Hata hivyo, kabla ya kueleza hayo naomba nikueleze wewe msomaji wangu ambaye unajisifu na kujitapa kutofuatilia mwenendo mzima wa matumizi ya simu ya mpenzi wako kwa madai kuwa hutaki presha! Hakika wewe unamchoche a huyo umpendaye kufanya mambo yake kwa nafasi tena bila wasi atawasiliana na vimada au mabwana zake kwa raha zake.
Hivyo, kama wewe ni miongoni mwa hao watu badilika sasa, usiogope kukutana na changamoto zitakazojitokeza mara baada ya kubaini kuwa mpenzi wako anajihusisha na uhusiano mwingine kwani kujua ukweli ni njia mojawapo itakayokupa nafasi ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo na kujikuta ukiishi kwa amani katika ulimwengu uliyojaa magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na ngono zembe.
Nirudi kwenye mada yangu, katika utafiti wangu wa miezi kadhaa nimebaini kuwa, usiri katika matumizi ya simu ndio nguzo pekee wanayotumia watu wengi wasio waaminifu kwa wenza wao.
Watu wengi hukimbilia kupekuwa kitabu cha simu (phone book) na sehemu ya kuhifadhia meseji (inbox) ili kujua kama kuna mambo yaliyopo nyuma ya pazia anayotendewa na la azizi wake, lakini nataka nikueleze kuwa kama wewe ni miongoni mwa hao watu tambua unajidanganya kwani wasaliti wengi huwahifadhi wapenzi wao kwa majina yasiyoweza kukupa hofu kama ni Kidawa basi atakuwa shangazi pindi anaporejea ama kuja kuonana na wewe na pindi atakapokuwa anaenda kukutana na kidawa basi jina hilo hubadilika na kuwa Sweetie na meseji zote tata hufutwa.
Kama hiyo haitoshi usiri mwingine wa wasaliti ni pale linapokuja suala la kutoacha simu chini hata kama anaingia bafuni! Hii ni kwa wanandoa ambao ni wasaliti hawa wakiwa nyumbani huhakikisha hawawapi mwanya wapenzi wao wakushika simu zao na wengine waliobahatika kuwa na usafiri wakiingia ndani basi simu zao huziacha kwenye gari.
Mbali na hilo wapo ambao huacha simu zao kweupe lakini huweka security code (namba ya siri) itakayokunyima nafasi ya kupekenyua vitu vilivyomo ndani ya simu kama ndugu yangu mmoja hivi wa pale Sinza Makaburini maana ukitaka ugombane naye muombe namba yake ya siri upekenyue simu yake lazima abadilike maana kutoka rangi yake nyeupe hadi nyekundu.
Kama hiyo haitoshi, kwa wapenzi ambao wenyewe hujiita girlfriend na boyfriend hawa mara nyingi kama mmoja wao si mwaminifu, ataweka simu yake silence au kwenye vibration pindi wanapokuwa pamoja na ni mwiko kwao kupokea simu mbele ya mwenza wake.
Hivyo basi kama wewe una mpenzi wako na kila ukitoka naye out hujawai kumuona akipokea simu wala simu yake ikiita, jua kuna walakini na wengi wa watu wenye tabia hii hupokea simu au hukagua simu zao kuangalia nani aliyemtafuta pindi mwenza wake akiwa ameinua sehemu walipoketi pamoja ama huinuka na kwenda msalani kuwasiliana na vimada ama wachumba waliomtafuta.
Baada ya kubainisha haya naomba nikueleze kuwa, endapo umeona moja kati ya dalili nilizobainisha hapa jua mwenza wako anakusaliti! Hivyo, jipange uweze kumdhibiti. Utamdhibitije? Kama hujui usisite kuwasiliana nami haraka iwezekanavyo!
Naomba nimalize kwa kusema kuwa, endapo una matatizo ya kimapenzi yaani kama kila ukiingia kwenye uhusiano mambo yanakwama au una tatizo la kuwahi kufika kileleni? Upungufu wa nguvu za kiume? Kutofika kileleni au kutosikia raha ya mapenzi.
Pia kama hujui jinsi ya kumpata mpenzi, uhusiano wenu una migogoro, unashindwa kupanga jinsia ya mtoto unayemtaka, hujui kutumia maumbile yako madogo kumpagawisha umpendaye, basi huna sababu ya kuhangaika kwa waganga wa jadi. Wasiliana nami nikusaidie.
Kumbuka wengi wamefanikiwa kwa tiba na ushauri wangu kupitia magazeti na majarida mbalimbali nchini, nipigie simu kwa ufumbuzi wa matatizo yako kwenye no. 0715 888 887 na ili ujibiwe SMS za maswali tuma vocha.
|