arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » risasi jumamosi » Mrembo amfanyia kitu mbaya mzungu.

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Ndoa na mabadiliko (3)
» CNN MULTICHOICE AFRICAN ...
» Wanaigeria wa Miembeni ...
» Ambani nipo fiti 100%, ...
» Mgosi mchezaji bora,Nur ...
» Kama una upungufu wa ng ...
» MTOTO ATUMBUKIA SHIMONI ...

Mrembo amfanyia kitu mbaya mzungu.

risasi jumamosi

Mrembo amfanyia kitu mbaya mzungu.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika, tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati Fide alipokaribishwa kulala katika chumba cha mzungu huyo ambaye alikuwa safarini.

Habari zinasema kuwa mwanamitindo huyo alikwenda Zanzibar akiwa ameongozana na rafiki yake na kufikia kwa dada wa rafiki huyo ambako Fide alipewa chumba cha kulala, naye kwenda kulala sehemu nyingine.

“Chumba ambacho Fide alipewa kulala, kilikuwa kinatumiwa na mzungu huyo ambaye ni mume wa dada wa rafiki wa mwanamitindo huyo ambapo wenyeji hao walikuwa safarini nje ya Zanzibar,” alisema mtoa habari huyo.

Ilidaiwa kuwa katika chumba ambacho mrembo huyo alikaribishwa kulala, kulikuwa na kabati ambalo lilikuwa na dola za Kimarekani 1800 sawa na shilingi za kitanzania 2,156,400 ambazo zilichukuliwa na mrembo huyo.

Aidha, imedaiwa kuwa kulikuwa na shilingi 300,000 tasilimu za Kitanzania ambapo Fide nazo alizichukua usiku huo.

Mtoa habari huyo alisema kuwa mwenyeji wao huyo hakugutuka juu ya upotevu huo wa pesa hadi asubuhi wakati Fide na rafiki yake huyo walipoondoka kurejea jijini Dar es Salaam.

“Mke wa mzungu huyo aligutuka mchana alipokwenda kuweka sawa chumba alicholala Fide, ambapo alikutana na mabadiliko ikiwa ni pamoja na kulikuta kabati la nguo likiwa wazi na ndipo alipobaini kuwa fedha za mumewe zilibiwa,” kilipasha chanzo hicho.

Baada ya kubaini kuibiwa alikwenda katika Kituo kikuu cha Polisi Zanzibari kutoa taarifa na msako ulianza.

Hata hivyo, habari zinasema kuwa shemeji wa mzungu huyo hivi karibuni alitua jijini Dar es Salaam na kwenda katika kituo cha Polisi Oysterbay kumsaka mwanamitindo huyo lakini hawakufanikiwa.

Mwandishi wetu alikwenda katika kituo cha Polisi Oysterbay ambapo askari mmoja (jina tunalihifadhi) alimthibitishia mwanahabari wetu kuwa mwanamke huyo kutoka Zanzibar alifika kituoni hapo kumsaka mtuhumiwa wake.

“Ni kweli huyo dada alifika hapa kituoni na akiomba msaada wa kumsaka mtuhumiwa wake, nasi tunamsaidia,” alisema askari huyo.

Mwandishi wetu jana (Ijumaa) alimpigia simu Fide na kumuuliza kuhusu madai hayo lakini alisema kuwa hafahamu habari hizo.

“Wewe ni mwandishi wa chombo gani?” Aliuza Fide, alipojibiwa alisema “Sifahamu habari hizo.”


 (Votes #: 3)
    (26 January 2008)
Soma Zaidi: 2379 | Maoni Yako (5)

Udaku Mwingine

risasi jumamosi
 
  • Mwanamitindo Maarufu ageuka kituko makaburini
  • JAMANI, SINA BWANA WA KIZUNGU!!
  • Wakware wamezea mate matiti ya Fide
  • FIDE MCHAFU, AKAA UCHI MBELE YA WAZIRI SIMBA
  • MISS ANYWA SUMU
  •    

    #1 Author: leila (26 January 2008 10:31)

    hii kweli noma duh mpaka ufikie kuwiba ni balaha mkimpata mpatieni azabu hili wengine pia wasifanye,,
     
    fast    

    #2 Author: vonostust (26 January 2008 13:49)

    Hii sasda ni aibu kubwa me huwa nasema kila siku akinadadsa huwa na tamaa kubwa sana hata akipewa nini akiona kingine anatamani sijui ni kwa nini, mtu anweza kumtuma mke wake tena akampa fedha nyingi yaani za safari pamoja na za matumizi tena za kutosha kakini akimuona mwanaume atakayempa Tshs10,000.00 tu anafanya naye mapenzi. Sasa watu wanakufanyia wema wewe unaiba katafuteni mkaadhibu kametia aibu.
     
    fast    

    #3 Author: talib kweli (1 April 2008 13:39)

    oooh nyie vipi mnaishiii dunia gani???
    gefeliciteite!!!hongera dada yangu!!!
    ukipata nafasi kumziliza mjinga kama
    huyo safi sanaa coz wanakuja home
    wanaishi kama wafalme na kwao wanatutreat
    kama maslave vile ...
    yani big up sanaa acheni kubana kula kuku
    mwana!!!mjinga kashaliaaaaa....
     
    fast    

    #4 Author: Mwaddy (15 April 2008 12:17)

    Aibu mwanadada mrembo kama Fide kuwa kibaka
     
    fast    

    #5 Author: MARK.MUSHI WA ITALY (17 May 2009 13:18)

    SAFI SANA FIDE PER QUELLA CHE HAI FATTA SEI STATA UNA DONNA CORAGGIOSA,KWA KILE AMBACHO UMEFANYA UMEKUWA MWANAMKE SHUPAVU,HII NDIYO BONGO....,SASA KAMA ANGELALA NA MZUNGU UYO GAZETI ZIMA LINGEUZWA CHAPU CHAPU BADALA YAKE KAMZIDI AKILI MTASHA UYO BIG-UP FIDE,NANI ASIYEITAJI PESA KWA NJIA YOYOTE HILE,PESA HIZO KWANZA SI AJABU ATA WAKAWA WAMEIBA PIA WAFANYA KAZI WA HIKO CHUMBA YOTE YAWEZEKANA,KISHA LONGOLONGO NYINGI,AU PIA WATU WAMEPANGA DIRI HILI WAMDHALILISHE FIDE,KAMA IMEKUTACHI,NIANDIKIE,CHELSEAFORTE1@YAHOO.IT,NIKO ITALY,MDAU,MARK,
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi



    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

     hit counter

    counters

    2008 © globalpublisherstz.com