Jana ilikuwa siku maalum ya kumkabidhi zawadi yake ya simu aina ya Blackberry mshindi wa lile shindano letu la kumtafuta msomaji wa milioni 5, ambaye alikuwa ni B. Saade Nassor aliyeko Oman, Arabuni ambaye aliwakilishwa na mdogo wake Harith Nassor aishie Kinondoni jijini Dar es salaam. Pichani ni hiyo Blackberry 8700G iliyotolewa kwa hisani kubwa kabisa ya duka maarufu linalouza vipodi halisi kutoka nchini Marekani, ARISE BEAUTY SUPPLY lililopo Mikocheni, kwa Nyerere jijini Dar es salaam.
Mdau mkubwa wa muziki na msanii maarufu nchini Tanzania, Bi. Dotnata, akimkabidhi Harith (shoto) zawadi yake huku akishuhudiwa na Balozi wa Zain, Issa Michuzi (kulia), Bhoke Maro wa Arise, Rose Gaspar ambaye ni Meneja wa duka la Arise na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
..Mrisho akitoa maelekezo mafupi kuhusu simu hiyo kwa mwakilishi
....Michuzi 'ze fulanazz' akipokea zawadi kali kutoka kwa Rose wa Arise baada ya kazi kubwa ya kuratibu zoezi hilo.
..Mama Dotnata naye akipokea zawadi yake
...Mrisho naye ni kicheko tu wakati akipokea zawadi yake.
..Hapa ndipo lilipo duka la ARISE BEAUTY SUPPLY.... TUNATOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWA WASOMAJI WETU WOTE KWA KUSOMA MTANDAO WENU NA KUUFANYA KUWA NAMBA MOJA NCHINI TANZANIA. SHUKRANI PEKEE ZIWAENDEE WADHAMINI WETU.ARISE BEAUTY SUPPLY...KWA KUTOA ZAWADI NONO YA BLACKBERRY KWA MSOMAJI ALIYEBAHATIKA NA BILA KUMSAHAU ISSA MICHUZI KWA KUHAMSISHA NA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MDHAMINI NA MWISHO KABISA TUNAMPONGEZA MSHINDI, BI SAADE NASSOR!
Majeruhi wa ajali ya daladala iliyopata ajali eneo la Kipawa Jet Club, Simon Sylvester akiwa katika wodi ya Sewahaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam ijumaa. (Picha na Yusuf Badi).
katika nchi nyingi za barani Africa neno democrasia hubakia tu kama neno la kawaida lisilogusa maisha ya raia wa kawaida bali viongozi pekee.Katika maisha ya kawaida ya Mtanzania masuala ya utawala bora hayapewi kipaumbele ila kiongozi ambaye maovu yake hufaamika na jamii ndiye Watanzania wengi humtupia macho na kutaka aidha ajiuzulu au ashitakiwe.hali hii imekuwa ikiwapa viongozi wetu jeuri kwani wanajua wananchi wengi si wafuatiliaji wazuri wa mwenendo wa viongozi wao wanapokuwa madarakani hivyo hutumia furksa hii kujirundikia mali za wananchi pasipo wao wenyewe wananchi kujua.Kufuatilia mwendendo wa kiongozi wako haina maana ni kufuatilia maisha yake binafsi,bali ni kufuatilia mwenendo wake kama anakiuka katiba au la.Hapa ndipo tatizo hujitokeza kwani asilimia kubwa ya watanzania hawaijui katiba yao! si jambo la ajabu kusikia baadhi ya wananchi wa Tanzania hata neno katiba hawalijui maana yake! je hii ni sawa kwa wananchi kusema nchi yao ni ya democrasia wakati hawajui hata nguzo za hiyo democrasia? Huu ni ukiukwaji mkubwa wa democrasia ambao viongozi wanaufumbia macho wakijui kuwa mwanzo wa uelewa wa wananchi juu ya democrasia ndio mwanzo wa viongozi kuanza kuwajibishwa.Hivyo basi kama kweli Tanzania ni nchi ya democrasia kama viongozi wetu wanavyoiita,viongozi hawana budi kutafuta nyia mbadala ya kuwaelimisha wananchi wake juu ya katiba ya nchi yao ili waweze kujua pale kiongozi anapotenda sawa na vinginevyo.
Hoja ya wapinzani kumtaka ajiuzulu yayeyuka Leon Bahati WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameangua kilio bungeni kuonyesha uchungu alio nao dhidi ya vitendo vya mauaji ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), hivyo kuyeyusha hoja ya wabunge wa upinzani waliokuwa wamepania kumbana, ili ajiuzulu kwa madai kwamba, alitoa amri ya kuua wauaji ambayo ni kinyume na katiba ya nchi....
Leon Bahati, Dodoma MBUNGE wa Kwela (CCM), Dk Christant Mzindaka, maarufu kama "mzee wa mabomu", ameibuka bungeni na kueleza kusikitishwa na uzembe uliofanywa na Waziri wa Maliasili, Shamsa Mwangunga kwa kuwaongezea muda wamiliki wa vitalu vya uwinfaji katika hifadhi za taifa kinyume na maagizo ya bunge....
Ofisa huduma kwa wataje wa Tigo Zanzibar Octavian Rwegasira(kushoto), akikabidhi zawadi ya simu ya mkononi kwa Sakina Abdalah, aliyojishindia wakati wa droo ya tisa ya promosheni ya jishindidie mtaji maalum kwa wateja wa Zanzibar ambapo hafla ya makabidhiano ilifanyika sambamba na droo ya mwisho ya promosheni hiyo.
POKEA ZAWADI YA CHEREHANI Ofisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi cherehani Abdalah Juma, ikiwa ni zawadi aliyejinyakulia katika promosheni ya JISHINDIE MTAJI wakati wa droo ya tisa ya promosheni hiyo iliyochezwa wiki iliyopita wakati wa hafla ya makabidhiano ya zawadi juzi, katika ofisi za Tigo zilizoko Mtaa wa Malindi Zanzibar ambapo pia Tigo ilitangaza kuisha kwa promosheni hiyo mara baada ya kucheza droo ya mwisho.
WATU tisa wamefariki dunia na wengine zaidia ya kumi kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya gari iliyotokea jana majira ya saa kumi alfajiri, eneo ya Jet katika Barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam...
Mamaa Dotnata na Mumewe ambao ni miongoni mwa wadau wakubwa wa masuala ya muziki na sanaa nchini wakipokewa katika duka la Arise na Bi. Bhoke Maro, ambaye ni mfanyakazi wa duka hilo lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa shughuli fupi ya kukabidhi simu. Hapa Dotnata alikuwa ajiribia 'make up' na kuona jinsi ilivyo mkubali.
HONGERA KWA KUWA MWAKILISHI Dotnata (kulia) akimkabidhi simu Bw. Harith Nassor ambaye ni mwakilishi wa Bi. Saade aliyeko Oman, wanaoshuhudia kutoka kushuto ni Meneja Mkuu wa Global Pulishers, Abdalah Mrisho, Meneja wa arise Beauty Supply Bi. Rose Gasper, Bi. Bhoke Maro ambae ni mfanyakazi wa duka hilo, akifuatiwa na Muhidin Issa Michuzi ambaye ni Balozi wa Zain na Mkuu wa Wilaya ya nanihiii.
HII NI SIMU BOMBA. Mwakilishi wa Bi. Saade, Bw.Harith akimuonesha simu hiyo kijana aliyemsindikiza.
NGOJA NIKAMFANYIE SURPRISE MAMSAP Mhangaikaji wetu wa mtandao huu, Christopher Lissa, ambaye alikuwepo katika makabidhiano hayo, akimchagulia kiatu 'my waifu wake' mtarajiwa katika duka hilo.
MAMBO YA MNUKISHO Haya ni baadhi ya manukato na vipodozi vinanavyopatikana dukani hapo.
ARISE BEAUTY HAPAKOSEKANI KIPODOZI Hivi navyo ni baadhi ya vikorombwezo halisi kutoka 'majuu' vinavyopatikana ARISE BEAUTY SUPPLY hapo Mikocheni kwa Mwl. Nyerere pembezoni mwa Klabu ya Talk of the Town.
VIBUTI VYA KISASA Kwa akinadada wanaokwenda na wakati mambo ya midundo, nd’o uspime kabisa dukani hapo, hii ni baadhi tu sampuri zilizonaswa kwenye moja ya kona za duka hilo.
BIDHAA ADIMU KIBAAAO Bidhaa kama hizi ambazo ni adimu sehemu nyingine, dukani hapo hupatikana kwa wingi tena kwa gharama nafuu. PICHA ZOTE: CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS /GPL.
Na Adolph Balingilaki Baada ya wiki iliyopita, Vijana wa ‘Masauti’ (Akudo Impact) kupagawisha vilivyo katika shoo ya kunadi shindano la Jishindie Pajero, sasa ni zamu ya Wazee wa Ngwasuma (FM Academia) kurusha njiwa na Global Publishers...
Musa Mateja na Catherine Kassally Lile sekeseke la kuchafuana kati ya Masupastaa wa Filamu nchini, Wema Sepetu na Steven Kanumba, ambao walikuwa wapenzi, juzi (Alhamisi), usiku wa manane, limechukua sura mpya baada ya wasanii hao kutwangana mbele ya ‘kadamnasi’ ya watu...
Na Mwandishi Wetu Ushahidi ambao gazeti hili limeupata, unaonesha kuwa, mmoja wa Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne katika Wizara nyeti (jina lake na la wizara tunayahifadhi kwa sasa), ‘ameoza’ kwa penzi la Miss Tanzania 5 2006, Irene Uwoya ambaye sasa nyota yake inang’ara vilivyo katika Tasnia ya filamu...
Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jana (Ijumaa), alilazimika kutumia busara kumwokoa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga kuadhibiwa na Bunge kutokana na kile kilichoelezwa na Mbunge wa Kwera, Christant Mzindakaya kwamba alipuuza haki za Bunge hilo, baada ya kukubali ombi la Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Erasmus Tarimo la kuwaongezea wawindaji miaka mitatu, wakati muda wa vibali vyao umemalizika mwaka huu...
Christopher Lissa na Richard Bukos Wakati kesi mbalimbali za watuhumiwa wa kesi za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) zikiendelea, juzi (Alhamis) jioni, hofu ilitanda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo, jambo lililosababisha mahakama hiyo kuimarisha ulinzi....
Ni Jumamosi nyingine tunakutana katika safu hii nzuri ya Uwanja wa Huba, ninaamini umzima wa afya njema na upo tayari kabisa kufuatilia kwa makini nilichokuandalia kwa juma hili...
Baada ya Joan kupoteza fahamu juu ya mwili wa mumewe aliyeamini amekufa alipoganda kwenye barafu, fahamu zinamjia ndani ya chumba chenye mwanga mkali kando yake amesimama Dk. Lewis, anamfahamisha kuwa eneo hilo siyo hospitali bali nyumbani kwa Gerald Smith, tajiri mmoja nchini Marekani.
Kwa haraka anataka kujua kwanini yupo hapo, Dk. Lewis anamfahamisha kuwa sehemu hiyo ni takatifu hivyo asiwe na wasiwasi, Joan anaanza kulia anapomkumbuka mwanaye John, mumewe pamoja na familia ya Joseph, hakuwa na uhakika kama walikuwa hai.
Wakati anaendelea kupata huduma na vyakula vizuri afya na uzuri wake unaongezeka maradufu na kuonekana msichana mzuri miongoni mwa warembo ndani ya jumba hilo, akiendelea kuhudumiwa na warembo wakimliwaza, kati ya wanaomhudumia Sonia anafichua kwa kumueleza Joan wazi kuwa nyumba aliyoingia wanawake wanafanyishwa biashara ya ngono.
Baadaye Gerald Smith anaingia na kumwambia Joan anataka kumfanyisha ngono na mwanaume mmoja kati ya kumi atakaowachagua. Kitendo hicho anakipinga na kila mwanaume anayeingizwa anamkataa ambapo anamuomba Sonia amletee sindano ya sumu.
Joan anajiandaa vema ndani ya chumba hicho na kuiweka sindano yenye sumu tayari kwa kuanza kazi ya kuwachoma wanaume watakaoingizwa, baadaye Gerald Smith anafika na kuzima taa na kumwambia Bravo aingie kufanya ngono na msichana huyo. Dakika chache alipoanza kumpapasa, kitu chenye ncha kali kinaingia tumboni mwa Bravo na kupiga kelele, Joan akashtuka na kugundua mtu aliyemchoma sindano ya sumu ni mumewe, wakaanza kulia wote.
Wakati huo ndani ya chumba cha VIP, Joan anaonekana msichana mzuri ndipo mwanaume mmoja mwenye asili ya kiafrika (Black American) anamnunua na kumpeleka nyumbani kwake, Joan anaendelea kumlilia mumewe, kila anapopewa chakula anakitupa kando, saa moja baadaye mlango unafunguliwa na kuona watu watatu wakiingia, mwanaume mmoja, wanawake wawili. Hapo ndipo anashtuka na kupoteza fahamu. Je, watu hao ni akina nani? Kwanini Joan amepoteza fahamu? SONGA NAYO...