Wakiongea na gazeti hili katika nyakati tofauti wadau hao wa filamu walisema kuwa, huko nyuma msanii huyo alikuwa na afya nzuri lakini sasa amekonda na kurudi kuwa mdogo kama mtoto.
?Heh! Huyu ni Johari ninayemfahamu mimi au mwingine? Mbona kakonda hivi? Au anaumwa? Maana anaonekana kupungua sana huku akionekana kama mtu aliyeathirika kisaikoljia,?aliuliza Jacqueline John mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kufuatia tetesi hizo za kuumwa kwa Johari, Amani lilimtafuta ili kuondoa utata ambapo mwenyewe aliamua kutia timu katika ofisi za gazeti hili ili kutoa ufafanuzi juu ya afya yake.
Akiongea na mwandishi wetu Johari alisema kuwa, skendo mbalimbali ambazo zimekuwa zikiandikwa katika magazeti dhidi yake ndizo zinazomkondesha hali inayomfanya kadiri siku zinavyokwenda mwili wake kuzidi kupungua.
?Yaani mimi maskendo yanayotoka katika magazeti kila kukicha yananichosha na kunichanganya akili kiasi cha kuhisi kuchanganyikiwa. Kwa kweli nawachukia sana mapaparazi kwasabau wananikosesha usingizi?alisema Johari Aidha msanii huyo ametanabahisha kuwa, hivi sasa hayupo freshi kisaikolojia na anawaomba watu wanaomfuatilia waachane na maisha yake kwani anahitaji kuishi kwa amani zaidi.
?Unajua kuna kipindi huwa nakaa na kufikiria kwanini naandamwa hivi lakini baadae nagundua kwamba haya yote ni sehemu ya maisha,?aliongeza kusema Johari.
|