Mtangzaji wa kipindi cha Bongo Movies cha Channel Ten, Joyce Kirya ndiye alikuwa MC upande wa kulia wa Vinara Awards 2008. Joyce pia ni mtangazaji wa Clouds FM.
Mwigizaji wa filamu ya Fake Pastors, Miss Lisa Jensen, naye alikuwepo kushuhudia mwigizaji mwenzie wa sinema hiyo Emmanuel Muyamba akitwaa tuzo ya mwigizaji msaidizi bora.
Halima Mlacha (HABARILEO 31/5/2008) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe, ambaye pamoja na polisi wengine 12 wanakabiliwa na kesi ya mauaji, jana alikuwa mbogo mahakamani baada ya kesi hiyo kuahirishwa....[b]
Na Waandishi Wetu Pati ya wachezesha muziki (Ma-DJ) maarufu jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni ilitaliwa na mambo ya uchafu baada ya wengi wao kufanya mambo yasiyofaa...
Christopher Lissa na Hamida Hassani Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusufu Manji amewabeba baada ya kukubali kuwa mlezi wa Kundi la Vichekesho la Ze Comedy ambalo kuanzia jana wametangaza rasmi kujiunga na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...
Prosper amerejea tena Uingereza kwa ajili ya Kliniki ya macho yake lakini kichwani mwake ana ajenda ambayo hata mke wake haijui, ya kwenda kuwasaka wabaya wake Seche na Ashura. Baada ya Kliniki na kuhakikishiwa kwamba macho yake yalikuwa yakiendelea vizuri, akiona kwa kutumia miwani yenye kamera ndogo iliyotupa taswira kwenye Retina ya bandia iliyopandikwa ndani ya jicho lake ambayo ilisafirisha mawimbi hayo kupitia mshipa wa Optic mpaka kwenye ubongo na kumfanya Prosper aone.
Ameamua kukamilisha kazi yake ya pili, anatoka hotelini akiwa amemdanganya mtoto wao Lusajo kwamba anakwenda kununua dawa, nje ya hoteli anakodisha teksi na kumwomba dereva ampelekee maeneo ya East London nyumba namba 165! Dereva anafanya hivyo na kumshusha nje ya lango la nyumba hiyo nay eye kuondoka zake kurudi hotelini.
Prosper anaingia hadi ndani na kuwaweka Ashura na Seche chini ya ulinzi akiwa na visu vyake viwili mikononi tayari kumdhuru yeyote ambaye angeleta ubishi, baadaye Ashura anampiga teke kichwani na miwani kuondoka, kuona kwa Prosper kunakoma! Hapo hapo anawekwa chini ya ulinzi na yeye ndiye anageuka mtu wa kuwaomba wasimuue. Je, nini kitaendelea? Prosper atauawa na ni nani atajua mahali alipofia? SONGA NAYO…
Jina la kolamu ni Uwanja wa Huba na siku ni Jumamosi, nipo hapa kwa ajili yako wewe msomaji wangu kukupa mbinu za kuwa mpya katika uhusiano wako ili uweze kuwa na fikra mpya juu ya mambo ya uhusiano na mapenzi. Imani yangu ni kwamba utakuwa mzima wa afya njema na upo tayari kabisa kufuatilia mtiririko wa mada yetu ya leo...