Rais wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’ Nyoshi El Saadat (kushoto) akishambulia jukwaa, wakati bendi hiyo ilipovamia ukumbi wa Vatican City Sinza, ambapo pia kulikuwa na bonge la Promosheni ya Shinda Pajero, inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa,Risasi, Amani,Uwazi na Championi.
KWA SH.400 TU UNAENDESHA PAJERO MPYAAAA! MC Elisha Thomas (kushoto) akiwa na Nyoshi wakinadi bahati nasibu ya shinda Mitisubish Pajero wakati wa onesho hilo.
WANENGUAJI WA FM ACADEMIA WAKINADI PAJERO Wanenguaji wa FM Academia wakinadi bahati nasibu ya Shinda Pajero ambapo walikonga nyoyo za mashabiki kisawasawa ukumbini hapo. PICHA NA MUSA MATEJA /GPL.
Mtangazaji nyota wa kituo cha Redio na Runinga cha East Africa Maimartha Jesse akimlisha keki mmoja wa mashabiki waliohudhuria onesho la bendi ya Akudo Impact, vijana wa masauti lililokuwa limeandaliwa na kampuni ya Manywele Entertainment inayomilikiwa na mtangazaji huyo.Onesho hilo lilifanyika ndani ya ukumbi wa Luxury Pub Temeke usiku wa kuamkia leo.Hata hivyo baadhi ya watu walimbeza mtangazaji huyo kwa kuwalisha keki watu wengi ambao walikuwa wamelewa chakali ambapo walidai kuwa Keki haiendani na Laga!
PEKECHA PEKECHA! Mashabiki hawa walinaswa wakipekechapekecha kwa staili hii wakati bendi ya Akudo ilipokuwa ikivurumisha Sebene la kufa mtu ukumbini hapo. PICHA NA CHRISTOPHER LISSA/GPL
Baada ya kinyang’anyiro kikali kati ya Bendi mbili za muziki wa dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na Akudo Impact ‘Chuo cha Masauti’ kumalizika ambapo matokeo tutawaletea baadaye, wiki hii Mtandao wako wa burudani nchini, unakuletea shindano lingine kali zaidi la wasanii wa kike katika anga za filamu nchini, nao si wengine bali ni Blandina Chagula ‘Johari’ na Nuru Nassor ‘Nora’. Hawa wote walianza kuonekana kwenye michezo ya kuigiza runingani, kupitia kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar es Salaam. Walisonga mbele na kuonesha umahiri wao kwa kushiriki filamu mbalimbali za hapa nchini. Kwa upande wake, Nora ameshashiriki filamu za Sikitiko Langu, Sweet Backreena, Upande wa Pili wa Ndoa, Johari na nyingine nyingi. Johari yeye ameshakamua kwenye Johari, Yellow Banana, Wicked Love, Fake Pastors, From China With Love, My Wife na nyingine kibao. Kazi kwako msomaji wa mtandao huu, Nani Zaidi?
Usiku wa kuamkia leo Bendi ya Diamond Musica ‘Vijana Classic’, walitambulisha rapu yao mpya ya ‘Mwanamke tabia sio bia’ ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar, ambayo ilipokelewa kwa shangwe na mashabiki ni waliofurika katika onesho hilo. Pichani muimbaji na rapa wa bendi hiyo , Didier Namba ‘Dume la Mende ‘ akipagawisha mashabiki kwa rapu hiyo.
ALLAIN MULUMBA AACHANA NA URASTA Mmoja wanamuziki waanzilishi wa Bendi ya Diamond Musica, enzi hizo ikiitwa Diamond Sound, Allain Mulumba Kashama pichani ambaye alikuwa rasta maarufu, sasa ameamua kunyoa upara na kuachana na urasta. Ni mishkaki kwa kwenda mbele.
VIUNO VYA DIAMOND MUSICA USIPIME 3.Squad ya unenguaji ya Diamond Musica ilishambulia jukwaa katika onesho hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana. PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL
Wakati mtuhumiwa wa 'soo' la ufujaji wa zaidi ya bilioni 220 katika ujenzi wa majengo pacha ya Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba akitupwa lupango, Keko jijini Dar es Salaam mtumishi wake wa ndani 'hausigeli' ametoa mpya baada ya kutoroka akihofia kuhojiwa na askari wa usalama wa taifa...
Gari la ushindi la Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, limezua utata mkubwa ndani ya familia yake baada ya mama mzazi wa Mnyange huyo, Mariam Sepetu kuling’ang’ania gari hilo na kuanza kulitafutia dalali...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, jana (Ijumaa), ilitupilia mbali pingamizi la Wakili wa utetezi, Majura Magafu anayemtetea Kada wa CCM, Rajab Maranda anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) la kupinga kupokelewa kwa maelezo ya onyo ya mshitakiwa huyo kwa madai kuwa, alihojiwa akiwa mgonjwa...
Hakuna anayeweza kusimama na kusema Mungu hajamfanyia kitu chochote kitakachomsukuma kumwambia ahsante! Huo ni ukweli ambao hauwezi kubadilika. Ndugu zangu nawakumbusha kumshukuru Mungu kwa kila tunachokifanya katika maisha yetu ya kila siku...
Joan anapatwa na mshtuko alipogundua kuwa mwanaye ana ugonjwa wa kifafa, dalili zilishaonyesha, simu yake inaita na kuongea na Dk. Charles na kumtaka aje nyumbani kwa Alex kumwangalia mwanaye, anatoka na kuingia chumbani alipomuacha mumewe na kugundua hali ya mumewe ni mbaya na asingeweza kupona.
Kwa tabu sana Bravo anamwambia mkewe amechomwa sindano na daktari wa Alex Ruben ndipo hali yake ikazidi kuwa mbaya na hana matarajio ya kupona, wakati huo anampigia simu Dk. Charles anayemwambia tayari ameshafika nyumbani kwa Alex Ruben.
Hofu ikiendelea kutanda akilini mwake kumpoteza mumewe mpendwa, Joan anafungua geti na kuingia na Dk. Charles anayempima Bravo na kugundua amechomwa sindano ya sumu, wote kwa pamoja wanajaribu kumuwahisha hospitalini ili akapate matitabu, njiani Bravo anafariki mikononi mwa mkewe.
Wote wanachanganyikiwa, Joan alilia sana na kwenda Kituo cha Polisi ili kuelezea mkasa mzima, askari walikuwa wanamsikiliza kwa makini kuliko alivyotegemea, anawaambia wazi mumewe ameuawa na Alex Ruben akishirikiana na Dk. Godwin.
Kipindi cha muda mfupi taarifa zinasambaa nchi nzima na duniani kote kuwa mwanamuziki mahiri nchini Marekani, Bravo amefariki dunia baada ya kuchomwa sindano ya sumu na baba mkwe wa pacha wake.
Ndugu wa Bravo nao waliungana na Joan kuhakikisha wanamkamata watuhumiwa wa mauaji hayo, wakati bado Joan yupo kituo cha polisi akielezea tukio zima, ujumbe mfupi wa maneno unaingia na Joan anaanza kuusoma.
Alex Ruben anasisitiza sababu ya kumuua mume wake ni mapenzi mazito aliyonayo, anaongezea kuwa alishirikiana kazi hiyo na Dk. Godwin. Mwanamke huyo anaanguka na kupoteza fahamu alipoambiwa mtoto anayekuwa naye si John bali ni mtoto Kennedy.
Kitendo cha kuanguka kwa Joan, kilisababisha Dk. Charles achukue jukumu la kumpeleka hospitalini, askari wanaingia kazini kumtafuta Alex Ruben na Dk. Godwin. Muda mfupi askari wa kike anaingia nyumbani kwa Alex Ruben akiwa na nguo za kiraia, anaambiwa na Dina kuwa mtuhumiwa ametoka muda mfupi uliopita. Je, Alex Ruben na Dk. Godwin watakamatwa? SONGA NAYO...
Waziri wa Afya Profesa David Mwakiyusa (kushoto) akiwa na Naibu wake Mh Aisha Kigoda Kulia wakiwa katika uzinduzi ofisi ya dawa za asili ya Afrika kwenye ofisi za AMREF zilizopo barabara ya Ally Hassani Mwinyi jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkali wa muziki wa Zouk hapa nchini Stara Thomas akiburudisha katika uzinduzi huo.
MAONESHO YA BIASHARA ZA CHAKULA NA USINDIKAJI YAZINDULIWA Halmashauri ya Biashara ya Nje leo imezindua maonesho ya biashara za chakula na usindikaji katika Viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es salaam pichani waliohudhuroa maonesho hayo wakiangalia bidhaa hizo.
Wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake wanatarajiwa kuondokana na kero ya usafiri baada ya barabara ya Kilwa pichani kuendelea kuboreka kama ilivyonaswa na kamera yetu eneo la Mtoni kwa Azizi Ally leo mchana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Rais wa Ireland, Mary McAleese kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Dublin kabla ya mazungumzo yao Februari 25, 2009. Alikuwa katika siku a kwanza ya ziara yake nchini humo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ukiongelea wanamitindo ambao wapo juu na jina linatajika sana huwezi kukosa kumtaja Mwanamitindo Belina ambaye ndiye hasa anayetabiriwa kuwa wa pili kutoka Fideline Iranga...
HATIMAYE aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye anatuhumiwa kutumia ofisi vibaya, Amatus Liyumba amejisalimisha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar, Jumanne wiki hii....