Na Dotto Mwaibale Binti mmoja ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mkuranga iliyopo Mkoani Pwani, Bi. Leah Saisai Aminiel amenusurika kufa baada ya Daktari aliyekuwa akimfanyia operesheni ya kujifungua kudaiwa kusahau vipande vya bandeji tumboni.....
Na Makongoro Oging’ Wanafunzi nchini wametakiwa kuacha tamaa ya pesa, badala yake wajitahidi katika masomo ili kuepuka na maambukizi ya magojwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi......
Nina imani wasomaji wangu wote ni wazima wa afya njema na mnaendelea vizuri kabisa na majukumu ya kila siku, hususan ya kusukuma gurudumu la maisha ambalo bila shaka ni gumu kusukumika!
Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru Mungu wangu wa mbinguni, kwa uaminifu wake mpaka kufikia hapa nilipo. Ninaamini hata wewe unayesoma makala haya, yapo mambo mengi ambayo Mungu amekutendea na una wajibu wa kumshukuru! Tamka kimoyomoyo 'Ahsante Mungu!' kabla ya kuendelea na mada yetu ya leo.....
Juzi nilikuwa napita maeneo ya Magomeni nikiwa ndani ya gari ghafla gari iliyokuwa mbele yangu ilipasuka tairi na kitoa mlio mkubwa ajabu! Nilichokishuhudia ni watu wote waliokuwa jirani na eneo hilo kushtuka, wengine mabega yakapanda juu kidogo, wengine vichwa vikaenda pembeni na baadhi wakataka kukimbia, mimi mwenyewe nisiwaseme wenzangu tu, nilitaka kuachia usukani wa gari kwa hofu na mapigo yangu ya moyo yakabadilika! Kifupi niliogopa, baadaye nilipogundua kuwa ni tairi la gari ndilo lililopasuka nilijiona muoga!......
Dan aliondoka Sagun akiwa amevunjika moyo kabisa, alijisikia mwenye bahati mbaya kuliko mtu mwingine yeyote. Isingewezekana hata kidogo mwanamke wa kwenye ndoto zake awe ameolewa na mwanaume mwingine, hakika hakuweza kuyazuia machozi kiasi kwamba dereva aliyekuwa naye ndani ya gari alilazimika kumuuliza kama alikuwa ana msiba na Dan akamsimulia kila kitu.....
Na Julius Kihampa, Tanga HUU ni mwaka wa kufa vigogo, kama huamini waulize Yanga kwamba juzi walifanywa nini na Ashanti United, usiporizika basi bisha hodi Msimbazi, Simba watakueleza ukweli walivyotendwa na Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.....
Na Adolph Balingilaki, DSM TIMU ya Ashanti United ‘Wauza Mitumba wa Ilala’ imesema ushindi wa Klabu ya Yanga ni kupitia vyombo vya habari hususan ni magazetini na siyo uwanjani.....
Na Immaculate Masanja, DSM BAADA ya timu Yanga ( pichani) kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watoto wa mjini, Ashanti United, uongozi wa Wanajangwani hao umekiri kuzidiwa uwezo katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro....
PAZIA la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara lilifunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja mbalimbali nchini. Kuanza kwa kinyang’anyiro hicho ni ishara kuwa, wakati wa wachezaji, makocha na waamuzi kuonesha makali yao umewadia.....
Na Elvan Stambuli SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), wiki iliyopita lilitangaza hadharani mkataba walioingia na wadhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Ni vema kuwakumbusha viongozi wa TFF kwamba wawe wazi kwa kila hatua wanapofanya mambo yao ya kuendesha Ligi Kuu, kwa kuwa wamekalia viti hivyo kwa manufaa ya umma wa Watanzania....
Na Julius Kihampa UKIUCHUNGUZA kwa kina usajili wa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, utagundua kuwa, katika kila kikosi kuna wachezaji wengi ambao ni mara yao ya kwanza kutia mguu katika michuano hiyo....
Na Imelda Mtema UPO usemi wa wahenga usemao ivumayo haidumu, ndivyo ilivyo kwa warembo wengi wa Tanzania, kwa kuwa majina yao huvuma wakati wakiwa na kofia ya tasnia hiyo, wanapoikabidhi kwa warithi wao huo ndio unakuwa mwisho wa kuwa ‘matawi ya juu’......
KATIBU Mkuu wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), Eugen Mwasamaki ametoa kali ya mwezi wa Ramadhan baada ya kutinga ofisini akiwa amelewa.
Tukio hilo lisilo la kistaharabu kwa kiongozi wa soka kama huyo, lilitokea Alhamisi ya wiki iliyopita katika ofisi za Shirisisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo Karume jijini Dar es Salaam.....
MSHIRIKI wa Tanzania katika shindano la Big Brother Afrika (BBA), Richard ameshindwa kujinasua katika mikono ya kimwana wa Angola, Tatiana. Tatiana amekuwa bega kwa bega na Richard huku akijaribu kutafuta njia ya kumhadaa akubali kumpa penzi.....
Hii ni wiki ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, swaumu inaendelea, pamoja na hivyo, nakuomba unipe nukta chache ili tuwezekuzungumza mapenzi. Love and Marriage ndiyo uga unaotuunganisha.
Matoleo mawili yaliyopita, nikiwa na maana ya Championi Jumatatu na Ijumaa nilikuwa nikidadavua mada ihusuyo namna ya kudumisha penzi la siri.....