Na Mwandishi Wetu BAADA ya kuitema Klabu ya Yanga, Agosti mwaka huu, aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho' anaviziwa na watani wao wa jadi Simba, imefahamika. Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Ndogo ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), Micho aliuaga uongozi wa klabu hiyo kuwa anakwenda Serbia kutibiwa, lakini baadaye aliitema timu hiyo akiwa kwao...
Na Adolph Balingilaki SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema Tanzania imepanda nafasi tatu juu katika viwango vya Shirikisho la Soka duniani (FIFA).
Akizungumza na Championi ofisini kwake Karume jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema kuwa kiwango hicho kimepanda baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) katika mechi ya kimataifa ya kirafiki...
Na Chausiku Omary KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Kondic Dusan amesema kuwa zoezi la kupima afya za wachezaji limemfumbua macho kwa kuweza kubaini matatizo makubwa...
NA Fatma Amri KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema mchezaji, Edwin Mukenya kurudi Yanga itakuwa ni ndoto kwa kuwa ana mapenzi binafsi na timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam...
Na Mwandishi Wetu KESHO si ndiyo Desemba mosi? Ndiyo, CCM Kirumba hakutakamatika, kuna nini? Wanamuziki wa Kizazi kipya wenye asili ya Mwanza wakishirikiana na mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha wanatarajiwa kuwasha moto...
Kijana mtanashati, Osward mwenye mafanikio makubwa na mcha Mungu, anakutana na msichana mrembo aitwaye Jennifer. Siku zote amekuwa na msimamo mkali juu ya uhusiano na wasichana kimapenzi, hiyo ndiyo ilikuwa sifa yake kubwa lakini baada ya kukutana na Jennifer kwenye taa za Morocco, msimamo wake uliyumba akajikuta katika mapenzi mazito na msichana huyo mwenye mvuto mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi iitwayo Outreach...
Kijana mtanashati, Osward mwenye mafanikio makubwa na mcha Mungu, anakutana na msichana mrembo aitwaye Jennifer. Siku zote amekuwa na msimamo mkali juu ya uhusiano na wasichana kimapenzi, hiyo ndiyo ilikuwa sifa yake kubwa lakini baada ya kukutana na Jennifer kwenye taa za Morocco, msimamo wake uliyumba akajikuta katika mapenzi mazito na msichana huyo mwenye mvuto mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi iitwayo Outreach...
Ni ukweli ambao haupingiki kuwa muziki ni moja kati ya ajira ambazo zimewatoa vijana wengi kimaisha. Kwa maana hiyo kazi hii inayobeba jina la sanaa, ni bora ikaheshimiwa na pengine kuwekewa misingi imara na serikali yetu, ili wafanyakazi wake wafikie malengo yanayotarajiwa.
Unaposimama mbele ya hadhara katika uga wa nchi yetu na ukataja neno muziki achilia mbali wa kizazi kipya au Bongo fleva utakuwa umetaja mfereji wa wazi kabisa wa pesa miongoni mwa watanzani walio wengi...
UNAPOZUNGUMZIA soka la wanawake hapa nchini, huwezi kuliacha jina la mchezaji Ester Chabruma ambaye mashabiki wa soka walimpachika jina la Lunyamila kutokana na kukifananisha kipaji chake na aliyekuwa mchezaji wa Yanga Edibilly Jonas Lunyamila...
Mungu aliyeumba mbingu na ardhi, ndiye aliyenipa ubavu wa kuitumia safu hii kama uwanja wa kutoa elimu kwa wengi. Ahsante Bwana, wewe ndiye kila kitu maishani mwangu...
Mfanyabiashara maarufu wa jijini Dar es Salaam, Mohamed Mpakanjia ‘Medy’ hivi karibuni amepasua jipu baada ya kusikia habari kuwa aliyekuwa mkewe, marehemu Amina Chifupa, amewekwa msukule katika shamba moja lililopo Kibaha, mkoani Pwani.....
Mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania 1999, Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyin, hivi sasa amedatishwa na penzi la mwanamuziki mwenzie Kheri Samir maarufu kama Mr Blue.
K-Lyn anaonekana kudata na penzi la bwana mdogo huyo ndani ya video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nipe mkono (Miamore) ambao amemshirikisha mwanamuziki huyo.....
Ingawa kuna madai kuwa Big Brother Richard Buzueidenhout kamaliza bifu kiana na Mkewe Ricki ambaye alikerwa na kitendo chake cha kujihusisha kimapenzi na Tatiana wa Angola, imedaiwa kuwa bado ana mawasiliano mazito na Muangola huyo Ijumaa limedokezwa.....
Digo, muuaji aliyetumiwa na Tina Richard pamoja na mwanae John Gurvey kuwaua watu mbalimbali waliosababisha kampuni yao ya Black American Media Group kukosa mikataba ya matangazo na kuchukuliwa na Broadway Media inayoongozwa na Natalia, amekwenda kanisani kutubu dhambi zake kwenye kitubio lakini padri aliyemsikiliza ambaye alifahamu mauaji yote aliyoyafanya, anatoa siri hiyo kwa hawara yake ambaye naye anazifikisha taarifa hizo polisi hivyo kulazismisha ofisi ya Black American Media ivamiwe na maaskari kwa lengo la kuwakamata Tina na mwanae John ili wahojiwe kwa mauaji ya watu wote waliotajwa.
Wakati taarifa hizo zinawafikia walikuwa ofisini kwa Mkurugenzi wao wa masoko Hellen, ambaye pia hivi sasa anamiliki asilimia nyingi ya hisa katika kampuni hiyo. Alichokifanya ni kuwatorosha kupitia mlango wa nyuma, lakini kabla ya hapo alifungua kabati na kutoa bastola pamoja na hati yake ya kusafiria. Safari yao iliwapeleka moja kwa moja hadi shambani kwa Hellen ambako aliwaingiza kwenye kibanda kidogo chenye shimo refu ndani yake! Wakiamini Hellen alikuwa mkombozi wao, ghafla mambo yanabadilika, anachomoa bastola yake na kuwalenga kisha kuwapa hati yake ya kusafiria waisome, iliandikwa jina la Tecla Jones! Akawakumbusha hapo hapo kuwa yeye ndiye mke wa Adrian Jones waliyemuua na kwamba aliingia kwenye kampuni yao si kupata kazi bali kulipa kisasi na siku ya kutekeleza hilo ilikuwa imefika.
Tina na mwanae hawakuamini walichokuwa wakikiona, wakamkumbuka Tecla Jones na kuukumbuka unyama waliomtendea mume wake. Wakijua Tecla angewaua na kuidumbukiza miili yao kwenye kisima kirefu alichochimba, walianza kumuomba msamaha lakini Tecla hakuwa tayari kufanya hivyo, kilichofuatia baada ya hapo ni milio ya risasi.
Amani ya Bwana Mungu, Yehova Mtakatifu iwe juu yenu nyote wapenzi wasomaji wa safu hii, leo tunaendelea tena na darasa letu la mapenzi. Leo tutakuwa tunaelimishana juu ya kumjua mtu anayekupenda na ambaye hakupendi.
Kwani nataka nieleweke kuwa si kila mtu anayekwambia ‘nakupenda’ huwa ana maanisha akisemacho. Wako watu husema nakupenda lakini kumbe ki dhati huwa anakutaka tu na si kukupenda.
Je, utajuaje kama hapa unapendwa au hupendwi na wote wametamka neno moja “nakupenda?” Kwa kawaida tumezoea kuwasikia wanaume ndiyo wakiwaeleza wanawake kwamba nakupenda katika kuanzisha mahusiano ya kimahaba. Ingawa wanawake pia wapo wanaojiamini kiasi cha kuthubutu kuwaambia wanaume nakupenda.....