Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan akisalimiana na mwandaaji wa Bonanza la Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kabla ya kuanza kwa mchezo wa kuvuta kamba kati ya waandishi kike na Mamisi Utalii leo katika viwanja vya Leaders
Warembo wa Miss Utalii 2008 wakivuta kamba kushindana na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika shindano la kuvuta kamba katika Bonanza la Wanahabari, Ma-mis hao walishinda raundi zote mbili
Pamboja na Mkurugenzi wa Aset kuwapiga tafu waadhishi wa habari wa kike katika mchezo wa kuvuta kamba haikusaidia kitu, kwani walishindwa!
Ma-misi Utalii wakishangilia kwa furaha mara baada ya kuwashinda wandishi wa habari wa kike wa vyombo mbalimbali katika mchezo wa kuvuta kamba. Media Bonanza hufanyika kila mwaka na huwakutanisha waandishi wa habari wote nchini. PICHA: Issa Mnally GPL
Usiku wa kuamkia leo kulifanyika onesho la muziki wa wasanii kutoka Nigeria wanaojiita P-SQUARE ambao wanatamba hivi sasa ni kabao chao kikali cha DO ME. Wasanii hao, Peter na Paul Okoye ambao ni pacha, walipagawisha vilivyo mashabiki waliofurika kwenye viwanja vya LEADERS CLUB usiku wa kuamkia leo. Onesho hilo la kufana liliandaliwa na EAST AFRICA RADIO/CHANNEL 5 za jijini Dar es salaam. Picha zifuatazo zilizopigwa na mpiga picha mkuu wa GPL, RICHARD BUKOS zinajieleza zenyewe...
VUNJA JUNGU DAR, BALAA Mdau maarufu wa bendi ya Akudo Impact Pius Luta maarufu kama Mzee wa Pamba akiyarudi na mashabiki waliofika katika Ukumbi wa Vatican City jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo katika onesho la maalum la vunja jungu. PICHA : RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA / GPL
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwembesonga iliyopo Morogoro mjini wakimkimbiza hospitalini mwenzao Happiness Gaitani wa Darasa la 4 A baada ya kulegea na kupoteza fahamu muda mfupi alipopewa dawa za kinga ya kichocho na minyoo PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE/ GPL
Na Christopher Lissa Malikia wa muziki wa taarabu nchini Khadija Kopa amefunga ndoa ya tatu na mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Jafari ambaye anaonekana kuwa mdogo kiumri yaani “Kiserengeti boy’...
Na Hawa Mkombozi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samweli Sitta, Jumanne, Agosti 26, mwaka huu, alisema kuwa anamzimikia sana mwanadada Jacqueline Ntuyabaliwe maarufu kama ‘K-lyin’ kwa mashairi na sauti yake tamu ya kuvutia...
Na Christopher Lissa Nguli wa muziki wa mipasho nchini wa Kundi la Jahazi Modern Taarab ‘Wana wa nakshi nakshi’ Mzee Yusuf ameibuka na kudai kuwa ana uwezo wa kuongeza wanawake wawili zaidi kwani bado ana uwezo wa kuwamudu...
Na Rhobi Chacha Baadhi ya wasanii wa Kundi la Fukuto Arts Promotion lililokuwa likirusha mchezo wake kwenye Kituo cha luninga cha TBC1 uliojulikana kwa jina la Jumba la dhahabu, wanasakwa na Polisi kwa kumtapeli kijana Moriss Lucas anayejulikana kwa jina la ‘Young Bilionaire’...
Kutoka utumwa wa ngono hadi kuwa nguli wa masuala ya Mitindo nchini Uingereza, haikuwa kazi ndogo. Dina amepita kwenye milima mingi lakini hatimaye akafanikiwa maishani, pato lake la kwanza baada ya kuingia mkataba na kampuni iliyomwibua ya England Modelling Agency (EMA) ilikuwa ni paundi milioni mbili, zaidi ya shilingi milioni mianne za Kitanzania. Kitu cha kwanza alichokifanya baada ya kupata mkabata huo, ni kuamua kusafiri kwenda Afrika Kusini kwenye mji wa Johannesburg alikokuwa akiishi kabla ya kwenda Uingereza. Anataka kwenda kutoa shukrani zake lakini pia kumtafuta John Kamau, mpenzi wake waliyepotezana muda mrefu.
Nje ya uwanja wa ndege, anakutana na Madame Modesta, mwanamke aliyeishi naye ndani akimtesa na kumfanya mtumwa wa ngono akiwa amefungwa minyororo! Hasira zinampanda Dina na kujikuta akitamani hata kumpiga risasi. Baadaye wanaongea na kusameheana, ndipo mwanamke huyo huyo akampa siri ya mahali John Kamau alipo, kwamba yupo kwenye gereza la Posmo katika Jiji la Capetown.
Dina anasafiri hadi kufika mbele ya gereza hilo lakini wakati anatembea kwa miguu kuelekea sehemu ya kuingilia, maaskari walijitokeza na kumweka chini ya ulinzi wakimwambia anashtakiwa kwa kosa la mauaji! Kichwani mwake hana kumbukumbu kabisa kama amewahi kuua akiwa nchini humo, amekosa kitu cha kujibu. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Msako mkali wa kumtafuta Patrick au Patii kama alivyojulikana na wengi unaendelea. Pamoja na Wapelelezi wenye uzoefu wa muda mrefu kumfuatilia, hakuna aliyefanikiwa kumtia mikononi zaidi ya kuambulia kifo! Tayari ameshaua Wapelelezi wanne; Peter, James, Anna na Mabesha.
Sasa Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi, Makao Makuu Moses Lupango, anawaagiza Wapelelezi Joel na Pius kumfuatilia kwa mara nyingine nchini Uingereza. Joe alipofika nyumbani, kabla ya kumueleza mkewe tayari alishahisi kwamba alitakiwa kusafiri, akapingana naye kwa nguvu zote. Joel akabaki njia panda! Je, Joe atamsikiliza mkewe au atatimiza majukumu yake ya kikazi? Mtunzi JOSEPH SHALUWA anaendelea...
...Wengi wanashindwa kukabiliana nazo Sina shaka mambo yenu ni mazuri wasomaji wangu wapenzi na mnaendelea kutimiza majukumu yenu ya kila siku vyema kabisa. Kwa upande wangu mimi ni mzima wa afya njema kwa msaada wa Mungu wa Mbinguni...
We are delighted to announce BBC commitment to Africa with launch of new branded channels
BBC Worldwide Channels pledged its commitment to the African market recently as plans were announced to launch a suite of BBC-branded thematic channels into the region. The channels will be available via MultiChoice’s DStv platform, Africa’s leading television provider, from 1 September 2008*
The new thematic channels - BBC Entertainment, BBC Knowledge, BBC Lifestyle and CBeebies - will replace and build on the success of existing channels BBC Food and BBC Prime, enabling viewers to access even more of the award-winning and high-quality programming from the BBC.
BBC Channels will be made available on channel 306 to all DStv Premium subscribers on the 01 September 2008 at 06:00 CAT
Regards,
Lucy Kiwhele PUBLIC RELATION MANAGER MULTICHOICE TANZANIA LTD
Job Chacha (katikati) ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo juu ya azma yake ya kuwania kiti cha ubunge Jimbo la Tarime kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kiti hicho kiko wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa akikikalia marehemu Chacha Wangwe,kushoto kwake ni Afisa wa Idara MAELEZO Sise Mwirabi na kulia ni mpambe wake.
LAZIMA MTU AFE PALE DDC! Mkurugenzi wa Kampuni ya Dynamite Promotions INC Shomari Kimbau (Katikati) akiwa tambulisha mabondia Ramadhani Miyeyusho (kushoto) na Selemani Said ‘tall’ ambao watatwangana Agosti 30 mwaka huu ndani ya ukumbi wa DDC Mlimani Jijini Dar es Salaam kuwania ubingwa wa Tanzania ‘Welterweight Title’
BONGO TAABU HATA KWA MAGARI Kufuatia ubovu wa miundombinu hususan ya kupitishia maji taka, leo mchana kamera yetu iliyanasa magari yakipita kwa taabu katika Barabara ya Uhuru Jijini Dar es Salaam kutokana na mvua za rasharasha zilizoanza kunyesha. PICHA :CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS / GPL
POSITION: Programme assistant QUALIFICATION: Secondary education, with a diploma/ advanced diploma in business/ public administration/ Human Resources Management. A first degree In business or public administration, edonomics, political science and social sciences would be advantageous, but not a stiff requirements. At least 3 to 5 years of progressive administrative, human resources, or programme experience APPLY TO: Development support Serveces Unit, UNDP, P.O.BOX 9182 Dar es Salaam DEADLINE; 5th September 2008 PUBLICATION: 21st August 2008 Daily News....
POSITION: Programme assistant QUALIFICATION: Secondary education, with a diploma/ advanced diploma in business/ public administration/ Human Resources Management. A first degree In business or public administration, edonomics, political science and social sciences would be advantageous, but not a stiff requirements. At least 3 to 5 years of progressive administrative, human resources, or programme experience APPLY TO: Development support Serveces Unit, UNDP, P.O.BOX 9182 Dar es Salaam DEADLINE; 5th September 2008 PUBLICATION: 21st August 2008 Daily News....