arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » ijumaa wikienda » TUMEWABAMBA!

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» TUMEWABAMBA!
» Mimi ni Mtanzania ?Pyua ...
» BURUDANI ZINAENDELEA
» How to Forget a Past Re ...
» Mtikila kuhojiwa na pol ...
» Meneja alinibaka na kun ...
» CCM yamkingia kifua Ric ...

TUMEWABAMBA!

ijumaa wikienda

Katika ushuhuda wetu kwa macho na kamera kwenye shamra shamra hizo zilizochukua nafasi Jumamosi iliyopita, Leaders Club, Dar es Salaam, mbali na wasanii hao kunaswa wakifanya mambo kinyume nyume, kwa ujumla Fiesta 2008 ilifana kupita maelezo.

Mastaa wawili kutoka Kundi la Orijino Komedi ambalo zamani lilijulikana kama Ze Comedy, Lucas Mhuvile ?Joti? na Emanuel Mgaya ?Masanja?, walinaswa gizani wakiwa na ?totoz? huku wakiwa wamekumbatiana ?kimtindo?.

Awali, kamera zetu ziliwaona Masanja na Joti wakiwa ?wamepozi? mbali na lilipokuwa jukwaa la burudani, lakini muda mchache uliofuata walitokea vimwana wawili ambao walijigawa kwa staili ya kila mtu na wake, hivyo kuanza ?kushoo lavu?.

Hata hivyo, Masanja aliwahi kuzishtukia kamera zetu na kutoka nduki, akimuacha solemba demu aliyekuwa amekumbatiana naye. Joti hakukimbia, badala yake alibaki amemtolea macho paparazi wetu. (picha hiyo inaonekana ukurasa wa kwanza).

Msanii mwingine aliyepoteza ?mshipa wa noma? siku hiyo ni Kiongozi wa Bendi ya Akudo Impact, Christian Bella ambaye alinaswa akimuimbisha demu nyuma ya jukwaa, akitumia takriban dakika 20 ili kumuweka sawa.

Pamoja na kupata upinzani mkubwa mwanzoni, mwisho kabisa wa ?muvi? hii, mambo yalieleweka kwa ?Stelingi? Bella ambaye alifanikiwa ?kumng?oa? kimwana aliyekuwa ?akizoza? naye kama picha ukurasa wa kwanza zinavyolonga.

Ukweli zaidi kuhusu Fiesta 2008 ni kuwa sherehe za mwaka huu zilionekana zipo ?more advanced? kutokana na ratiba zake, ubora wa wasanii waliokamua, ulinzi wa kutosha, huku jukwaa likifagiliwa kwamba ni la ?levo? ya kimataifa.

Kuhusu wasanii, mwanadada kutoka Marekani, Kate De Luna alifanya kweli, baada ya kutoa ?shoo? ya kuwaacha Wabongo midomo wazi, hivyo kumfanya kila ?Mtizedi? aliyelipa kiingilio Leaders, kusuuzika na moyo wake.

Kijana aliyetaka kuushindwa muziki kutokana na kujiingiza kwenye ?uteja?, Albert Mangwea ?Ngwea? alidhihirisha kuwa hivi sasa amerudi ?fresh? kutokana na mambo mazito aliyoyafanya jukwaani, huku ?singo? yake ya Nipeni Dili ikigeuka lulu.

Wakali wengine waliopagawisha ni Kundi la NAKO 2 Nako Soldiers, Joseph Haule ?Profesa Jay?, Seif Shaban ?Matonya?, Ali Saleh ?Alikiba?, Hamis Mwinjuma ?Mwana FA? na ?bwa mdogo? anayefanya vema kwenye mchiriku hivi sasa anayekwenda kwa jina la Dogo Mfaume.

Hata hivyo, msanii Nakaaya Sumari alipoteza mvuto jukwaani na kujikuta akizomewa, huku Aboubakar Katwila ?Q Chillah? akikosa shangwe kwa mashabiki kutokana na utangulizi wa kuimba nyimbo za TID na Papii Kocha.

Kuhusu usalama, hakukuwa na vibaka waliopata mwanya wa kuharibu utaratibu, kwani ulinzi ulikuwepo wa kutosha na kwamba watu waliolewa ?tilalila?, walilala mpaka asubuhi katika viwanja hivyo pasipo kuibiwa vitu vyao.

Mmoja kati ya watu waliopombeka na kulala mpaka palipokucha ni jamaa mmoja aliyekuwa na wajihi wa kibosi ambaye picha yake inaonekana ukurasa wa kwanza.


TUMEWABAMBA!


TUMEWABAMBA!


TUMEWABAMBA!


TUMEWABAMBA!


 (Votes #: 3)
    (10 November 2008)
Soma Zaidi: 1057 | Maoni Yako (8)

Udaku Mwingine

ijumaa wikienda
 
  • WABONGO WALIVYOJIRAMBA NA KAT DE LUNA FIESTA 2008
  • Vitimbi Mwaka Mpya
  • Ze Comedy waua!
  • NI MKOSI: Orijino Komedi ni PROBLEM, soo la Channel Five bado kidonda kwao
  • ORIJINO KOMEDI WAMVAA DK. SHEIN
  •    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

    hit counter

     

    2008 © globalpublisherstz.com