Na Hamida Hassan Miss Tanzania namba tano, mwaka 2006, Irene Uwoya, ameonekana kuwadatisha wanaume wengi wakware kutokana na umbo lake lenye mvuto wa aina yake. Wanaume hao ambao wamekuwa wakilipigia simu gazeti hili kwa muda mrefu, walisema kuwa mbali ya kudatishwa na umbo, pia sura ya mrembo huyo ni alama nyingine ‘inayowakong’oli’ kupita kiasi.
Fatma Amri na Rehema Sapali P amoja na dua za kuwatakia heri Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Juma Kapuya na Mbunge wa Mchinga (CCM), Mudhihir Mudhihir kuendelea kumiminika, fikra za Watanzania bado zinauliza kwanini (why), juu ya ajali zilizowakumba viongozi hao...
Na Issa Mnally Sherehe ya kutimiza umri wa miaka 19 ya Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, ilikuwa kufuru, kutokana na kutawaliwa na vituko kemu kemu, wakati wa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani...
Na Richard Bukos Kundi la vichekesho la Ze Comedy, mwishoni mwa wiki iliyopita liliua sherehe ya uzinduzi wa mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi, zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar- es Salaam.
Ze Comedy ambalo huonesha vichekesho vyao kupitia Luninga ya EATV, liliua uzinduzi huo muda mfupi baada ya kupanda jukwaani kutokana na kusababisha vurugu kubwa iliyohatarisha maisha ya watu......
Najisikia furaha sana moyoni mwangu, furaha hiyo inatokana na uzima niliojaliwa na Mungu. Karibuni tujifunze jinsi ya kuwa bora zaidi katika uhusiano wetu na wachumba ama ndoa zetu. Kila kitu kinawezekana tukikubali kujifunza. Kama kuna kitu kinachouma zaidi katika uhusiano ni kuachwa, hasa kama ulikuwa una mapenzi mazito juu ya mwandani wako........
Laibon alikuwa na akili nyingi kuliko kawaida, alichokifanya alipokuwa nyumbani kwa rafiki yake Milkov katika Jiji la Moscow, Urusi ni kujifunza kuogelea baharini! Hakuwa na haja na mashindano wala umaarufu, alifanya hivyo akiwa na lengo la siku moja kuzamia hadi kwenye Meli ya St. Petersbugy, akiamini kama asingefanikiwa kuwaona ndugu zake, basi utajiri wa madini ungekuwa halali yake.........