arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » ijumaa » ZIPOMPA: MIMI SIJAOA JAMANI,NIMEOLEWA

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Mpenzi mwenye tabia hizi m ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Mduara wa Mahaba (19)
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) MDUA ...
» Aisha Madinda: NGONO INANIU ...
» JACKLINE AMUANIKA ALIYEMTOA ...
» KANUMBA: NARGIS ALINITESA ...
» ZAWADI MWENZANGU!
» Niliishi kuzimu miaka i ...
» HERI MASKINI MUAMINIFU ...
» Chameleon jambazi
» NA MIMI JE?
» MSHINDI WA HON KONG ARE ...
» SABASABA 2008

ZIPOMPA: MIMI SIJAOA JAMANI,NIMEOLEWA

ijumaa

Kwa kuanzia, Mwandishi wa safu hii anaanza kwa kumuuliza:
Mamuu: Habari yako dada Zipompapompa?

Zipo: Nzuri, usiniite jina reefu ka’ treni. Niite Zipo tu kwa mkato. Lakini kana unaona hutachoka litamke lote.
Mamuu: (kicheko) Kwanza kabisa napenda kujua kama umeolewa?

Zipo: Sasa unacheka nini. Huu mwili ndivyo nilivyoumbwa ala! Nimeolewa ndiyo, mume wangu we humjui?
Mamuu: (kicheko tena). Nashukuru kwa kusikia umeolewa. Sasa Zipo, wewe una mume, lakini unafanya shughuli za u-MC ambao unakuweka nje ya nyumba yako mpaka usiku mwingi, mzee anakuruhusu kweli?

Zipo: Tulikaa kitako tukayaongea hayo, akanikubalia. Sasa unataka nini tena!
Mamuu: Wanawake wengi dada Zipo hupenda kubeba kibegi kama wewe. Je, wewe ukibeba kibegi kama hicho ndani yake unapenda kuweka nini?

Zipo: Pesa za advance ya kazi yangu ya u-MC. Kioo cha kujipodolea, nguo ya ndani na vikorokoro vyangu vingine. Wewe je?

Mamuu: (kicheko) Hata mimi. Kuna habari zinasema kuwa, una dogodogo nje ya mumeo. Na hii yote ni kwa sababu ya mitoko yako ya usiku eti ni kweli?

Zipo: (kicheko) acha kunichekesha. Hao wambeya wenu hao! Iko siku! Mimi niko bize sana, huyo dogodogo atanifaidi saa ngapi kwanza?! Isitoshe, najulikana na wengi, ningekuwa na dogodogo mume wangu angeshasikia, angeshanifurumua siku nyingi.

Mamuu: Kazi yenu ya u-MC inategemea zaidi bahati, lakini kuna madai kwamba wewe hutegemei bahati wala kujuana na watu, bali unatumia mitishamba, unasemaje kuhusu hilo?

Zipo: (kicheko kingine) Jamani nyiye ah! Watu wenye imani za kishirikina wanaweza kusema hivyo. Lakini mimi ni Mkristo safi, namtegemea Mungu. Najulikana sana na watu, nafanya kazi ya u-MC vizuri, wenye shughuli wananikubali baada ya kazi, wanakwenda kuwaambia wengine ndiyo maana napata tenda kila wakati. Namshukuru sana Mungu.

Mamuu: Inadaiwa kuwa, kutokana na kutegemea sana tenda za u-MC kwa hiyo umekuwa ukitoa mimba ili kuzuia muda wa kuibeba na kulea mtoto ni kweli?

Zipo: Sijawahi kucholopoa ujauzito kwa makusudi wala kwa bahati mbaya. Nilishazaa, watoto wakubwa nilionao wanatosha, sasa niendelee kuzaa kwanini? Si itafikia mahali mama una mimba mtoto ana mimba! Nani atatafuta jina la mtoto wa mwenzake?

Mamuu: Ni kwanini wewe MC Zipompa, tena maarufu sana lakini umekuwa na bifu na ma-MC wenzako, kwanini lakini?
Zipo: Unaposema kwanini lakini unakuwa kama una uhakika! We nani amekwambia habari hizi za uongo? Mimi sina bifu na MC yeyote yule. Kwanza wenyewe wananipenda sana kwa sababu si mchoyo wa kazi. Nikipata tenda nyingi huku sina uwezo nazo nawapa. Huyo mwenye bifu na mimi hebu mtaje.

Mamuu: Tuache huko. Kuna uvumi kwamba, mumeo uliyenaye ni kama umemuoa, kwa sababu haongei, hatoi sauti mbele yako. Anakuogopa kama vile wewe ndiye mume. Ni kweli?

Zipo: Wenye wivu wajinyonge. Mimi sijaoa jamani, nimeolewa. Mimi na mume wangu tunaishi kama wazungu. Akitoa sauti naitii kwa sababu ni mume wangu. Na mimi nikiongea ananisikiliza kama mke wake. Sijawahi kumvunjia heshima. Namtii, na yeye ananipenda.

Mamuu: Kuna habari kwamba licha ya kufanya kazi ya u-MC lakini pia wewe ni kuwadi mzuri kwa wanawake wenzako. Unalisemaje hili dada Zipo?

Zipo: Nikijitetea sana ntaonekana naogopa ukweli wewe nitajie huyo mwanaume niliyewahi kumkuwadia. Nitajie hata jina moja tu la ukoo, nikamsute sasa hivi.

Mamuu: Eti nasikia unaweza kukata ‘maji ya mende’ chupa kumi na mbili na kuku mzima peke yako?
Zipo: Hilo kweli. We mwili unauonaje huu! Kwanza kuku nakulaga mmoja na nusu kama hawa wa kisasa! Wa kienyeji mmoja ananitosha.

Mamuu: (kicheko) asante kwa ushirikiano wako dada Zipo, tutawasiliana siku nyingine.
Zipo: Haya, kazi njema mdogo wangu.


 (Votes #: 0)
    (21 November 2008)
Soma Zaidi: 572 | Maoni Yako (7)

Udaku Mwingine

ijumaa
 
  • NYOTA WAZIRI: Kutokuzaa kwangu si mkono wa mtu
  • RICHARD: AKINA NANIHII WANATAKA KUNIOA
  • Wanawake wenye pesa ?wanatununua? wenyewe
  • Sijasababisha ‘mijimama’ kupigana kwa ajali yangu
  • CHRISTIAN BELLA: Kwetu Kongo njaa kali
  •    

    #1 Author: majoy (21 November 2008 08:04)


    dada zipo nimependa sana interview yako yaani ni bomba sana, napenda sana jinsi unavyojiamini na uwazi ya nini kusema uongo?!! kipaji unacho wala si ndumba wenye wivu wajinyonge.kaza buti dadangu.

    Mdogo wako,

    Joyce - Sinza
     
    fast    

    #2 Author: QT (21 November 2008 10:04)

    ZIPOMPA UKO JUU KAMA MUASHOKI
     
    fast    

    #3 Author: Lupe Fiasco (21 November 2008 10:23)

    AISEE "QT" HATA WEWE UKO JUU MNO KULIKO MUASHOKI!UNATISHA KAMA JELA ZA KIBONGO!JOYCE WA SINZA HATA WEWE UNATISHA MAMA UNACHANGIA VIZURI SANA.HONGERA ZAKO!PIA DADA ZIPOMPAPOMPA ZIPAPILE PAPAPA.....!!!MAMBO YAKO SI MCHEZO MC KAMA UMEENDA XUL VILE SIJUI UNGEENDA XUL INGEKUWAJE UNGETISHA KULIKO....
    UNATISHA NA UKO JUU MNO,ILA TAFUTA HATA KACOROLLA NDUGU YANGU MAANA UNATAABIKA NA DALADALA MARA TAX !FANYA HIVYO MAMA..LOL


    lupeboy@yahoo.com

    LUPE-USA
     
    fast    

    #4 Author: walewale (21 November 2008 12:05)

    Hii interview ilikua tamu kama isiishe vile kweli we ni Mc maana hayo majibu yako nimeyapenda.......
     
    fast    

    #5 Author: asha (21 November 2008 13:33)

    wewe lupe acha ushamba alihiyo ujafika ukifika je uko USA si tutakoma ..ujaulizwa una kaa wapi
     
    fast    

    #6 Author: Lupe Fiasco (21 November 2008 16:10)

    Asha mimi na wewe nani mshamba??Italy na US ni sehemu mbili tofauti.ukweli niko US,kwa majoyn alivyoandika yuko sinza ni dhambi???au wewe unavyoandika uko Italy ni dhambi???Asha najua unataka nini ila nitakupa tu usijali!

    Kwanza kabisa hongera dada Zipo ila uache kamchezo kako ka ukuwadi.Haya Lupe na Asha tatizo ninini??hebu kuweni marafiki wazuri jamani haipendezi.Asha dear nimepoteza email yako tafadhali naomba unipatie Asante!
     
    fast    

    #7 Author: Musa Kidichi (22 November 2008 05:52)

    sifa za kijinga!jamaa kwa kujifagilia huyu sifa za kijinga,jamaa ana majina mawili sifa za kijinga,humshindi fulani kwa kukandia watu sifa za kijinga! no comments zaidi feel
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

    hit counter

     

    2008 © globalpublisherstz.com