Washindi watatu wa droo ndogo ya kwanza katika Bahati nasibu ya Shinda Benz au Mitisubishi Pajero inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd wamepatikana.
Washindi hao ni Bi.Zubeda Mkangumbe aliyejishindia seti ya Sofa za kisasa, Hamida Kissere aliyejishindia kabati la nguo na Iluminata V.Bunga aliyeondoka na Dressing table.
Droo hiyo ilichezeshwa jana katika viwanja vya Bakhresa Manzese Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wananchi pamoja na maofisa kutoka Bodi ya michezo ya Bahati nasibu nchini ambao ni Bakari Maggid na Emmanuel John Ndaki.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa majina ya washindi hao, Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdalah Mrisho alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutuma kuponi zao ili kuweza kujishindia zawadi kemkem ambazo zitapatikana katika droo zingine zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
?Pamoja na zawadi nyingi ambazo tunatarajia kutoa, lakini zawadi kubwa ni gari mbili aina ya Mercedes Benz na Mitsubish Pajero.Tunaomba wasomaji wetu waendelee kutuma kuponi kwa wingi ili kujiwekea nafasi nzuri ya kushinda?alisema Meneja huyo.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio ya wakati wa uchezaji droo hiyo
Baadhi ya wananchi wakichanganya Kuponi tayari kwa kuchagua washindi.
Msanii mahiri aitwaye Wabojo alitoa burudani safi wakati wa droo hiyo
Mhariri mshauri wa gazeti la Uwazi Elvan Stambuli akimkabidhi mwanadada huyu kitabu cha hadithi ya Machozi na Damu baada ya msichana huyu kujibu swali kwa ufasaha.
Wanenguaji hawa Veronica Stepahano?Chichinaa? na Abdul Nohamed wakisindikiza droo hiyo.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Abdalah Mrisho akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa washindi katika droo hiyo.
SALUNI POPOTE PALE! Vijana hawa walinaswa na kamera yetu maeneo ya Manzese Jijini Dar es Salaam wakinyoana nywele mtaani.Hali ngumu ya maisha inasababisha watu wengi kushindwa kumudu gharama ya Saluni. Picha zote na Christopher Lissa
Wakati kipute cha kumtafuta Miss Tanzania mwaka 2006 kinaanza, wengi walimgaia nafasi ya kwanza, lakini baada ya matokeo alipoteza kura hizo na kumfanya abambe nafasi ya 3. Ni Lisa Jensen, ndiye anayekumbana na Mamuu katika safu hii ya Ten Questions wiki hii....
Na Imelda Mtema Lile sakata la Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim kudaiwa kutembea na mume wa mtu aitwaye Mwinyi Ahmed limefikia tamati kufuatia Mhariri wa gazeti hili na uongozi wa Kampuni ya Global Publishers, kuwakutanisha wawili hao na kuongea nao huku akiwataka kuvunja uhusiano wao haramu....
Na Mwandishi Wetu Mnenguaji ?kipotabo? ambaye yupo ?sex? zaidi, Susan Chubwa ?Queen Suzy? hivi karibuni alitwangana ?kiroho mbaya? na mwanamke anayeitwa, Mary Jackson....
Mariam Mndeme na Amina Salim Msanii mwenye heshima tele katika uga wa vichekesho nchini, Amir Athuman ?King Majuto?, hivi sasa ameipa kisogo fani hiyo na kujikita kwenye uganga wa kienyeji (usangoma)....
KWA WASOMAJI WAPYA Ukishazipata zile tura, tafuta sindano mbili ambazo hazijatumika kabisa, wala sindano hizo zisiwe zina kutu. Umuhimu wa kuwa mpya ni kujaribu kupambana na nguvu zao ambazo wakati mwingine zinaweza kukudhuru. Chukua uzi mpya ambao haujatumika na baada ya kupata vitu vyote hivyo, utaanza kutumia hatua hizi zifuatazo ili uweze kuwaondoa na kuwafukuza kabisa. Endelea...
Bwana na bibi Massawe ambao ni wazazi wa Richard, mwandishi wa habari Mtanzania aliyejishindia tuzo ya ushujaa baada ya kuripoti vyema vita vya Irak akifanya kazi na shirika la utangazaji wa SkyNews na baadaye kurejea nyumbani kumuoa msichana aitwaye Anitha na kufariki siku chache baadaye kwa ajali iliyoleta utata wakiwa mbugani Serengeti, wamerejea kutoka Kibosho huko Kilimanjaro walikokwenda kwa ajili ya mazishi ya vijana hao wawili.
Kitu cha kwanza walichofanya ni kuwatembelea wazazi wa Anitha nyumbani kwao ambao waliwapa habari za kusikitisha kwamba kila siku usiku, Richard na Anitha huenda nyumbani kwao na kuita wakiomba nguo na kamera! Jambo hili bwana na bibi Massawe hawakuliamini kabisa wakidai wazazi hao walikuwa wakiwindwa na ugonjwa wa akili na walistahili kumuona daktari mapema kabla hali haijawa mbaya.
Waliyasema hayo bila kujua wao pia hali hiyo ingewapata, kwani usiku wa siku hiyo tu sauti za Richard na Anitha zilisikika dirishani wakiomba nguo na Kamera! Bwana na bibi Massawe wakachanganyikiwa kabisa, hawakuelewa ni kitu gani kilikuwa kikitokea, isingewezekana wawe pia wanawindwa na ugonjwa wa akili wakati walifahamu kabisa! Hofu kubwa ikawashika. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO?
Inawezekana ni jana tu, umeachwa na mpenzi wako unayempenda kwa moyo wako wote. Wakati mwingine inaweza kuwa unajiona huna thamani tena katika maisha yako, unajichukia mwenyewe kutokana na fikra mbaya zinazoutawala ubongo wako.
Na Adolph Balingilaki Baada ya kuwa kisiki kigumu kwa Wekundu wa Msimbazi, mlinda mlango wa kimataifa wa Yanga, Circovick Obrien amesema kuwa nguvu zake anazielekeza katika kutafuta namba katika timu ya Taifa ya Serbia...
George Kayala na William Macha MABINGWA wa soka nchini Yanga, kesho Jumamosi, wanatarajiwa kujihakikishia pointi 30 watakaposhuka Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kukipiga na Polisi Moro, ukiwa ndiyo mchezo wa kufunga pazia la mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom iliyoanza Agosti 22, mwaka huu...
Adolph Balingilaki na Khadija Mungwai Baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga, Simba kesho Jumamosi inatarajia kushuka katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kujiuliza kwa Moro United....
Sato, binti mwenye sura ya kuvutia mfanyakazi wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya NACL, mchumba wa kijana aitwaye Greyson ambaye wanafanya kazi ofisi moja anaugua kikohozi na kuamua kwenda hospitali ambako daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dk. Terrence Kisendi amegundua Sato ana tatizo kwenye moyo wake na kuamua kumfanyia upasuaji. Ingawa Sato alibisha sana mwanzoni akidai hakuwa na tatizo la moyo, ushawishi wa Greyson ulimfanya akubali kupasuliwa kwani kulikuwa na siku chache tu mbele kabla hawajafunga ndoa na hakutaka siku ya harusi wapate matatizo! Kwa shingo upande Sato akakubali na kuingia chumba cha upasuaji akiamini angetoka salama lakini haikuwa hivyo, akafa akiwa juu ya meza ya upasuaji!
Baada ya kifo chake, Dk. Terrence alimkabidhi kijana mmoja aitwaye Albert kisanduku na kumwamuru akikimbize uwanja wa ndege wa Mwanza ambako alikabidhi kisanduku hicho kwa rubani wa ndege iliyokuwa imekuja mjini humo kubeba minofu ya samaki, baada ya kukabidhi naye alipewa kisanduku kingine na kuondoka nacho hadi nyumbani kwa Terrence ambaye alikipokea na kukuta kuna maburungutu ya dola, akachukua kiasi kidogo na kumkabidhi Albert ambaye aliondoka, mbele kidogo akapata ajali ya gari na kufa.
Kifo cha Sato kilipokelewa kwa mshtuko mkubwa sana familia yake, haikuwa tayari hata kidogo kukubali kwamba kilikuwa ni cha kawaida, ikabidi waombe mwili wake ufanyiwe uchunguzi ili kujua kilichomuua. Wizara ya Afya ikamteua Dk. Bernadetha Ndadayo kuifanya kazi hiyo, tayari amemaliza na anaingia kwenye chumba cha mikutano kusoma matokeo ya uchunguzi huo, alipoanza kusona kidogo kikohozi kikamshika. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYOÖ
Mwanamke huyu pichani anayejishughulisha na kazi ya ombaomba leo mchana alinaswa na kamera yetu akiwa taabani kwa njaa maeneo ya Posta jijini Dar es Salaaam, baada ya kuomba kutwa nzima bila mafanikio.
WANAHABARI WAZINDUA MTANDAO WAO Mwenyekiti wa mtandao wa wana habari huitwao NEJAC ambao umetangazwa leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Bwana Hussein Siyovelwa akizungumza na wanahabari katika utambulisho wa mtandao huo, kushoto ni Bwana Philbert Mmary, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa mtandao huo. PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta International' usiku wa kuamkia leo walitambulisha staili mpya ya uchezaji hiitwayo 'kisigino' katika ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam kama wanenguaji wa bendi hiyo wanavyoonekana pichani baada ya kunaswa na kamera yetu.
MI' MTU MZIMA DOGO MOTO WANGU HUUWEZI Muimbaji wa African Stars 'Twanga Pepeta International' Saleh Kupaza licha ya utu uzima alionao lakini kiuno chake balaa, pichani akishindana na kunengua na mnenguaji wa bendi hiyo Abilahi Saleh Zungu aliye kushoto.
KUPAZA UMETUKUNA MI' NA MKE WANGU Muimbaji wa Twanga Saleh kupaza akipewa 'hi' na shabiki mmoja alifika na mkewe katika ukumbi wa Mango Garden waliofika kuhudhuria onesho maalum la usiku wa Zain baada ya kuwakuna kwa minenguo yake. PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
Mashabiki mbalimbali wamemuonea huruma msaanii maarufu wa maigizo nchini Blandina Chagula ?Johari? kutokana na mwili wake kupungua uzito kwa kiasi kikubwa huku baadhi wakiuliza kama mwanadada huyo anaumwa...