arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for March 2008 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» Kwa nini wengine wanapa ...
» BREAKING NEWS:::: TIGO ...
» Nilivyobakwa na baba ya ...
» KARIBU KATIKA ULIMWENGU ...
» CONTRACTS MUST BE OPEN, ...
» CCM YASHINDA KITETO
» AFUNGWA KIFUNGO CHA MAI ...

 

MWAGA MIPESA

photos  
MWAGA MIPESAPedeshee maarufu jijini Dar es Salaam “Papaa Msofe" (katikati) akimwaga pesa katika jukwaaa la Akudo Impact Msasani Beach jijini DSM (Picha na Richard Bukos)
    (31 March 2008)
Views: 331 | Maoni (0) |

 

WATANGAZAJI WAPEKECHA PEKECHA

photos  
WATANGAZAJI WAPEKECHA PEKECHAWatangazaji wa Radio Clouds, Dina Marious(mbele) akiwa na Gerald Hando wakicheza mtindo wa pekechapekecha katika jukwaa la Akudo Impact jana usiku (picha na Richard Bukos)
    (31 March 2008)
Views: 353 | Maoni (0) |

 

Nembo ya Abuu Semhando wa Twanga!!

photos  
Nembo ya Abuu Semhando wa Twanga!!Nembo aliyoiweka mwanamuziki wa African Stars 'Twanga Pepeta', Abuu Semhando katika pikipiki yake imezua maswali mengi kwa watu. Nembo hiyo inaonyesha katuni ya mwanaume na mwanamke wakiwa uchi wakifukuzana, lakini alipoulizwa mwenyewe kisa cha kuweka nembo hiyo alisema kuwa hiyo ni Boliti ikiifukuza Nati. Wewe je unasemaje? (Picha na Issa Mnally).

    (31 March 2008)
Views: 304 | Maoni (4) |

 

Joto kali lakini Kahawa inanyweka jijini

photos  
Joto kali lakini Kahawa inanyweka jijini
Kutokana na ukosefu wa ajira vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na biashara mbalimbali kama kijana huyu alivyokutwa katika mitaa ya jijini Dar es salaam akitembeza kahawa (Picha na Issa Mnally)
    (31 March 2008)
Views: 201 | Maoni (0) |

 

MKAPA, YONA WALIVYONYAKUA KIWIRA

---  
MAKAKATI WAO ULIANZA IKULU DESEMBA 2004

NYARAKA zilizopatikana kwa uchunguzi zinabainisha mbinu zilizotumiwa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kunyakua kifisadi Mgodi wa Makaa ya mawe wa Kiwira wakati ukiwa mali ya umma chini ya Shirika la Taifa na Maendeleo (NDC).
MKAPA, YONA WALIVYONYAKUA KIWIRA
Nyaraka zimethibitisha wazi kwamba viongozi hao wawili wa serikali ya Awamu ya tatu ya Tanzania (1995-2005) walikula njama wakiwa Ikulu na kuunda kampeni yao binafsi iitwayo Tanpower Resources na kisha kuisajili rasmi Desemba 29, 2004, kabla ya kujinyakulia hisa binafsi nono katika Mgodi wa makaa ya Mawe wa Kiwira Mechi 2005.

Mgodi huo ulioko mkoani Mbeya hivi sasa unakamilisha mradi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 27.8 (takribani bilioini 340/-) wa kuzalisha umeme utakaouziwa Shirika la Taifa la Ugavi wa Umeme (Tanesco).

Kilikuwa ni kipindi kisichozidi miezi mitatu tu (Desemba 2004 hadi Mechi 2005) wao na kuwa matajiri wakubwa kwa kutumia Ikulu na nyadhifa walizodhaminiwa na umma wa wapiga-kura na walipa-Kodi wa Tanzania. Katka kutekeleza hatua hiyo Mkapa na Yona walihakikisha kampeni yao waliyosajili, inakuwa na wanahisa ambao ni familia zao, jamaa au marafiki wa karibu sana.

Nyaraka zinaonyesha kwamba mambo yalianza moto-moto kwa Daniel Yona kuandika barua akiwa Waziri wa Nishati na Madini mnamo Machi 24, 2005 kwa Evans Mpundi aliyepewa ukurugenzi katika kampuni yao – Tanpower Resources (T) Ltd. Namba CDA 48/171/01,

Yona anasema kwa Kiingereza “I am glad to inform you that the government has agreed to go into joint venture partnership with TanPower Resources (T) Ltd in managing and operating Kiwira Coal Mines Ltd, as outlined in your writen proposal.” Tafsiri yake: “Nina furaha kukuarifu kwamba Serikali imekubali kuwa na ubia na TanPower Resources (T) Ltd. Katika kumeneji na kuendesha kampuni ya Mgodi wa Kiwira.”

Yona anaendelea kwa Kiingereza katika barua yake akisema “As you are fully aware, ital and its expatriate as well as loal staff need to be paid and reassured of the future of the company,” Tafsiri yake: kama unavyofahamu fika KCML inahitaji mtaji, utaalamu na wafanyakazi wake wanahitaji kulipwa ili kuhakikishiwa mastakabali wa baadaye wa kampuni.”

Katika barua hiyo, Yona anasema serikali imeteua timu ya kufanya majadiliano na TanPower Resources jinsi ya kufanya mchakato huo kwa haraka kisheria na kitaalamu.

Barua inataja majina ya maofisa wa serikali walioteuliwa katika timu ya majadiliano kuwa ni: Ms A. Bukuku (Mwenyekiti); kaimu kamishna wa Madini, Omari Chambo; mtaalam wa ushauri wa PSRC (Parastatal Sector Reform Comminission), J.J. Ngelime; na wakili wa Serikali, B. Sahel.

Nakala za barua hiyo zimesambazwa kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba, aliyekuwa waziri wa Mipango na Ubinafsishaji Dk. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Andrew Chenge, aliyekuwa Waziri wa Katibu Kiongozi Ikulu, Marten Lumbanga, aliyekuwa mwenyekiti wa PSRC JohnRubambe, na aliyekuwa Mwenyekiti wa KCML Rumisha Kimambo.

Katika mkataba wa ubia TanPower Resources imenyakua asilimia 70 ya hisa (na kuwa wamiliki)KCML.

Mkataba huo wa kifisadi ulisainiwa juni 8,2005, na Mwenyekiti PSRC Rubambe, \meneja wa KCML Adam Salim Abdu, na wakurugenzi wawili wa TanPower Resources (Evans Mapundi na Wilfred Malekia). Hatimaye TanPower Resources ilijinyakulia hisa zaidi hadi kufikia asilimia 85 na kuiahi Serikali asilimia 15 tu.
MKAPA, YONA WALIVYONYAKUA KIWIRA
Nyaraka moja inaonyesha jinsi Evans mapundi alivyomuandikia barua Yona Januari 2005, akielezea dhamira ya “kampuni yake” (TanPower Resources) kuingia ubia na serikali katika kuendesha KCML kwa kuingiza mtaji wa bilioni 40.1/- kwa mwezi kwa kampuni kubwa tatu ambazo ni IPTL, Songes, Richmond na sasa Kiwira.

Wachambuzi wa masuala ya kifedha wamebainisha kwamba Tanesco itakuwa inajimaliza kwani itakuwa haina uwezo wa kulipa kiasi hicho. Mapato ya Tanesco kwa mwezi ni chini ya dola za Marekani milioni 19.25 (takriban bilioni 25/-)

Awali TanPower Resources ilisajiliwa na majina ya wakurugenzi waasisi watano ambao ni: Anna Mkapa (mke wa rais mtaafu), Daniel Yona, Nicholas Mkapa (mtoto wa rais mstaafu); Joseph Mbuna (baba mkwe wa Nicholas Mkapa) na Evans Mapundi. Baadaye katikati ya mwaka 2005 TanPower Resources ilinyakua hisa za asilimia 85 katika kampuni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCML), na kuingia mkataba wenye utata na Tanesco wa kuuza umeme wa megawati 200 katika gridi ya umeme ya Taifa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kuaminika ndani ya serikali, kuna uwezekano wa kutokea athari kubwa katika mkataba huo na mradi wenyewe unaonekana kusuasua ingawa mkataba ulifanywa zaidi ya miezi 20 iliyopita.

Hofu waliyonayo watoa habari ni kwamba huenda mkataba huo ukaliingiza taifa katika gharama kuwa kwa seriikali na hatimaye kwa watumiaji umeme kama ilivyotokea kwa mradi tata wa IPTL mwaka 1995 na Richmond 2006. wanasema Tanesco huenda itaanza kulipa Kiwira Coal and Power Limited dola za Marekani milioni sita

(takriban bilioni 8/-) kila mwezi wakati itakapoanza kununua umeme huo ghali wa megawati 200 kwa mujibu wa mkataba. Hali hiyo itasababisha Tanesco kuwa na majukumu ya kulipa madeni yanayofikia dola za Marekani milioni 20 (takriban bilioni 26/-) kwa mwezi kwa kampuni kubwa tatu ambazo ni IPTL, Songas, Richmond na sasa Kiwira.

Wachambuzi wa masuala ya kifedha wamebainisha kwamba Tanesco itakuwa inajimaliza kwani itakuwa haina uwezo wa kulipa kiasi hicho. Mapato ya Tanesco kwa mwezi ni chini ya dola za Marekani milioni 19.25 (takriban bilioni 25/-)

(Imetolewa na Kulikoni, Jumatatu Machi 31, 2008)
    (31 March 2008)
Views: 225 | Maoni (0) |

 

Asteria wanatishaaa!

photos  
Asteria wanatishaaa! Galikipa wa timu ya Soka ya Simba Juma Kaseja (kushoto) na Tipo Mkurugenzi Zizuu wakipata Juice katika Mgahawa wa Asteria uliopo katika ofisi za magazeti ya Uwazi, Ijumaa Risasi, Amani na Championi.
(Picha Zote na Issa Mnally) Intenational Photo.

    (31 March 2008)
Views: 256 | Maoni (0) |

 

Hii Ndio Twangaa bwanaaa!

photos  
Hii Ndio Twangaa bwanaaa! Ruiza Mbutu wapili kushoto akiwaongoza wanamuziki wenzake kunengua katika onyesho la bendi ya African Stars 'Twangapepeta' lililofanyika jana usiku katika ukumbi wa TCC Club uliopo Chang'ombe jijini Dar es salaam.
    (31 March 2008)
Views: 310 | Maoni (1) |

 

Mambo ya Msondo

photos  
Mambo ya MsondoMpuliza midomo ya Bata mahili wa bendi ya Msondo Romani Mg'ande (kushoto) na Mtoto wa TX Mosho William Hassani Moshi wakiwapagawisha mashabiki.
    (31 March 2008)
Views: 70 | Maoni (0) |

 

Mambo ya Msondo

photos  
Mambo ya MsondoMnenguaji wa bendi ya Msondo Musica Mama Nzawisa akiwapagawisha mashabiki katika onyesho la bendi hiyo lililofanyika jana usiku katika ukumbi wa Africenter uliopo Ilala jijini Dar es salaam.
    (31 March 2008)
Views: 389 | Maoni (0) |

 

Fumanizi

ijumaa wikienda  
FumaniziNa Jopo la Ijumaa Wikienda
Ali Ramadhani Suleiman (46), mkazi wa Mbezi Makabe, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, amefumwa ndani ya chumba cha gesti, akiwa katika jaribio la kuvunja amri ya sita na mke wajirani yake...
    (31 March 2008)
Views: 4337 | Maoni (17) | Soma Zaidi

 

Mshindi wa friji

ijumaa wikienda  
Mshindi wa frijiMshindi wa friji katika droo ya kwanza ya Bahati Nasibu ya Jishindie Safari ya Hong Kong, Emmanuel Msunya (kushoto) wa Musoma, akipokea zawadi yake kutoka kwa mwakilishi wetu kanda ya ziwa, Hamisi Kikasi



    (31 March 2008)
Views: 219 | Maoni (1) |

 

Chameleon jambazi

ijumaa wikienda  
Na Mwandishi Wetu
Chameleon jambaziWakati Watanzania wengi wakimchukulia Joseph Mayenja a.k.a Jose Chameleon kama mfano wa kuigwa na wanamuziki wetu hapa nyumbani, mdau maarufu wa muziki nchini, amemuelezea msanii huyo katika sura tofauti...
    (31 March 2008)
Views: 879 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Niliishi kuzimu miaka 20- 15

---  
Maisha ya Zubeda yamejaa utata, kila hatua ina vizingiti vyake. Amewahi kunusurika kuwekwa msukule mara mbili Muyobozi na Nyakageni. Kutokana na kuzingirwa mno na mazingara ya kishirikina, alijikuta akipoteza uwezo wa kumudu masomo darasani na kuishia kufeli mtihani wa darasa la saba, wakati mwanzoni, kila mtihani alishika nafasi ya kwanza.

Pamoja na kumfanya ashindwe kufika mbali kimasomo, bado wachawi wanamuandama, wanapanga mbinu tofauti ili kumteketeza, na sasa kiguga lililokubuhu, Mzee Iminsi Ragugwa, linatumia hila aolewe na mwanaye ili wakifanikiwa wampoteze kabisa. Endelea kusoma…
    (31 March 2008)
Views: 347 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Unaijua lunch time Sex? Shoga unaibiwa!-2

Mahaba  
Unaijua lunch time Sex? Shoga unaibiwa!-2Niambie shoga, za tangu wiki iliyopita? Natumai unaendelea vema, hivyo basi napenda tuungane pamoja kumshukuru Mungu kwa kutusalimisha mpaka leo hii. Mimi ni mzima wa siha njema...
    (31 March 2008)
Views: 522 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

SHE IS TOO YOUNG TO DIE (Ni mdogo mno kufa) -11

---  
Baada ya kuishi maisha ya raha mustarehe kwa kipindi kirefu, Gilbert ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya WorldCom inayojishughulisha na uuzaji wa kompyuta katika nchi za Afrika Mashariki, yeye na mke wake wameanza kuingia katika matatizo ambayo hata siku moja hawakuwahi kuyawazia. Kwanza kabisa, mke wa Gilbert (Salome)

anakwenda kijijini kwao likizo akiwa mjamzito, huko anakwama kurejea mjini baada ya mvua kubwa kunyesha na kuharibu miundombinu ya maeneo hayo! Madaraja yamevunjika na barabara zimechimbika vibaya, hakuna uwezekano wa basi kufika kijijini hapo. Wakati hayo yote yakitokea Salome ni mjamzito karibu kabisa kujifungua na hali yake ni mbaya.

Alichokifanya Gilbert ni kukodisha helkopta kutoka Dar es Salaam mpaka kijijini ambako alimchukua mkewe na kumsafirisha hadi hospitali ya Sengerema ambako alifanyiwa upasuaji, mtoto akatolewa akiwa mzima lakini yeye aliendelea kuvuja damu nyingi,

madaktari wakashauri mfuko wake wa uzazi uondolewe jambo ambalo Gilbert hakukubaliana nalo kwa sababu alitaka watoto zaidi! Akaamua kuhamia hospitali ya Bugando ambako madaktari walimwambia hapakuwa na uamuzi mwingine tofauti na aliopewa kabla, akawa hana jinsi zaidi ya kukubali na mfuko ukaondolewa.

Salome na mtoto wao waliyempa jina la Faith wakawa wamepona na familia nzima ikarejea Dar es Salaam. Tofauti na alivyokuwa amefikiria kwamba matatizo yamekwisha, ghafla Faith alianza tabia ya kulia mfululizo, wakampeleka katika hospitali mbalimbali ambako madaktari waliendelea kumchoma sindano wakidai alikuwa na kichomi lakini hazikumsaidia! Afya yake ikaharibika, akapoteza uzito mkubwa na ngozi yake ikababuka sababu ya kuchomwa madawa makali.

Mwisho wakazigomea sindano na kuamua kutafuta msaada kanisani, ambako nafuu ilipatikana kidogo lakini baadaye hali ikarejea palepale, ndipo wakaamua kumtafuta daktari mwingine bingwa wa magonjwa ya watoto aliyeitwa Dk.

Msomekela katika zahanati yake iliyopo ya Sinza ambaye baada tu ya kumwona mtoto na kumsikiliza kifuani aliwaambia hapo hapo kwamba mtoto wao alikuwa na tatizo liitwalo PDA! Wakakutwa na mshtuko, ilikuwa ni mara ya kwanza wao kusikia jina hilo.
Je, nini kitaendelea? Maisha ya mtoto huyo pekee wa Salome na Gilbert yataokolewa? SONGA NAYO…
    (31 March 2008)
Views: 389 | Maoni (0) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 21 22 23  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page |