arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for September 2008 Year

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» Vigogo wa TFF
» (Kazi ya damu- 27)
» From china with true lo ...
» Balozi wa Msumbiji
» Mkapa alia mbele ya waz ...
» I can’t kill part 4
» Mama MZAZI WA BABU SEYE ...

 

EID MUBARAK!

photos  
EID MUBARAK!
Uongozi na wafanyakazi wote wa Global Publishers, unawapongeza waislamu wote duniani kwa kumaliza salama funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na unawatakiaEid Mubarak!
    (30 September 2008)
Views: 92 | Maoni (0) |

 

NEC YALIA NA UCHAGUZI KWA WANGWE!

photos  
NEC YALIA NA UCHAGUZI  KWA WANGWE!

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeelezea kufadhaiashwa na kusikitishwa na taarifa za matukio yanayotishia amani katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Tarime.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Lewis Makame amewaeleza waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es Salaam kuwa, NEC imepata taarifa za kuwepo kwa matukio hayo ikiwa ni pamoja na kuumizwa kwa viongozi wa vyama vya siasa na wananchi pamoja na vitisho,uchochezi na lugha za matusi hali ambayo ameonya kuwa haitavumiliwa na Tume yake.

?Ikumbukwe kwamba vitendo hivyo ni ukiukwaji wa sheria na endapo wanaouhusika watabainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao?alionya Jaji Makame.Pichani kushoto Jaji Makame akifafanua jambo alipokuwa anaongea katika mkutano huo na waandishi wa habari.

MUFTI MKUU WA TANZANIA ABURUZWA MAHAKAMA KUU!

NEC YALIA NA UCHAGUZI  KWA WANGWE!
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa bin Simba pamoja na baadhi ya viongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) leo wameburuzwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafukuza baadhi ya viongozi waandamizi wa Baraza hilo.

Hata hivyo Mufti hakufika mahakamani hapo na badala yake aliwakilishwa na Wakili wake Alhaji Said Elmaamry.Kesi hiyo Namba 592008 iko mbele ya Jaji Projesta Rugazia.

Hata hivyo kesi hiyo ilikwama kidogo kutokana na hati za upande wa mashitaka zilizofikishwa mahakamani hapo kuwa na kasoro nyingi na hivyo kuilazimisha mahakama kuuamuru upande wa mashitaka kuwasilisha hati nyingine zilizo sahihishwa.

Sambamba na Mufti kesi hiyo pia inaihusu Bodi ya wadhamini wa BAKWATA. ambapo Masheikh wanaomshitaki Mufti ni aliyekuwa naibu Muft Abubakar Zuberi, Sheikh Mataka, Sheikh Chizenga, Sheihk Hamid, Sheikh Abdul Yusuf na wengine ambao wanadai walitimuliwa na BAKWATA kinyume cha sheria.

Pichani Wakili wa kesi hiyo El Maamry (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya mashekh walalamikaji katika kesi hiyo (kushoto ni Sheikh Shaban Maaka)

PICHA NA CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (30 September 2008)
Views: 77 | Maoni (0) |

 

ALBINO AKUTWA HOI KWA MCHAWI

uwazi  
ALBINO AKUTWA HOI KWA MCHAWI Na Dunstan Shekidele, Morogoro
Mtoto John Benedict ambaye ni albino wa Kijiji cha Misongeni, kilichopo nje kidogo ya mji wa Morogoro alikutwa akiwa hoi kwa mama mmoja, Matrida Aloyce (59) anayedaiwa kuwa ni mchawi baada ya kutoweka kwa wazazi wake kimazingara kwa siku tatu....
    (30 September 2008)
Views: 1018 | Maoni (9) | Soma Zaidi

 

Uwazi lapongezwa kwa habari za uchunguzi

uwazi  
Na Issa Mnally
Gazeti la Uwazi linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers LTD, limepongezwa kwa kuandika habari nzuri za kiuchunguzi na adimu hapa nchini....
    (30 September 2008)
Views: 106 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Meja wa Jeshi

uwazi  
Na Mwandishi Wetu
ASKARI wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) wa Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam, Meja Charles Chanyika maisha yake bado yapo hatarini kutokana na madai kwamba wabaya wake waliomteka na kumjeruhi bado wanaonekana mitaani na wamekuwa wakiendelea kutishia maisha yake....
    (30 September 2008)
Views: 274 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Gari la Zitto lapigwa mawe Tarime

uwazi  
Gari la Zitto lapigwa mawe Tarime Na Mwandishi Wetu, Tarime
Gari la kampeni analotumia Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe (pichani) na viongozi wengine wa chama hicho limepigwa mawe jimboni Tarime....
    (30 September 2008)
Views: 551 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

NI WAKATI WA KUWAPIMA VIONGOZI WETU KABLA YA UCHAGUZI MKUU UJAO

Pasua Jipu  
KWANZA nimshukuru Mungu kwa kunipa uhai na afya njema nikiamini pia wewe msomaji wa safu hii una afya njema kufanya shughuli zako za kila siku.

Wiki hii niwakumbushe kidogo hotuba ya mzee Benjamin Mkapa aliyoitoa Agosti 25, mwaka 2004, kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete na wenzake madarakani, mstaafu huyo wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alitoa moja ya hotuba kali kabisa....
    (30 September 2008)
Views: 101 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Nilizaa na dada na mama yangu mzazi - 12

Mikasa ya kusisimus  
Bado mauzauza ya kishirikina yanaendelea kumkumba Sebastian Majuto akiwa mwanafunzi wa sekondari kidato cha nne mwenye ndoto ya kuwa Padri, jambo ambalo hakutegemea ni dada yake kumwambia kila mwanaume anayetembea naye humwacha bila sababu ya msingi, Sebastian anamwambia dada yake ni mapepo wachafu na kumtaka waende kwa mchungaji wakaombewe, jambo analopinga Sechelela na kwenda kwa mganga wa kienyeji, anaporejea anamwambia mganga amesema kisa cha kukimbiwa na wanaume ni jini mahaba linalomsumbua na ili kuliondoa lazima afanye mapenzi na kaka yake. Sebastian anapinga kitendo hicho na Sechelela anatishia kujiua, kaka mtu anafanya mapenzi kumuokoa dada yake, hata hivyo ukweli unagundulika baadaye kuwa Sechelela alitumia njia hiyo kufanya mapenzi na kaka yake ikiwa ni masharti ya mganga wa kienyeji ili kupata utajiri. ....
    (30 September 2008)
Views: 849 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

THE BLOOD DEAL ? 14

hadithi za Shigongo  
Msichana tajiri Priscilla amempenda mlemavu aitwaye Muddy. Wote wana historia zao mbaya za maisha na hawafahamiani vizuri!

MUDDY:
Huyu ni yatima aliyelelewa na bibi yake aliyemtesa sana mpaka akafikia uamuzi wa kutorokea Dar es Salaam ambako alijiunga na kundi la majambazi waitwao Komandoo Yosso lililopanga kumtumia kuwa anaingia ndani ya nyumba na kufungua milango kwa sababu ya umbile lake dogo, tukio la kwanza tu kushirikishwa halikuzaa matunda, maaskari waliwazunguka na kuwakamata wenzake wote isipokuwa kiongozi wao Tom Kundea aliyefanikiwa kuondoka eneo la tukio akiwa na Muddy kwenye buti ya gari.

Eneo la Tazara gari lake lilizingirwa na maaskari, akamiminiwa risasi nyingi lakini baadaye ikagundulika alikuwa bado hajafa, hivyo akakimbizwa hospitali ya Amana. Hakuna aliyeelewa kwamba ndani ya buti kuna mtu, gari likavutwa mpaka kituo cha Polisi ambako usiku Muddy alibetua na kutoka kisha kutambaa hadi Stesheni ya Tazara, akapanda kwenye treni akiamini ni ya reli ya kati ili arudi nyumbani kwao Kilosa, baadaye akagundua alikuwa amepanda treni ielekeayo Zambia akiwa tayari amekwishavuka mpaka.

Mzee Kantalamba waliyesafiri naye anajitolea kumchukua na kwenda naye nyumbani kwake Porini kabisa, huko ndiko Muddy anagundua kwamba mzee huyo alikuwa ni mganga wa tiba za Jadi. Amelipenda eneo hilo na anaamini atajificha hapo kwa miaka mingi bila kukamatwa.

PRISCILLA.
Priscilla anafiwa na mwanamke aliyeamini kwamba ni mama yake kumbe haikuwa hivyo, mama yake mzazi alikufa kwa kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua, lakini hakuna aliyemwambia jambo hilo. Baada ya mazishi ya bibi aliyeamini kwamba ni mama yake yaliyofanyika mjini Moshi kwa msaada wa Halmashauri ya mji, mwanamke mmoja anajitokeza kumchukua kwenda kuishi naye nyumbani kwake, huko ndiko Priscilla amegundua kwamba mwanamke huyo ni msagaji, alitaka kumgeuza mke wake. Uamuzi alioufikia ni kutoroka.

Akipita gizani usiku huo anasikia watu wakiimba kanisani, anasogea karibu na kuingia ndani kwani amegundua ni siku ya Mkesha wa Pasaka, ameketi nyuma kabisa akiwaza, mahubiri hayamwingii kichwani mwake kabisa. Ibada ilipokwisha alimfuata Mchungaji na kumsimulia historia yake, kwa huruma Mchungaji huyo alimchukua na kwenda kumtambulisha kwa mke wake, huo ndio ukawa mwanzo wa kuishi nao, wakamchukulia kama mtoto wao na kumpeleka shule.

Priscilla akaanza kufurahia maisha lakini baadaye mke wa Mchungaji alipata nafasi ya kwenda kusoma mjini Nairobi, akawaacha wawili tu ndani ya nyumba, Priscilla hakuwa na wasiwasi wowote akiamini Robert Njenga alikuwa ni mtumishi wa Mungu na alimpenda na kumchukulia kama mtoto wake hivyo asingeweza kumdhuru.

Mchungaji akaanzisha utaratibu wa kutengeneza juisi nzuri kila siku jioni lakini Priscilla alipokunywa juisi hiyo alihisi kupata usingizi wa ajabu, akalala bila hata kujiegeuza na alipoamka asubuhi kwenda kujisaidia chooni, sehemu ya haja kubwa ilikuwa ikimuuma kupita kiasi, alikuwa amechanika na hakufahamu kilichomchana kwani kabla ya kulala hakuwa na tatizo hilo. Wasiwasi mwingi ulimwingi lakini hawezi kumuuliza Mchungaji Robert. Je, nini kitaendelea katika maisha ya watu hao wawili? SONGA NAYO?
    (30 September 2008)
Views: 669 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

Uchokozi wa Kimahaba waweza kuimarisha upendo kwa wanandoa -2

Mahaba  
Uchokozi wa Kimahaba waweza kuimarisha upendo kwa wanandoa -2 Jumanne nyingine wapenzi wasomaji wa safu hii, ambapo kwa mapenzi ya Muumba wa vyote tunakutana tena katika safu yetu hii maridadi. Wiki hii nitakuwa ninaendelea na mada niliyoianza wiki ya jana....
    (30 September 2008)
Views: 335 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

MVUA YAITESA DAR

photos  
MVUA YAITESA DAR
Mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, leo imesababisha baadhi shughuli kusimama kama inavyoonekana pichani wafanyabishara wa Soko Kuu la Kariakoo hapa jijini, wakifanyabishara katika mazingira magumu baada ya mvua hiyo kufurika eneo lao la kazi.

KIMVUA KIDOGO TU, BONGO NYAKANYAKA
MVUA YAITESA DAR
Jamaa huyu pichani alinaswa na kamera yetu leo mchana, akizibua mrefeji wa maji machafu katika mtaa wa Swahili jijini Dar es Salaam, baada ya maji ya mvua kutuama hapo kutokana na miundo mbinu mibovu.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL

    (29 September 2008)
Views: 90 | Maoni (0) |

 

(SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUARA WA MAHABA - 11

Mahaba  
ILIPOISHIA IJUMAA..
Wakati nikiwa katikati ya shughuli hiyo pevu, mara Lina akaanza kuongea vitu ambavyo sikuvielewa, lakini baadaye akanichanganya baada ya kutaja jina la mtu ambaye simfahamu.
?Dismas, Dis, nipe raha jamani....tamuuu...? nikapagawa.
?Nani Dismas?!? Nikamwuliza kwa ukali.
?Ingiza bwana, endelea kwanza...?
?Sema nani Dismas??
?Boyfriend wangu!?
?Nini??
?Kwani hujasikia??
?Sasa ndiyo unamtaja hapa??
Nikachomoa mchi haraka kwenye kinu kisha nikarukia kwenye sofa kubwa.
?Kibwana njoo basi mpenzi!?
?Siwezi mapenzi ya aina hii? Nikaonyesha hasira....
    (29 September 2008)
Views: 5042 | Maoni (12) | Soma Zaidi

 

HAPA TUMESHTUKIWA, TUHAMIE KIJIWE KINGINE

photos  
HAPA TUMESHTUKIWA, TUHAMIE KIJIWE KINGINE
Kijana huyu aliyelala ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amedaiwa kuwa na tabia ya kujiangusha makusudi na watu wanapojitokeza kujua kilichomsibu, hujielezea kuwa na matatizo mbalimbali ambayo si ya kweli, pichani akiinuliwa na rafiki yake baada ya watu kuwabaini na kuwaumbua juu ya janja yao maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

MDOSI ANAPOKOLEZWA NA DEMU WA KIBONGO
HAPA TUMESHTUKIWA, TUHAMIE KIJIWE KINGINE
Jibaba hili la kidosi lilinaswa na kamera yetu usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam, likiserebuka na kuonesha kukolea kwa demu wa kibongo katika Bonanza la Bendi ya Akudo Impact, juhudi za mapaparazi wetu kujua kama mdosi huyo ndio shemeji yetu au laa, ziligonga mwamba baada ya kukataa kuzungumzia hilo.
PICHA : RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA / GPL
    (29 September 2008)
Views: 147 | Maoni (2) |

 

JAMANI SOMENI GAZETI LA CHAMPIONI

photos  
JAMANI SOMENI GAZETI LA CHAMPIONI
Gari la Kampuni Global Publishers likiwa ndani ya Uwanja wa Taifa, likiwahamasisha mashabiki wa soka Nchini wasome magazeti ya Championi yanayotolewa mara tatu kwa wiki, Pia wanunuwe magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani, Risasi,Ijumaa Wikienda, ili wapate koponi ya kushiriki katika Bahati Nasibu ya kujishindia Benz.

TUNAPENDEZA JAMANI
JAMANI SOMENI GAZETI LA CHAMPIONI
Mashabiki wa soka wakiangalia mchezo wa mpira kati ya Simba na Mtibwa ya Morogoro, wakiwa wamevaa fulana za gazeti la Championi katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
PICHA NA ISSA MNALLY / GPL

    (29 September 2008)
Views: 144 | Maoni (1) |

 

Ooh! TID atendwa ufirauni gerezani

ijumaa wikienda  
Ooh! TID atendwa ufirauni gerezani Catherine Kassally na Rhobi Chacha
Ikiwa leo ni siku ya 68 tangu ?suspataa? wa Bongo Flava, Khaleed Salum Mohamed ?TID? ahukumiwe kifungo cha mwaka mmoja jela, mwanamuziki huyo amelieleza Ijumaa Wikienda matukio yote ya ukatili anayotendwa ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam...
    (29 September 2008)
Views: 2431 | Maoni (44) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2 3 ... 18 19 20  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Author: admin


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo