuli Siri nzito imefichuka kuwa ajali iliyompata Mbunge wa Mchinga, Mhe. Mudhihir Mudhihir imetokana na madai ya kuombewa dua mbaya na shehe mmoja jijini Dar es Salaam.
Wakiongea na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam, walisema Mheshimiwa Mudhihir aliombewa dua mbaya na shehe huyo siku ambayo wapinzani walikuwa wakimpokea Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe katika Viwanja vya Jangwani.....
Nilizaliwa katika familia ya kikristo na kulelewa katika maadili hayo hayo ingawa baadae enzi zile za shule nilianguka na baadae kusimama tena. Ni kawaida yetu wanadamu kuanguka na kusimama hakuna hata mmoja wetu ambaye katika maisha yake hajawahi kuanguka, kibaya ni kuanguka na kubaki chini ndugu zangu!
Wakati ule nikiwa mjinga nilikisoma kitabu cha Mungu, Biblia kama "Novel" nikiziona hadithi zote nilizozikuta ndani yake juu ya watu kama Ayubu, Mathayo, Mussa, Ibrahim, Yakobo nk. kama simulizi tu za watu walioishi zamani, kifupi kama hadithi ya sungura na fisi na baada ya kusoma yote yaliishia hapo, hakika sikujifunza kitu chochote kile katika kusoma kwangu.
Lakini ndugu zangu, leo hii mambo ni tofauti, kila ninaposoma Biblia najifunza jambo kubwa, naamini kila andiko la Mungu lina pumzi yake! Hakuna swali lolote katika maisha ya mwanadamu lisilo na jibu ndani ya vitabu vya Mungu! Huu ndio ukweli..........
Inajulikana kidini kwamba mtu akifunga anapata thawabu, hilo halina mjadala na pengine waumini wa dini zote, hufunga ili kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini tunapaswa kujua kwamba kufunga kuna faida kubwa kiafya na pengine Mungu alituamrisha kufunga siyo tu tupate thawabu, bali pia tuboresha afya zetu.
Katika makala haya, tutazungumzia faida za kufunga kiafya kama vile ambavyo zimethibitishwa na wanafasayansi mbalimbali duniani waliofanyia utafiti suala hili. Baadhi ya watu wanaamini kufunga kuna faida kiroho zaidi kuliko kimwili, kwani kwa mtizamo wa kawaida, mwezi mtukufu wa Ramadhani unapoingia kama hivi, Waislamu dunaiani kote hufunga ili kutekeleza moja kati ya nguzo tano za Uislamu. Halikadhalika kwa Wakristu, hufunga Kwaresma kama ibada.
Msichana wa Kimasai, Liti Olemorieti aliyekulia kijijini Sagun, anakutana na bahati ya ajabu maishani mwake na kuolewa na mfanyabiashara tajiri aitwaye Leonard Osborn aliyekuja Afrika kutafuta mke wa kuoa baada ya kuishi muda mrefu bila mke wala watoto. Mzee huyu ni mafia, aliyepata utajiri wake kutokana na biashara ya dawa za kulevya. Ni mtu asiye na huruma linapokuja suala la kutoa uhai wa mtu, yote hayo Liti hayafahamu anaishi ndani ya jumba kubwa la mzee huyo akifanyiwa kila kitu kama Malkia.
Maisha ya Liti yanabadilika kabisa, wataalam wa ngozi, urembo, lugha ya Kiingereza pamoja na mavazi wanakodishwa kuja kumfundisha kila kitu ndani ya nyumba ili siku akitoka watu wachanganyikiwe, hilo linafanyika na siku Liti alipotokeza nje, watu wote waliomwona hawakuamini kuwa ndiye yule waliyemwona uwanja wa ndege akiwasili kutoka Afrika, uzuri wake ulikuwa umeongezeka maradufu! Kila alipokwenda kamera na waandishi wa habari walimfuata, akayatawala magazeti yote ya Marekani na Uingereza, hakika alikuwa mbinguni.
Ghafla nyota wa Hollywood wakaanza kuvutiwa naye, hawakutaka kukubali kabisa kuwa msichana mzuri kama huyo eti alikuwa mke wa mzee Leonard Osborn, mwanaume mwenye sura ngumu ya kutisha ambaye hakika kilichomsaidia ni utajiri wake. Wengi waliogopa kumfuata Liti kwa kumwogopa Osborn, sifa zake zilitisha.
Kijana mmoja tu, hakurudi nyuma, huyo alikuwa ni Tevin Edmond, huyu alifikia mpaka hatua ya kumpigia simu Liti na kumweleza alivyompenda na kwamba alitaka kumuoa, mwisho alimfananisha Osborn na Nguruwe! Aliyasema maneno yote hayo bila kuelewa Osborn alikuwa akimsikiliza, kwani alikuwa amewekwa kwenye kile ambacho wenye simu hukiita 'loudspeaker' Wiki moja tu baadaye, Liti akipitia magazeti ya Marekani, alishangaa kukutana na habari ya Tevin Edmond, alikutwa ufukweni mwa bahari amekufa! Mshtuko huo ulimfanya ageuke na kumpa mume wake taarifa. Je,
Mungu ni mkubwa, ni mkubwa kwa sababu bila nguvu zake leo tusingekutana katika safu hii maridhawa ya kupashana mambo mbalimbali ya uhusiano na mapenzi. Karibu tujifunze pamoja!
Huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, inatupasa kuachana na dhambi na kuwa makini katika mwezi huu mtukufu. Umeingia salama, basi tuuache uishe salama huku tukitumia nafasi hii kuomba toba kwa Mwenyezi Mungu Subhana Wataalah! Kama una mambo yako yasiyofaa, hebu pumzika kwanza katika mwezi huu, naamini kwa uweza wake Maulana, hata baada ya kuisha utaendelea kuwa na tabia njema kama binadamu kamili.
Somo letu ni juu ya mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia katika ndoa. Tulianza tangu wiki iliyopita, leo tunamalizia kipengele kilichosalia. Kabla ya kuingia katika ndoa lazima ujiulize swali lifuatalo..