Mamuu: Mambo Big Brother? Nini tofauti ya maisha ya zamani na sasa kwa upande wako? Richard: Mambo poa, tofauti ipo kubwa zamani nilikuwa mtu wa kawaida hivi sasa supastaa hivyo nafanya vitu kwa uagalifu kuliko zamani.
Mamuu: Ni nchi gani ambayo unapenda kwenda kufanya maisha kama ikitokea ofa ya aina hiyo? Richard: Ni Canada kwa sababau ni Nchi ambayo anatoka mke wangu na mke wangu ni mwema basi naamini wote watakuwa wema.
Mamuu: Unaichukulije BBA, kama ikitokea ndugu wako wa karibu anataka kushiriki unamruhusu? Richard: Naichukulia poa, namruhusu hata ndugu yangu kwa sababu ni kama filamu, ni mchezo mzuri na nauheshimu kwa sababu umenitoa.
Mamuu:Vipi uliporudi kutoka BBA ulipima afya yako? Richard: Huwa tuna kawaida ya kupima kila baada ya miezi mitatu mimi na mke wangu hivyo nadhani jibu umelipata, nipo salama kabisa.
Mamuu: Ni kweli kuwa huwa unapata tenda za kufanya kazi katika nchi mbalimbali lakini mkeo huwa anakuzuia? Richard: Hapana hawezi kunizuia na nilishawahi kwenda kikazi mara nyingi.
Mamuu: Unawezaje kukabiliana na matamanio ya madem tangu umetoka BBA mpaka leo maana umejulikana Dunia nzima.
Richard: Kwa kweli ni kazi kubwa, inataka moyo, kwa sababu siyo Tanzania tu hata nje wengine wanataka hadi kuninunua kwa bei kubwa,kikubwa ni msimamo naiheshimu ndoa yangu Mamuu.
Mamuu: Naomba nikuulize juu ya pesa zako ulizozipata BBA vipi zimebaki shilingi ngapi mpaka hivi sasa na umefanyia nini?
Richard: Dah, Mamuu mbona hiyo binafsi sana, ok pesa zipo kama zilivyo zipo benki na sijazionja hata shilingi, amini hivyo.
Mamuu: Mmeshawahi kuwasiliana na mshiriki mwenzio aliyerudi hivi karibuni na mmeongea nini? Richard: Ah no sijapata nafasi ya kuongea naye si unajua jinsi nilivyokuwa bize.
Mamuu: Bize na nini na kazi kubwa ulishaimaliza South? Richard: Nipo bize sana na kazi ya usanii, nafanya Filamu na hivi sasa ni dierector wa Filamu ya Kundi la Wahapahapa ambayo ina mambo mengi na inakuja kuwashika watu.
Mamuu:Hebu niambie Richard uliwezaje kumaliza bifu kubwa wewe na mkeo maana ilikuwa balaa, ulimtulizaje? Richard: Mamuu we acha,kazi kubwa ilifanyika, vikao,na kwa kuwa nampenda nilifanya juu chini,hivi ninavyokwambia yaani nimepewa ?last chance? ameniambia akisikia au akiniona tena na mwanamke wa aina yeyote achana na huyo Tatian nimemwagwa tena ya kiukweli bila msamaha hata wa Rais. sasa hivi nipo makini, naiheshimu ndoa yangu, nampenda mke wangu. ?Thats all?.
|