arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » ijumaa » REDIHENDED!

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» Maaskofu waionya serik ...
» WALIOPATIKANA HAI WATOB ...
» Unavyoweza kukabiliana ...
» MGAMBO WA JIJI
» UTOAJI WA ZAWADI MOVEN ...
» Jinsi ya kumbaini mwan ...
» Wema amnasa Richard

REDIHENDED!

ijumaa

REDIHENDED! Kikao cha usuluhishi kilichochukua saa moja kilifanyika kwenye ofisi za Global zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar es Salaam licha ya kujitokeza kwa mizozo ya hapa na pale ya wawili hao kila mmoja akivutia madai yake kwamba ni ya kweli kuliko ya mwenzake.

Katika kikao hicho, Mwinyi ambaye pia ni Mr Dar es Salaam 2006, alikiri kumtapeli kimapenzi Miss Tanzania huyo, akijitetea kwa kusema kwamba, alifanya hivyo kutokana na mahaba mazito mazito, makubwa makubwa aliyokuwa akipewa na mrembo huyo kutoka Kanda ya Ziwa.

Akiendelea kujichana mwenyewe, Mwinyi ambaye alidai ana miaka 24 na siyo 18, alisema kuwa, penzi alilokuwa akipewa na Miss Tanzania huyo hakuwahi kulipata popote pale katika maisha yake kiasi kwamba alifika mahali akamtenga mkewe ili alifaidi penzi hilo kwa raha zake.

?Kusema ukweli, hata nilipooa, Nasreen aliniuliza, nikataa kwani mapenzi mazito aliyokuwa akinipa Nasreen sijawahi kuyapata popote. Alikuwa akinipa mapenzi yale yanayohitajika mwanaume kupewa, au siyo bab..ooh sorry, eti nilitaka kusema baby,? alichonga Mwinyi na kusababisha mshangao kutoka kwa Nasreen.

Hata hivyo, akasema anawaomba radhi Watanzania wote kwa kitendo chake cha kumtapeli Miss Tanzania huyo kwamba hana mke, hajafunga ndoa na wala hana mchumba zaidi ya yeye (Nasreen) na kusisitiza kuwa, uhusiano wao wa kimapenzi na mlimbwende huyo UMEKUFA kwa faida ya ndoa yake na majukumu ya Nasreen kama Miss Tanzania.
Aidha, Mwinyi aliyekuwa amevaa suruali ya ?jinsi? iliyokatiza makalio maarufu kama Kata K, alisema anamuomba radhi mkurugenzi wa mashindano ya Miss Tanzania, Anko Hashimu Lundenga na Kamati yake yote kwa kitendo alichofanya kwa vile kimewatia kichefuchefu hata wao.

REDIHENDED! ?Hata hivyo, ningependa kuiomba radhi Kamati ya Miss Tanzania, anko Lundenga pia kwa kitendo nilichomfanyia mrembo wao. Naamini niliwachefua na wao,? alisema Mwinyi aliyevaa kofia ya soksi kichwani.

Mwinyi aliendelea kuzimimina samahani zake kwa mkewe kipenzi, Zahra kwa kitendo cha kumkana si mkewe na kumsaliti kwa kutembea nje ya ndoa akisema ni shetani tu alimpitia, ?lakini nampenda sana mke wangu,? alisema.

Akiendelea kudomoa, Mr Dar es Salaam huyo alisema toka kuzagaa kwa habari zake na Nasreen amekuwa akipokea meseji na kupigiwa simu na watu mbalimbali wakimlaani na kumuita ni muuaji, firauni, fisadi wa mapenzi, mbadhirifu na mnyanyapaa wa ndoa, hasa wale wanaofahamu kwamba ana ?jiko? tayari.

Akiendelea kuongea huku akijisahau na kumuita Nasreen jina la mapenzi, Mwinyi alisema anamuombea samahani mama yake mzazi kwa watanzania wote, kwani na yeye alishiriki kumdanganya Nasreen.
Kwa upande wake, Shigongo aliwataka kusimamia maadili yao kwa kila upande kwani jamii inawatazama na inawategemea kubadilika kuhusu hilo.

Alimtaka Mwinyi kukomaa na mkewe, Zahra huku akimsisitizia Nasreen kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya kwani jukumu lililo mbele yake la kuwaikalisha Tanzania kwenye kinyang?anyiro cha Miss World kitakachofanyika Afrika Kusini mwezi Desemba ni kubwa na linahitaji utulivu wa akili na amani ya moyo.

Awali, Mr Dar es Salaam huyo alitinga mwenyewe katika ofisi za Global na kudai anataka kuweka mambo sawa lakini akionekana kupingana na baadhi ya madai ya Nasreen kwamba yalimdhalilisha wakati ukweli siyo huo.

REDIHENDED! Ndipo alipoitwa Nasreen huku Mr Dar huyo akiendelea kubwabwaja kuhusu madai ya Nasreen kwamba baadhi si ya kweli.
Hata hivyo, baada ya Nasreen kufika, naye akiwa hajui kama angemkuta ?mbaya? wake huyo, kimya na mshituko vilitawala kwa muda mpaka pale Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo alipoanzisha baraza la kuisaka suluhu ambapo Mr Dar huyo alikiri kumtapeli kimapenzi Nasreen.

Kwa upande wake, Nasreen alikubali ombi la Mwinyi na kusema hata yeye kwa ombi hilo mambo yameisha na kuweka wazi kwamba, mapenzi yao HAYAPO TENA zaidi ya kaka na dada.

Wakati wa kuondoka, Mr Dar aliyefika kwenye ofisi za Ijumaa na gari la Lady Jaydee, alimtaka Miss Tanzania waongozane, lakini alikataa akidai alikuwa na usafiri wake na awe na amani tu.


 (Votes #: 4)
    (31 October 2008)
Soma Zaidi: 1544 | Maoni Yako (26)

Udaku Mwingine

ijumaa
 
  • Nasreem ni mwizi tu
  • NASREEM ANYATIWA NA MSHIRIKI BIG BROTHER
  • KUMBE: Nampa uroda mume wa mtu!
  • CHANGIA MADA YA LEO!
  • Miss TZ 2008
  •    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Author: admin


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

    hit counter

     

    2008 © globalpublisherstz.com