Na Mariam Mndeme Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa ambaye alijiuzulu nafasi hiyo kwa kuwajibika na Kashfa ya Richmond, amesema baada ya majaribu yote aliyoyapata ameamua kurudi nyumbani kwake Monduli, kwa lengo la kuendeleza mila na desturi za kabila lao za ufugaji....
Na Mwandishi Wetu Msanii maarufu nchini wa filamu na maigizo, Blandina Chagula `Johari`, amekanwa na anayedaiwa alikuwa mpenzi wake, MacDonald Mwakamele, aliyedai hajawahi hata siku moja kumtamkia neno la mapenzi....
Na Catherine Kassally Miss Utalii Dodoma mwaka 2005/06, Fania Hassan, hivi karibuni alizusha vurugu kubwa katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kuzidiwa na kilevi....
Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa, mapenzi yamegawanyika katika sehemu mbili zisizo rasmi, yaani maumivu na furaha. Kupata mateso au furaha katika uhusiano inategemea zaidi na wewe, jinsi ulivyoanzisha uhusiano huo, unavyoulea na hata staili unayoishi na mpenzi wako....
Gilbert amerejea kutoka Marekani alikokwenda kuchukua digrii ya pili ya mambo ya kompyuta na kuanzisha kampuni aliyoiitwa WorldCom, muda mfupi baadaye akiwa katika kilele cha mafanikio baada ya kuwa mtu wa kwanza aliyeuza kompyuta nyingi za Microsoft katika nchi za Afrika Mashariki, anamuoa Salome msichana kutoka Mwanza vijijini na kwa miaka kadhaa waliishi bila mtoto, lakini Krismasi ya mwaka 1998 Salome akiwa mjamzito wa miezi minane anaomba ruhusa kwenda kwao kuwaona wazazi wake kabla hajajifungua! Ingawa kwa shingo upande, Gilbert anamruhusu.
Anachelewa kurudi tofauti na walivyokubaliana, Gilbert akaanza kupiga simu akifuatilia lakini mawasiliano yakawa mabaya! Baadaye akaambiwa kwamba mvua kubwa imenyesha maeneo aliyokuwepo mkewe, madaraja yamevunjika na kuna mafuriko! Hakuna njia ya kutoka. Akitafakari nini cha kufanya ofisini kwake, ghafla anaingia askari kutoka kituo cha polisi cha kati na kumwambia alikuwa na habari za kusikitisha. Je, amekuja kumwambia nini? SONGA NAYO…
Baada ya ukweli kubainika kwamba Liki na John ni mtu na dada yake, mipango yote ya ndoa inasimamishwa! Kazi iliyobaki ni moja tu, kuokoa maisha ya mama yao ambaye kwa muda mrefu alikuwa mgonjwa wa kupooza lakini hivi sasa amepoteza fahamu baada ya kugundua Liki na John walikuwa wametoroka! Madaktari wamegundua kuwa sehemu ya ubongo wake imeharibika na matibabu hayawezekani mjini Khartoum.
John anamwomba mzee Laibon atumie uwezo wake ili mgonjwa asafirishwe kwenda Marekani, hapo ndipo ndege ilipodishwa na mgonjwa pamoja na wao wenyewe kusafiri hadi jijini Washington ambako mama huyo anafanyiwa upasuaji wa ubongo, damu iliyoganda chini ya fuvu inaondolewa na hali yake inabadilika ghafla na kuwa nzuri! Hapo ndipo John anamwita Liki pembeni na kumweleza ukweli kwamba, pamoja na majibu ya DNA kuthibitisha kwamba wao ni mtu na dada yake, bado alimpenda na alitaka kumuoa. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Kwa wasomaji wapya, kijana Nassor mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, alimuoa jini mahaba aliyekuwa akimsumbua kwa muda mrefu. Hata hivyo, hakuifurahia ndoa yake kutokana na tabia ya jini huyo kupenda kufanya mapenzi kila wakati. Kufuatia kero hiyo aliamua kumuacha ndipo jini huyo alikuwa akijigeuza mwanaume na kumwingilia Nassor kinyume na maumbile. Kufuatia adhabu hiyo, sheikh mmoja alimshauri arudiane na jini huyu ambapo alikubali.
Hata hivyo, jini Maimuna hakuacha tabia yake hiyo ambayo ilimkera sana Nassor. Kutokana na hali hiyo jini huyo alimweleza Nassor ni bora waachane ili akatafute mwanaume mwingine atakayeweza kumpa raha. Kabla hajafanya hivyo alimwambia anakwenda kuomba ushauri kwa baba yake.Je, Mzee Sharif ambaye ni baba wa jini huyo atakubali bintiye waachane na Nassor ambaye anampenda? Fuatilia mkasa huu wa kweli…
Na Mwandishi Wetu Zikiwa zimebaki saa 48 kabla ya Yanga kushuka katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kesho kutwa Jumapili kumenyana na As Adema ya Ethiopia, watabiri wa soka wa hapa wameipa timu hiyo ya Tanzania ushindi wa mabao 3-0...
Na Mwandishi Wetu Huku timu ya Simba ikiwa nchini Ethiopia tayari kwa pambano lao la marudiano dhidi ya Awassa City ya huko, mashabiki wa soka wa hapa waliliambia Championi kwamba, kwa sasa wanaiwazia Enyimba na si Waethiopia hao....
Rebeka Bernard na Hawa Mkombozi TIMU ya Taifa (Taifa Stars), inatarajia kushuka dimbani Machi 26, mwaka huu kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Msumbiji (The Mambas).....
Acha Mungua aitwe Mungu, kwani shani yake ni ya ajabu mno. Angetokea wapi binadamu bila idhini yake? Oksijeni inayotupa jeuri ya kutamba kwenye sayari hii tungeitoa wapi? Hayo ni maswali ambayo majibu yake hata mtoto wa chekechea anaweza kuyatoa.....
Ni msichana mrembo mno, mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Outreach! Tajiri ambaye utajiri wake haueleweki unatokana na nini kwani haulingani kabisa na pato lake! Wanaume wengi wanamwogopa wakiamini ni mwanamke wa watu wenye fedha ambao nao hawana habari naye.
Hakuna mtu hata mmoja anayefahamu kwamba Jeniffer si binadamu wa kawaida bali ni Jini aliyetumwa na wenzake kuja duniani kama wakala wa kuwakusanyia damu ambayo ni chakula chao! Anazo nguvu za kichawi machoni mwake ambazo huzitumia kuwaua watu, amekwishaua wengi tangu akisoma shule ya msingi na baadaye sekondari ambako alihama shule moja kwenda nyingine baada ya matatizo yake kugundulika.
Nchini Kenya alifukuzwa, akahamia Uganda ambako alimaliza kidato cha sita akarejea nchini na kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jeniffer hana mpenzi wa kiume kwani ni mke wa jini! Hatakiwi kuwa na uhusiano na mwanaume kimapenzi, akifanya hivyo mwanaume huyo atakufa! Mume wake jini ndiye humpa zawadi za madini ya Almasi na Dhahabu ambayo huyauza na kujipatia fedha nyingi, hivi sasa amenunua nyumba kubwa ufukweni mwa bahari ya Hindi karibu kabisa na nyumba ya Waziri Mkuu.
Mlezi wake, bibi Brigitte, ameingiwa na wasiwasi na kumtembelea Jeniffer nyumbani kwake ambako anambana ili aeleze siri ya utajiri huo! Je, atakuwa tayari kueleza? Kumbuka historia yote hii, Jeniffer anamsimulia kijana aitwaye Osward aliyejikuta katika mapenzi mazito na msichana huyo ingawa aligundua kabisa hakuwa wa kawaida. Nini kitaendelea leo? SONGA NAYO…
• Asema hakumtuma kuingia mikataba ununuzi wa jengo • Adai zilitengwa bilioni moja na si tatu.
ALIYEKUWA Katibu Mkuu Kiongozi, Marten Lumbanga (60), amemruka Balozi Costa Mahalu mahakamani akisema hakumtuma kuingia mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Lumbanga, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa nchini Uswisi, alidai hayo jana katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Mfawidhi sivangilwa Mwangesi.
Madai hayo aliyatoa alipotoa ushaidi katika kesi ya kuhujumu uchumi na wizi wa zaidi ya sh. Bilioni mbili inayomkabili Profesa Mahalu, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na aliyekuwa ofisa utawala wa ubalozi huo, Grace Martin,
Lumbago alidai akiwa katibu Kiongozi, alitumia nafasi hiyo kuishawishi serikali kununua jingo la ubalozi huo, baada ya Profesa Mahalu kwenda kumlalamikia kwamba anafanya kazi katika mazingira magumu.
Alidai Profesa Mahalu alimlalamikia kuwa hadi mtu afike kwenye ofisi za ubalozi, inabidi apite kwenye sebule ya nyumba ya mtu mwingine.
Lupanga alidai alichofanya yeye kutokana na malalamiko hayo ni kutoa pendekezo la kununuliwa kwa jengo la ubalozi.
Alidai hakuwahi kumpa maelekezo ya kuingia mikataba miwili katika ununuzi wa jingo hilo na hana taarifa zake, zaidi ya kesoma magazetini.
“Sikumpa maelekezo ya kuingia mikataba mwili na wala sihusiki na ununuzi wa jingo hilo.
“Nahusika kwa kuwa Mahalau alikuja ofisini kwangu kunipa habari za kusikitisha kwamba ukitaka kufika ofisini kwake lazima upite katika sebule ya mtu, nikatumia nafasi yangu kuishawishi serikali kwa kuwa kulikuwa na umuhimu wa kupata jengo, ili awe na mazingira mazuri ya kufanyia kazi,” alidai Lumbanga.
Akiongozwa na Mwendesha mashitaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) , Joseph Hole, alidai baada ya ombi la Mahalu kukubaliwa, serikali ilitenga sh bilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa jengo hilo, ingawa zilionekana hazitoshi kwa kuwa lilikuwa likiuzwa kwa sh. Bilioni tatu.
Balozi Lumbanga alidai baada ya kutolewa kwa fedha hizo, mwaka mmoja baadaye, Mahalu alimfuata na kumuomba amuunge mkono ili fedha ziongezwe, kwani kama angenunua jengo kwa sh. Bilioni tatu, angeweza kupata msamaha wa kodi.
Alidai alimueleza Mahalu kuwa suala la msamaha wa kodi si la serikali ya Tanzania hivyo ni vyema akawasiliana na serikali ya Italia ili asije kuvunja sheria za nchi hiyo.
Alihojiwa na wakili alex Mgongolwa anayewatetea akina Mahalu, Balozi Lumbanga alidai hakuwahi kupata taarifa zozote juu ya maandalizi ya ununuzi wa jengo hilo na mikataba miwili inayohusu ununuzi wake.
Lumbanga alizikana nakala alizokuwa akionyeshwa na Mgongolwa kwamba Novemba 11, mwaka 2005, alipata barua inayoonyesha Mahalu ameingia mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi kwa sh bilioni tatu.
“Hizi nakala sina kumbukumbu nazo na sijawahi kuziona wala hazijaletwa kwangu, labda kama zilipokewa na mtu mwingine, lakni si mimi,” alidai Lumbanga.
Alipoulizwa na Mgongolwa kuhusu kikao cha 39 cha Bunge kilichofanyika Agosti 3, 2004 kwamba Bunge lilithibitisha kuwa mkataba wa ununuzi wa jengo ni sh. Bilioni 2.9, Lumbanga alidai bajeti ya serikali ilikuwa ni sh bilioni moja na kama ziliongezwa zilikuwa jitihada za Maalu kutaka fedha nyingine za ununuzi wa jengo hilo.
Profesa Mahalu na Grace wanakabiliwa na mastaka sita ya kutoa taarifa za uongo ju ya ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Roma , Italia kwa lengo la kumdanganya muajiri, kughushi, kuhujumu uchumi, wizi wa zaidi ya sh. Bilioni mbili na kusababisha hasara kwa serikali.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machi 14, mwaka huu.
Na Mwandishi Wetu Tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya vigogo wa serikali nchini, zimemuingiza kwenye ulingo Rais Jakaya Kikwete na kumuweka katika wakati mgumu wa kupambana nao, uchunguzi wetu umebaini...
Na Mwandishi Wetu- Musoma Mwita Kimusa [37] mkazi wa Mugumu, wilayani Serengeti mkoani hapa anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumuua mkewe kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili....