..ni wakati wa kubadilishana mawazo na Afisa Uhusiano wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco (kulia).
...Ni wakati wa kula chakula na kutafakari kuhusu fainali za Jumamosi.. warembo walipotembelea City Garden Julai 30.
...ni wakati wa kutafakari kuhusu Jumamosi.... warembo walipata wasaa wa kutafakari walipotembelea Coco Beach Julai 30 mchana. PICHA ZAIDI NENDA:MISS-TANZANIA.COM
Kampuni ya simu za mkononi Tanzania, Vodacom, leo imetoa msaada wa madawati 280 kwa shule ya msingi Vijibweni, iliyopo Wilaya ya Temeke, Kigamboni jijini Dar es salaam. Kazi hiyo ya kukabidhi madawati, imefanywa na Afisa Uhusiano wa Vodacom Foundation mbele ya Miss Tanzania anayemaliza muda wake kesho kutwa, Richa Adhia pamoja na washiriki wengine wa Vodacom Miss Tanzania 2008. Vodacom siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada mbalimbali ya kijamii nchini Tanzania kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation. Mwenyekiti wa shule ya Msingi Vijibweni Bw. Anderson (kushoto) akisoma risala mbele ya Afisa Uhusiano wa VODACOM Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) na Miss tanzania 2008, Richa Adhia.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Vijibweni wakifurahia msaada huo wa madawati.
Mtandao wako huu uupendao umeandaa taji la miss globalpublisherstz.com na kitita cha shilingi 500,000 za Kitanzania kwa mrembo atakayechaguliwa kuwa mwenye mvuto wa sura kuliko washiriki wengine wa VODACOM MISS TANZANIA 20008. Atakae mchagua mrembo huyo ni wewe mwenye mtandao huu, unachotakiwa kufanya ni kupiga KURA YAKO kwa ‘ku-klik’ kwenye jina la mrembo wako (ORODHA YA MAJINA YAO IKO HAPO KULIA) kisha bonyeza neno VOTE lililopo chini ya logo ya VODACOM na tayari utakuwa umeshampigia kura mrembo anayekuvutia. Kuangalia nani anaongoza hadi sasa, bonyeza RESULTS. Piga kura yako kadri utakavyoweza, picha zaidi za warembo hawa zipo kwenye ‘gallery’ ya BONGO CELEBRITIES upande wa kushoto au mwishoni mwa ukurasa huu.System ya upigaji kura hairuhusu kupiga kura zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ili kupiga kura nyingi, tumia kompyuta nyingine au piga siku nyingine au baada ya kuzima kompyuta yako kwa muda au ‘clear history’. Pia temebelea mtandao rasmi wa WWW.MISS-TANZANIA.COMna mtandao wa wadhamini wakuu WWW.VODACOM.CO.TZ Kumbuka: Zimebaki siku mbili tu! ***************************************************************************** FLORA MVUNGI - NO 19
Brazameni mmoja alialikwa kwenye sherehe ya birthday.Kwa uroho jamaa akafakamia vyakula kisha baadae kuanza kucheza muziki na demu mmoja. Mara mshikaji akashikwa na tumbo la kuhara ndipo alipokwenda chooni na kujisaidia. Baada ya kumaliza haja yake, kuangalia kwenye ndoo maji ya kunawia hamna kwahiyo akaamua kutoa ‘engachifu’ yake na kujifutia kisha kuikunja vizuri na kuirudisha mfukoni. Aliporudi ukumbini akaendelea kucheza muziki hadi kuloa jasho. Si akajisahau na kutoa ile ‘engachifu’ aliyokwishaitumia kujisafishia chooni na kujifutia. Akijikuta amejipaka kinyesi usoni na kusababisha harufu mbaya iliyowafanya watu kumkimbia...
Na Salum Mnette Utata wa mazingira ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Tarime kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, umezua maswali mengi huku baadhi ya watu wakiamini kuwa mheshimiwa huyo kauawa...
Na Christopher Lissa Jeshi la Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam, limeanza kuwabana vilivyo watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulenya, ambapo habari za watuhumiwa kuanza kukimbia jiji zimepatikana...
Na Mwandishi wetu, Mbeya. Mama mmoja (jina tunalihifadhi kwasababu za kimaadili) mkazi wa Kijiji cha Malowe mkoani hapa, amefanyiwa unyama kwa kubakwa na mkwewe aitwaye Kenny Mwakaleya ambaye ni mdogo wa mume wa mtoto wake...
Na Richard Bukos Siku chache baada ya kesi yao dhidi ya kituo cha Televisheni cha EATV iliyokuwa ikinguruma katika Mahakama ya Biashara jijini Dar es Salaam kutupiliwa mbali, kundi la Vichekesho la Ze Comedy linatarajia kuandamana hivi karibuni...
Ndugu msomaji, wiki iliyopita nilianza mkasa huu mpya unaomhusu kijana Beka ambaye katika harakati za kutafuta maisha, amejikuta akiwa kiongozi wa wachawi baada ya kupewa nguvu hiyo na mzee mmoja tajiri aliyeko Zanzibar. Uchawi huo umemuwezesha kuwa mganga anayetibu watu wenye matatizo ikiwemo kuzindika nyumba nk. Haya unganeni nami KULWA MWAIBALE ili kujua kilichomsibu kijana huyo ambaye kwasasa anaishi jijini Dar es Salaam...
Ndugu zangu, kupanda na kushuka, kupata na kukosa, kufanikiwa na kutofanikiwa ni miongoni mwa kanuni zinazochukua sehemu kubwa ya maisha yetu. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anafanya jambo huku akiwa na uhakika wa asilimia mia moja wa kulifanikisha lakini, kila tunalolifanya lazima tuwe na imani ya kulifanikisha kwakuwa tunaamini kwamba hakuna kinachoshindikana chini ya jua...
Wiki iliyopita nilianza kuzungumzia mada iliyokuwa inahusu mambo ambayo mwanamke akiyatimiza anajiweka katika nafasi nzuri ya kumdatisha mpenzi wake. Niliishia kuzungumzia tabia ya kuwa mjanja na kusema kwamba, hiyo ni sifa ambayo mwanamke anatakiwa kuwa nayo ili kumvutia mpenzi wake...
T ayari Aileen na Rei wameingia nchini Ufilipino ambako maisha yao yanabadilika kabisa, Rei hakuwahi kufahamu kwamba Aileen alikuwa mtoto wa tajiri Francisco Morientes na kwamba jina lake halisi aliitwa Monee. Baba yake mzazi anafariki, Aileen anarithi utajiri wote ambao mzee huyo aliutafuta nusu ya maisha yake, kwa kitendo hicho tu tayari Aileen amekuwa mwanamke tajiri kuliko mwingine yeyote nchini Ufilipino.
Maisha yao yamebadilika kabisa, wanaishi kitajiri kwenye jumba la mzee Morientes lililopo nje kidogo ya jiji la Manila. Kwa Rei, mama na binamu yake Regina waliokulia Umasaini, wakiishi pamoja na mifugo na kulala chini, kinachowatokea ni ndoto lakini wamelazimika kukubaliana na ukweli. Mama yake Rei na Regina wanashindwa kabisa kuamini kwamba Aileen alishawasamehe kwa kitendo cha kikatili cha kumfanyia tohara kama sharti la kuolewa na ndugu yao, wanalazimika kumwomba msamaha tena lakini yeye anawaondoa shaka na kuwataka wasahau yaliyopita.
Jamii ya Wafilipino wanashindwa kumkubali Rei moja kwa moja, wakidai haikuwa halali kwa Aileen kuwaacha wanaume wote wa Kifilipino kwenda kuolewa na Mmasai, hii inafanya anyanyapaliwe kila mahali alikopita. Baadaye Aileen aligundua njia ya kulimaliza tatizo hilo, akachukua fedha nyingi na kuzitoa kwa jamii lakini yeye hakuonekana, aliyefanya hivyo alikuwa Rei, ghafla Wafilipino wakaanza kumkubali kwa jinsi alivyowasaidia, tabia ya kunyanyapaliwa mtaani ikaisha, si kwake tu bali pia kwa mama na dada yake.
Wakati mambo yakiendelea kuwa mazuri, Rei amekwishazoea maisha ya Ufilipino ambako aliheshimiwa na kila mtu, akiishi maisha ya kifahari na kuendesha magari ya thamani kubwa, ghafla mke wake akaja na wazo kwamba alitaka kurejea Afrika, mahali ambako siku zote alipachukulia ndio nyumbani kwake, uamuzi huu unamshtua Rei na kumfanya aulize maswali mengi. Je, nini kitaendelea? Watarejea Afrika? SONGA NAYO…
MADA YA WIKI HII Miaka miwili iliyopita ulipata ajali mbaya sana na kuvunjikaa kiuno na hivyo kutoweza kushirikiana kimapenzi na mke wako.
Awali ‘mamsapu’ wako alikuwa karibu na wewe kwaa kila kitu na ndiye aalikuwa mfariji waako mkubwa. Hivi kaaribuni, mkeo amekuwa na mabadiliko ya tabia kwani hakujali kama zamani na akitoka nyumbani uchelewa kurudi.
Baada ya kufanya uchunguzi umegundua anatoka na jirani yako mmoja. Ungekuwa wewe ungefanya nini?
Na Abraham Makinda Wakati watanzania wakiwa katika majonzi makubwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Tarime kupitia chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuna madai kuwa baadhi ya watu wameshusha pumzi zao kuonyesha mtazamo na hisia tofauti...