arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Amani » Wema atiwa mbaroni

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» MAMBO YA BOZIBOZIANA NA ...
» HOTUBA YA ERIC J.SHIGON ...
» NJIA ZA KUTAFUTA NA KUP ...
» Kondic: Nurdin, Ngassa ...
» MAGARI MATATU MTARONI
» Beyond Love -35
» ALBINO HUYU KWA MAUNO B ...

Wema atiwa mbaroni

Amani

Wema atiwa mbaroni

Mrembo huyo alitiwa katika mkono wa dola pamoja na wifi yake aitwaye Asha Jumbe walipokuwa nyumbani kwa mpenzi wake wa sasa aliyetambulika kwa jina moja la Jumbe, maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, juzi majira ya saa 5:00 asubuhi, zilifika defenda mbili nyumbani kwa akina Jumbe ambapo walifanikiwa kuwatia nguvuni Wema na wifi yake huyo kisha kuwapeleka katika Kituo cha Polisi, Magomeni.

Ikadaiwa kwamba, wakati mlimbwende huyo ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa hakauki magazetini akipandishwa kwenye gari la polisi, alionekana akitokwa na machozi huku mwenzake (Asha) akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote.

Amani lilifika katika Kituo cha Polisi Magomeni majira ya saa 6:00 usiku na kuwakuta ndugu zake Wema na Asha wakihaha kuwawekea dhamana ambapo mpaka linaondoka eneo hilo, hakukuwa na dalili zozote za kuweza kutolewa.

Aidha, alikuwepo pia mpenzi wake wa sasa akijaribu kufanya ‘mandingo’ ili akalale nyumbani na mpenzi wake huyo lakini juhudi zake ziligonga mwamba kwani taarifa tulizozipata wakati tunakwenda mtamboni zilidai kuwa, watuhumiwa hao walilala selo.

Hivi karibuni, Kanumba alifungua jalada la kesi katika Kituo Polisi Magomeni kwa madai kuwa, alivamiwa na Wema akiwa na shoga zake kisha kupigwa na kuharibiwa vibaya gari lake.


 (Votes #: 2)
    (5 February 2009)
Soma Zaidi: 2631 | Maoni Yako (17)

Udaku Mwingine

Amani
 
  • Wema Sepetu anaswa kwa wizi!
  • Wema agombewa gerezani
  • Wema, Kanumba watwangana
  • Wema alala Segerea
  • WEMA: Najuta kumfahamu Kanumba
  •    

    #1 Author: mtombakumabure (5 February 2009 01:35)

    Yeah hii habari GP hawajadanganya niliisoma kwenye magazeti mengine kama mawili hivi!Duuu Kanumba kaosha jina..Pole Wema ndio ujue mambo ya ubabe ni mabaya kama unabisha muuulize mwenzio TOP IN JAIL atakwambia!
     
    fast    

    #2 Author: wa kwetu (5 February 2009 01:52)

    hapo sawa, kashenzi sana haka kasichana
    walau kamekojolea debe,
    na kwa kuwa wazazi wamenyoosha mikono
    acha kanumba awasaidie malezi ya binti yao,
    na utakoma wema, kudadeki
     
    fast    

    #3 Author: mhh!!! (5 February 2009 02:17)

    Haya ukitoka huko tafuta balaa jingine ili uandikwe kwenye gazeti maana unaona ujiko kuandikwa uchafu wako kwenye magazeti
     
    fast    

    #4 Author: lmami (5 February 2009 03:56)

    mnanichefua na huyo kichefuchefu kazidi uliona uspa staa dili ukataka kumjohncna kanumba sasa kakuundertaker safi sana kanumba komesha huyo fisadi wa wanaume
     
    fast    

    #5 Author: Hi (5 February 2009 04:14)

    Pole sana Dada.Usijali hayo ni mapito tu.Mambo mengi yatakutokea,kumbuka Mungu ndio mpaji wa yote.Nakushauri urudi shuleni ukamalizie digrii yako.Ukiwa na Elimu pamoja na uzuri wako milango mingi sana ya Fulsa itafunguka.Ama sivyo utatumika tu kama chombo cha starehe cha wanaume.Shule ndio kila kitu .kumbuka Rais Obama amefanikiwa kuwa madarakani kwa sababu ya shule sio kingine.Uzuri ni kitu cha kupita tu.Watakuja dogodogo wengine.Lazima uanzekufikiria kuanzia sasa maisha yako ya baadae yatakuwaje.Unataka watoto wako wame na maisha gani ya Baadae?Hawawezi kuwa na mafanikio kama ya wewe uliokuwa nayo ya kuwa Miss Tanzania kama iwapo hutawajengea misingi bora,ambayo unaijenga kwa kuwa na elimu bora.
    Angalia watu kama kina Oprah wanafanya vitu vya kueleweka kwasababu ya shule.Ukitoka huko dada angu nakushauri rudi shule.Kumbuka katika mwimbo wa Ngwea "sikiliza",mna ambiwa kuwa mnamegwa mna achwa.Na ndio kinachokutokea.Jaribu kufikiri niwanaume wangapi wamekumega na kukuacha?Vipi walivyokuahidi nakukutimizia?Nimaisha gani unataka wanao waje kuiga kutoka kwako?
    Je unadhani watajivunia wakija kujuwa habari zako baadae?

    Kuwa makini dada nakutakia kila la kheri katika maisha yako!
    Hi...
     
    fast    

    #6 Author: Monica Joel (5 February 2009 05:30)

    Huyo mtoto aache ushamba, inamaana yeye ndio anajua kupenda kuliko wanawake wengine wote? Angetakiwa kwenda rumande siku 14 ili atie akili mwendawazimu mkubwa.
    Ina maana Kanumbe alikuwa akimpa nini asichoweza kukisahau?
    NAKUPA POLE MSICHANA, UTAWAPIGANIA WANGAPI?
     
    fast    

    #7 Author: mimi (5 February 2009 05:32)

    kama huna maelewano na wazazi wako unategemea nini?laana itakuandama popote uendapo,so young girl jirekebishe uache umalaya na tabia mbaya mtu ambaye ulipewa heshima ya kupeperusha bendera ya taifa kwa kuwa miss sasa umejifanya takataka!!!sasa hapa Lundenga atafanikiwa vipi kuwashawishi wazazi kuwa u miss si uhuni waache watoto washiriki!! mnaibisha sana fani hii,ma miss wa nchi nyingine wanashiriki katika shughuri za maendeleo,sio kama akina Wema!!!!!
     
    fast    

    #8 Author: awisha (5 February 2009 05:45)

    hilo ndilo swala la muhimu ili kumkomesha huyo kijidu mtu ambaye anajidai kuwa yeye ndio bomba kuliko wasichana wote. ingefaa sana hata akanyongwa ili asiendelee kuwaambukiza watu hivyo VVU kwa makusudi.
    pole sana dada kwa uliyokwishayafanya yanatosha.
     
    fast    

    #9 Author: tauss (5 February 2009 08:31)

    SIDHANI KAMA NI BUSARA KUMPELEKA POLISI MPENZI WAKO WA ZAMANI.Kanumba ningekuona una busara kama ungeyamaliza mezani.[b]Jaribu kuwa na busara hata katika uovu.
     
    fast    

    #10 Author: Mzee wa Busara (5 February 2009 09:15)

    We tauss hapo juu, unataka busara wakati kioo cha gari kimevunjwa?
     
    fast    

    #11 Author: angalia (5 February 2009 10:23)

    kanumba wewe ni mwanaume tumia busara achana na mambo ya kummpeleka mpenzi wako wa zamani mahakani na polisi, hata kama amekufanyia u****uni gani wewe play cool ndo inakuwa busara! nina hakika hapo atakuwa amejifunza zaidi ya mambo ya kupelekana polisi na mahakamani
    sasa mtu alikuvulia nguo mkalala wote na kufaidi leo mnaprove msemo kuwa there is a very thing line btn love and hate!

    wewe ni mwanaume play ya cards right and the right way ni kuacha kulumbana na mwanamke au wanawake mind ya bussiness magazeti na wanahabari watawachonganisha na kuwagpmbanisha kisha wao wanafanya biashara kwa habari na skendo zenu! hiyo hailipi mshikaji futa hiyo kesi wachana naye mtakie maisha mema na umsaidie pale inapobidi huo ndo uanaume nakushauri ndugu yangu hapo utakuwa umewini lakini si mambo ya kkupelekana polisi!

    mh its disgusting to me!

    mdau
    USA
     
    fast    

    #12 Author: fresh (5 February 2009 11:46)

    nakuunga mkono ANGALIA hapo juu, mambo ya mapenzi wala usishangae kusikia mtu kajirusha kwenye gorofa/kavunja kioo/kamuuma meno mtu..kifupi kugombanagombana.kweli kama huyo Kanumba angekuwa na busara kama mtu mwenye busara zaidi na jamii inasikilizia hii habari angefanya kila liwezekanalo kumsaidia.kwani demu alipokuwa anakubali kupewa ile habari ya baba na mama mbona kanumba hakukimbilia polisi kusema demu ananivunja utamu kuwa na wengine.ninamsahauri kama kweli ni mwanaume,kwani kioo cha gari nini...hakifiki hata laki 2 ya kitanzania.yeye asingeweka beef na mamsapu wake huyo wa zamani(kama alivyosema Pro.j enzi zilee).futa kesi na msaidie pale inapobidi.kwani mashindano yako na yeye ni kama kupoteza muda tu.

    inafedhehesha kwa jamii
    mdau
    JAPAN
     
    fast    

    #13 Author: haya (5 February 2009 11:54)

    please tembelea: www.zeutamu.com
     
    fast    

    #14 Author: walewale orijino (5 February 2009 17:13)

    wasanii wa bongo kazi mnayo watu tunawaza jinsi ya kufanya kazi na kutafuta pesa wenzetu mnawaza kupigana,kuvunjiana vioo,kupeana mapenzi ya uongo....kweli tunapishana kimawazo japo kimaumbile wote ni binadamu....
     
    fast    

    #15 Author: BLACKMANNEN (5 February 2009 18:53)

    Watu wengi mnarukia kumsakama Wema kwa kumwona ni mkosaji katika kila alitendalo. Lakini bila kufikiria kitu kinachofanya yeye aonekane sana katika magazeti ya udaku. Kuna mambo mengi. Lakini mimi nitazungumzia moja tu.

    Matatizo anayoyapata Wema sasa hivi yamesababishwa na Wazazi wake ambao haelewani nao kwa sababu moja kuu.

    Wazazi wa Wema ni watu wanaopenda kuendesha maisha ya mtu ili awe kama wanavyotaka wao. Wazazi wa Wema wanajiona kuwa wao ni waadilifu sana katika matendo na malezi kuliko wazazi wengine. Wema hana kauli kuhusu kujiamuliwa lolote katika maisha yake. Yupo jela ya nyumbani.

    Kitendo cha Wema kuamua kutowasikiliza wazazi na kuamua kuanza kujiamulia kuwa yeye kama Wema katika maisha yake. Kimewaudhi sana wazazi hao na ndiyo maana wanamtumia Kanumba ili kumwadhibu kwa njia za kisaikolojia.

    Lakini Kanumba aelewe kuwa, kitendo anachomfanyia Wema kama binadamu mwenzie katika kumlipizia kwa yale aliyomfanyia, yatamrudia yeye Kanumba. Mwenyezi Mungu hamtupi kiumbe wake. Kama kweli aliona Wema kamvunjia kioo cha gari lake kwa sababu wanayoijua wao wawili, kwanini imechukua siku kadhaa kupita ndipo achukuliwe na Polisi?

    Kanumba, Shinikizo unalolipata kutoka kwa wazazi wa Wema kumwadhibu mpenzi wako sio kitu cha kistaarabu hata kidogo. Jaribu kusikia walichokushauri baadhi ya watu hapo juu katika maoni yao.

    It's Great To Be Black=Blackmannen
     
    fast    

    #16 Author: kishanshuda (6 February 2009 00:07)

    HIVI WEMA TOKEA UMEANZA KU..... UMEFIKISHA WANAUME WANGAPI? NA UMEDANGANYA WANAUME WANGAPI? MIE NAONA KANUMBA KAKUKOMESHA SANA TU UACHE KUWADANGANYA WATOTO WA WANAUME WENZIO.ULIPOVUNJA KIOO ULITEGEMEA UMEMKOMESHA KUMBE UMEKOMESHWA MWENYEWE HADI UMELALA LUPANGO DUH MTOTO MPANA WEWE SURA IMESHAKUKOMAA KWA SABABU YA KUPENDA KU..... LOL SASA HIVI NAONA UTASHIKA ADABU KIDOGO.
     
    fast    

    #17 Author: eric (10 February 2009 08:35)

    sidhani kama kanun=mba ana kosa ila Wema hakutumia busara kuvunja kioo cha mwenzake wazamani naweza sema kuwa bado anampenda ila anazuga tu ,,,,,, wink pole Wema kwa yaliyokukuta ndio ulimwengu huo mama
     
    fast    

    Add comments

    Name:
    E-mail:

    Code:
    Include security image CAPCHA.
    to renew the code
    Enter Code:

     

    Kura Yako / Poll

    Habari Katika Picha


    Gazeti la Uwazi


    Nani Yupo / Alikuwepo


    Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

     hit counter

    counters

    2008 © globalpublisherstz.com