Gwiji huyo wa wachawi, aliongeza kunieleza kuwa, mtu anayehitaji utajiri wa majini akiwa kwa mganga wake anaweza kupewa kamba iliyo na ndoano kwa ajili ya kutimiza moja ya masharti aliyopewa na Rufita.
Baada ya kupewa kamba hiyo, mganga atamwambia aitupe uwanjani kama wafanyavyo wavuvi wavuapo samaki, kisha aanze kuivuta.
Mzee huyo aliongeza kuwa baada ya mganga kumweleza hivyo, mteja wake itabidi atekeleze na baada ya kuifunga atamtaka aivute kamba hiyo.
Atakapokuwa akiivuta mganga watamuuliza kama ni ngumu, kwa kuwa itakuwa ngumu atamwambia aendelee kuivuta hadi kitu kilichonasa kisogee karibu yao.
Mzee huyo huku akitabasamu aliongeza kuwa baada ya mtu anayehitaji utajiri kuivuta kamba ataona kitu kilichonasa ni mtu aliyetakiwa na Rufita, anaweza kuwa mama yake mzazi, mtoto wake, baba au mdogo wake wa damu.
Gwiji huo wa wachawi aliongeza kuwa kwa kawaida ni lazima mtu huyo akiwa analia au mwenye huzuni atamwita ndugu anayetaka kumuua ili apate utajiri na kusema: “Fulani ni kweli unataka kuniua kwa sababu ya pesa?”
Kama ni mama au baba atasema: “mwanangu (atamtaja jina), kweli unaniua kwa ajili ya utajiri?” Atafanya hivyo huku akitiririkwa na machozi.
Mzee huyo alinieleza kwa kuwa tayari mtu husika atakuwa amesaini mkataba wa kutekeleza masharti aliyopewa na Rufita itabidi kitu kinachoitwa huruma akiweke pembeni na kuamua kumuua mzazi, mwanaye au nduguye kwa njia atakayoelekeza na mganga wake.
Gwiji huyo alinieleza kuwa kuna njia nyingi za kuua kama kumchinja kama kuku, kumpiga kichwani na kitu kizito au kumdunga machoni kwa sindano nk.
Mtu aliyenaswa hutoweka katika mazingira ya kutatanisha ndipo mganga atamfahamisha mteja wake kwamba nyumbani kwao tayari kuna msiba wa mtu aliyemuua.
Kutokana na hofu niliyokuwa nayo baada ya mzee huyo kunieleza habari hizo, aliniangalia usoni, akatabasamu na kusema: “Kijana wangu, kazi yetu ni ngumu sana na inatisha, lakini utaiweza kwasababu wewe ni jasiri sana”. Baada ya kunieleza hivyo aliendelea kunieleza kuwa, mtu huyo akiwa kwa mganga atafanyiwa ndumba na kupewa maelekezo ya nini cha kufanya atakapofika msibani.
Aliongeza kuwa mambo hayo hutofautiana kati ya mganga na mganga kwani mwingine atamweleza mteja wake akifika asithubutu kulia au kwenda moja kwa moja kuiangalia maiti.
Mganga mwingine anaweza kumweleze mteja wake akifika msibani aangue kilio hata kujifanya kazimia kuonesha ni jinsi gani alivyo na uchungu na marehemu lakini moyoni akifurahia mambo yake mumnyokea muda si mrefu.
Mzee huyo aliendelea kunieleza kuwa, masharti mengine yanakataza mtu husika kuhudhuria msibani hadi upite muda fulani hivyo hata akipewa taarifa ya msiba wa mzazi, mwanae au nduguye mpendwa atawaeleza wazike kwani atachelewa kufika.
Aliongeza kuwa kutokana na masharti aliyopewa hulazimika kuchelewa ili atakapofika msibani asiwakute watu wengi na kufanya mambo aliyoelekezwa na mganga wake kirahisi.
Mzee huyo aliongeza kuwa baada ya mtu husika kutekeleza masharti ya awali, hatachukua muda mrefu mambo yake yataanza kumwendea vizuri sana kiasi cha baadhi ya watu kuhisi juu ya mafanikio yake.
Aliongeza kuwa ili mtu huyo azidi kuwa bwana mapesa na kuheshimiwa na kila mtu atalazimika kila baada ya muda kwenda kuonana na Rufita au malkia wa majini kama atakavyoelezwa na mganga wake.
Gwiji huyo alisema jambo hilo ni muhimu kukfanyika ikiwa ni pamoja na kutekeleza masharti mengine ya kawaida kama ambavyo walikubaliana na Rufita ambayo ni kama kutoa sadaka kwa maskini kila baada ya muda fulani ambapo wapo wanaofanya hivyo siku za Ijumaa, baada ya miezi kadhaa ama mwisho wa mwaka. Kuhusu masharti hayo aliongeza kuwa wapo wanaotakiwa kutoa damu za binadamu baada ya miaka mitatu hiyo ni kwa sababu wachawi wapo wengi sana hivyo huchukua muda mrefu hadi kufikia zamu zao.
Aliongeza kuwa, wapo ambao hutakiwa kufanya mapenzi na mabinti zao wa kwanza kuzaliwa au wazazi wao kwa mwaka mara moja ili kuziongezea nguvu biashara zao.
Kuhusu utaratibu wa matajiri hao kwenda kwa Rufita ama malkia wa majini kwa muda waliopangiwa, alisema kuwa ni tofauti na ule walioutumia mara ya kwanza wa kuzikwa katika kaburi au kupitia baharini baada ya kurusha mayai saba.
Ni utaratibu gani? Fuatilia wiki ijayo kujua mambo hayo ya ajabu na jinsi kijana Beka alivyofundishwa, uchawi hatimaye uganga ambao anautumia kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali, maoni, ushauri piga 0712-707630.
|