
Mai na Benny walibambwa na kamera yetu Septemba 23 mwaka huu wakiwa wamekumbatiana kimahaba ndani ya ukumbi huo, jambo lililowafanya baadhi ya watu waliokuwa wakiwatazama kuhisi kuwa, huenda wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.
Ilidaiwa kuwa, watangazaji hao walifika pamoja ukumbini hapo kwa kutumia gari dogo aina ya baluni majira ya jioni na kwenda kuketi meza moja kabla ya kuagiza vivywaji na kuanza kubadilishana mawazo.
“Walifika pamoja wakakaa meza moja lakini kadiri muda ulivyozidi ndivyo walivyozidi kuonesha vioja, kuna wakati walikumbatiana na kubusiana,” alisema mtoa habari wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Aliongeza kuwa, baada ya kujiachia kwa bashasha za wazi watangazaji hao waliongozana tena hadi kwenye gari lao walilokuwa wameliegesha kando ya ukumbi huo ambako waliendelea kukumbatiana kama picha ya ukurasa wa mbele inavyoonesha.
Tukio hilo limetokea siku chache baada ya kuwepo kwa madai kuwa Maimatha alikuwa ametoswa na mchumba wake ‘Paff Daddy’ baada ya kutokea kutoelewana baina yao, hata hivyo habari hiyo ilikanushwa baadaye na wachumba hao.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya watu waliowashuhudiwa walinong’ona kwamba huenda mtangazaji huyo wa kike anatafuta mrithi wa penzi la mchumba wake aliyedaiwa kumpa kisogo.
Hata hivyo mwandishi wetu alipomtafuta Maimatha ili kujua kilicho nyuma ya pazia baina yake na Benny alisema, "Eh, sema Mai jina langu, Didy Mume wangu na Afro Beat kipindi changu,kinakushangaza nini kuona mimi na Benny tumekumbatiana, mume wangu hana mashaka naye wewe macho yanakutoka vipi?
“Kwani kuna mtu hamjui Beny kama ni mfanyakazi mwenzangu, tatizo liko wapi ina maana siruhusiwi kufanya mambo yangu binafsi,” alisema Mai kwa nyodo.
Naye Benny alipoulizwa juu ya hilo alisema kuwa anamheshimu Mai kama dada na mfanyakazi mwenzie na kwamba hayuko tayari kumvunjia heshima yeye pamoja na mume wake anayemchukulia kama mtu wake wa karibu.
“Kukumbatiana ni ishara ya kufurahi tu, siku hiyo tulikuwa na furaha, michongo (mipango) yetu ilifanikiwa tukakamata pesa za kutosha,” alisema Benny huku akimtaka mwandishi wa habari hizi kutomchonganisha na marafiki zake muhimu.