Mnenguaji mahiri wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Suzan Chuwa maarufu kama Queen Suzzy akiwa amemdandia shabiki baada ya kupandwa na mzuka katika onesho la bendi hiyo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
MUNENE NA MUNENE Mfanyabiashara jijini Dar, Pius Rutta maarufu kama Mzee wa Pamba akiselebuka na kimwana mwenye umbo la ubwanyenye kama yeye mwenyewe katika onesho la FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' lililofanyika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Jana Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars, iliibugiza timu ya Taifa ya Sudan mabao 3-1 katika mchezo wa kufuzu kucheza fainali za mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa ndani uliofanyika Uwanja mpya wa taifa jijini Dar, pichani mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa timu hiyo na kupeleka dhahama golini kwao.
Hawa ni Bahati Bukuku na Rose Muhando ambao ni waimbaji mahiri na maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania. Ingawa wote ni wakali, lakini nani zaidi? Tupigie kura yako (angalia upande wa kulia mwa ukurasa huu)
Muasisi wa kipindi cha Mitikisiko ya pwani kinachorushwa hewani na Radio Times FM, Hadija Shaibu au Dida wa G. kama anavyojiita baada ya kunanihiwa na Mchopanga, akimlisha keki Mkurugenzi wa kituo hicho, Rehule Nyaulawa katika sherehe za kutimiza miaka minne ya kipindi hicho zilizofanyika Msasani Club, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. PICHA ZOTE MUSA MATEJA NA RICHARD BUKOS /GPL
Bi. Christina Edward aliyejitambulisha kama shemeji wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye yeye na mwenzake Basil Mramba jana walifikishwa Mahakama Kuu kuomba kulegezewa masharti ya dhamana. PICHA NA RICHAR BUKOS/ GPL
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TMARC, Nelson Karanja akimpigia simu mmoja wa washindi wa droo ya saba ya Sikia Kengele jana ambapo mshindi huyo alijishindia muda wa maongezi wa Tsh.80,000/= kwa kutuma neno Sikia kengele kwenda 15796, kulia ni Afisa Mipango wa kampuni hiyo, Said Amori. PICHA NA RICHARD BUKOS/ GPL
Kiguru juu, ndivyo alivyokuwa akijiachia mrembo huyu baada ya kupandisha mzuka katika shamrashamra za miaka minne ya mitikisiko ya Pwani iliyofanyika New Msasani Club, usiku wa kuamkia leo. PICHA NA RICHARD BUKOSI/ GPL
Katika hali ya kushangaza, wavunja mbavu wa Kundi la Ucheshi la Orijino Komedi walikamatwa na kushikiliwa kwa muda na Polisi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kutinga mahakamani hapo kwa nia ya kuwaigiza mawaziri wa awamu ya tatu, Basil Mramba na Daniel Yona...
Wakili maarufu kutoka Marekani John Cochran amekuja nchini Tanzania kumtetea Dina katika kesi ya mauaji inayomkabili na anafanikiwa kumwokoa na kifo cha kunyongwa baada ya kutumia kipengele cha umri alipokuwa wakati anaua, Dina alikuwa na miaka kumi na sita wakati huo. Kifungo chake kinabadilishwa na kuwa cha maisha jela!
Ni siku ya masikitiko makubwa kwa watu wengi lakini kwa Dina ni ahueni kwani kwake ni bora kutumikia kifungo cha maisha akiendelea kuwaona watoto wake kuliko kunyongwa na kufa! Dk. Ian Duncan na watoto wa Dina wanashindwa kujizua na machozi kuwabubujika wanapomwona Dina akipakiwa ndani ya Karandinga la Polisi tayari kwa kupelekwa gerezani. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Hii hapa Jumamosi nyingine tunakutana tena katika safu yetu pendwa ya Uwanja wa Huba. Sina shaka utakuwa u mzima wa afya njema kwa uweza wa aliye juu. Ukweli ni kwamba palipo na Mungu, shetani hawezi kusogelea hata siku moja, huo ndiyo ukweli rafiki zangu...
Mwanadada huyu bubu ambaye pia ni kiziwi, amekuwa akiwashangaza watu kwa kukata nyonga za kufa mtu katika maonesho ya makundi ya taarabu kama alivyonaswa na kamera yetu katika onesho la kundi moja lililofanyika Mango Garden jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
WEE NJEMBA, ACHA UROHO Baada ya Kiziwi/Bubu huyo kuzidisha kufuru ya nyonga njemba lenye ukwasi lilianza kumsarandia. kama ni kiziwi kweli anausikiaje muziki huo, au kiziwi feki?. PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Kimbembe cha matumizi mabaya ya madaraka ambacho ‘kimechombeza’ mawaziri wawili wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba na Daniel Yona kuburuzwa kortini, kimeanza kutoa tafsiri yenye wigo mpana kwamba hatopona kigogo yeyote mwenye skendo ya ufisadi...
Mtoto Glory mwenye umri wa miezi minne tu, ambaye katika hali ya kushangaza anazungumza, amezidi kuibua maajabu zaidi na kuwafanya wakazi wa mjini hapa kumiminika katika Mtaa wa Bin Seif kumshuhudia...
Ndoa ya aliyekuwa mshiriki na mshindi wa Big Brother Afrika III, 2008, Richard Bezuidenhout iko vululu vululu kufuatia habari iliyoandikwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa Wikienda) kuwa amewahi kujihusisha kimapenzi na msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Janeth...