Wiki iliyopita, timu ya Promosheni ya Bahati Nasibu ya jishindie Pajero, inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers, ilikuwa Mkoani Arusha na Manyara kuhamasisha wasomaji wake. Picha zifuatazo, zinaonesha jinsi wasomaji wa magazeti ya Global Publishers katika mikoa hiyo walivyochangamkia Promosheni hiyo ambayo droo yake ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Alhamis ijayo, April 9 jijini Dar es salaam.
Wakazi wa Arusha maeneo ya Mbauda Sokoni, wakiwania kuponi za Jishindie Pajero, Jumamosi wiki iliyopita.
Mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, maeneo ya Ngaramtoni, Arusha, (aliyeinua gazeti na kitabu katikati) akiwahamasisha wasomaji wengine wa eneo hilo kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero, kwa kununua magazeti ya kampuni hiyo.
Wananchi wa Arusha mjini eneo la Soko Kuu, wakiwania kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero, kwa kununua magazeti na vitabu mbalimbali vya kampuni ya Global Publishers.
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wa Monduli, mkoani Arusha, wakiwa wamejipanga kupata magazeti na machapisho mbalimbali ya Global Publishers.
Mkoani Manyara pia wasomaji wa magazeti maarufu ya Global Publishers, walishiriki kwa hamu kubwa katika kununua magazeti ya kampuni hiyo, ili kushiriki katika Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero. Picha: Musa Mateja /GPL.
Kamera yetu pia iliweza kunasa shughuli mbalimbali za wakazi wa Monduli, ikiwa ni pamoja na kinamama waliokuwa wakitumia usafiri wa ‘punda’ katika kubebea bidhaa zao kuelekea katika masoko mbalimbali.
Wakazi wa Monduli, wakiwa sokoni katika harakati za kila siku za kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kama walivyonaswa na kamera yetu. Picha: Musa Mateja /GPL.
Msanii wa muziki wa Injili nchini, Kabula J. George, anatarajiwa kuirekodi albamu yake ya ‘Ushindi’ ambayo nyimbo zake zimeanza kuwashika watu wengi wanaozisikiliza kupitia vituo vya radio nchini, kwenye video...
Na Elias Ally, Iringa DUNIANI kuna magonjwa mbalimbali ambapo kuna mengine hayajawahi hata kuonekana na mengine kutokea kwake kwaweza kukawa ni mara ya kwanza....
WAFANYAKAZI wenzake na marehemu katika Hoteli ya Mwanza, ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, wameibua mambo mapya kwa kutoboa siri za Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali, kwa kueleza uhusiano wake na mmoja wa Marehemu Vicky ulivyokuwa kabla ya ajali...
KUFUATIA ajali nyingine ya treni iliyotokea Jumapili mwishoni mwa Wiki iliyopita katikati ya Stesheni ya Gulwe na Msagali wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo watu 7 walikufa papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa, wahanga waliohojiwa na Uwazi wameilaumu Serikali kwa ajali za mara kwa mara zinazolikabili taifa na kusababisha maisha ya maelfu ya raia wema kupotea...
Wiki iliyopita nilianza kuongea juu ya Adui wa CCM yupo ndani ya CCM yenyewe na kama adui huyo hayuko ndani basi CCM haina sababu yoyote ya kuhofia maadui wa nje, maana hawatakizulu Chama hicho kikongwe nchini. Niliongea mengi na mwisho nikashauri kama Mtanzania, kwamba ni wakati mzuri wa Chama Cha Mapinduzi kuingiza damu changa ndani ya chama chao, kuwekeza katika siku za usoni badala ya kuendelea kubakiza madaraka mikononi mwa wazazi wetu ambao wamenza kuchoka, huu ni wakati wa wao kupumzika. Leo naendelea…
Mke wa mtu anapanga mashambulizi ya kimya kimya ili kumuua mumewe aweze kuolewa na mwanaume tajiri mwenye asili ya kiarabu na kwenda kuishi Uarabuni, wametumwa wanaume watatu waliopanda ndani ya teksi maeneo ya Mlandizi na kumuwekea bastola kichwani tayari kumuua. Jambo moja analotamka mumewe anamuomba Shakila amwambie sababu au kosa gani linalostahili kifo? Mkewe anamjibu kuwa hajamkosea jambo lolote isipokuwa ameamua kufanya hivyo ili akaolewe na mwanaume tajiri mwenye asili ya kiarabu, mumewe anamruhusu akaolewe na kumtaka asimuue kwani watoto wake watabaki yatima na hakuna wa kuwalea.Je, nini kitaendelea? Fuatilia mkasa huu wa kuhuzunisha utajifunza jambo...
Msichana mrembo Priscilla ameingia mikononi mwa wanyonya damu, wanaomlazimisha kufanya kazi haramu ya damu. Halikuwa jambo rahisi kwa Priscilla kukubaliana na watu hao katili. Maishani mwake hakutaka kuua kiumbe cha Mungu, anapinga na kuomba arudishwe nyumbani Tanzania lakini Jimmy anamwambia lazima wamnyonye damu kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi akisisitiza kila anayeingia ndani ya jumba hilo lazima akubaliane na matakwa yao vinginevyo mauti humfika.
Moyo ulimuuma na kuanza kulia, anaingizwa chumba maalumu kwa ajili ya kunyonywa damu kisha anaambiwa hapo ndipo uhai wake utakapotoweka. Katika chumba hicho chenye chupa nyingi za damu za makundi tofauti, Priscilla alishuhudia mwanaume mweusi akinyonywa damu mshtuko mkubwa ulimpata na kupoteza fahamu.
Katika hali ya kutisha, Priscilla anaanza kunyonywa damu taratibu, sindano ya kwanza ilipoingia mwilini alihisi kizunguzungu, baadaye akahamishwa chumba kingine ambako alivuliwa nguo zote na kulazwa juu ya kitanda, Wairimo mwanamke mweusi akakabidhiwa afanye kazi yake, baadaye Jimmy anaingia na dumu la lita tano Priscilla akahisi kifo kilikuwa mbele yake.
Huruma ilimuingia sana Wairimo na kuanza kumtetea Priscilla, baadaye anamuomba Jimmy atoke ili waweze kuongea naye, walibaki wawili katika chumba chenye chupa nyingi, Wairimo anapomweleza siri na mafanikio ya kazi ya damu, Priscilla anajikuta akiridhia na kuingiwa na uchu wa kuwa bilionea.
Muda mfupi anaanza kuzoea maisha magumu ya unyonyaji damu aliporidhia kazi ya damu, wanaondoka Humberg nchini Ujerumani na kuingia jijini Dar es Salaam, kazi kubwa mbele yao ikiwa kunyonya watu damu na kuisafirisha hadi nchini Ujerumani nyumbani kwa Jimmy.
Ndani ya jiji la Dar es Salaam, wanyonya damu hao wanashukia Hoteli ya Sweet Dream iliyopo Masaki, wanafanya mazungumzo kwa siri juu ya kuanza kazi yao, jinsi gani wangeweza kufanikisha zoezi hilo bila kutiwa mikononi mwa Vyombo vya Sheria.
Usiku huo, Priscilla hakutaka kulala anamwambia Wairimo anatamani kuanza kazi hiyo mapema, wanakubaliana na kumuacha Miloslov chumbani na kuvaa nguo za kimahaba zinazoshawishi wanaume. Kila mmoja anaridhika kuwa amependeza ndipo anapochukua teksi iliyowapeleka hadi Manzese Tip Top katika baa moja inayopiga muziki siku za mwisho wa wiki. Je, atafanikiwa kunyonya damu au atatiwa mikononi mwa Polisi? SONGA NAYO...
Kitimtim cha aina yake kilihibuka kati ya polisi mmoja wa Usalama barabarani (Trafiki) na dereva mmoja wa daladala ifanyayo safari zake kati Mwenge na Kariakoo ambaye alitaka kumgonga polisi huyo wakati akiongoza magari katika taa zilizopo Bamaga jijini Dar es Salaam. Kitimtim hicho kilianza baada ya dereva kupita katika taa za kuongozea magari wakati taa nyekundu zikiwa zinawaka na aliposimamishwa na Trafiki huyo, alikataa kusimamisha gari lake ndipo askari huyo wa usalama barabarani alipoamua kupanda gari ndogo na kuifukuzia Daladala hiyo ambayo ilikwama kutokana na foleni za barabarani.
Askari huyo wa usalama barabarani akimpeleka dereva huyo katika kituo cha Polisi ili sheria ikafuate mkondo wake.
Wakionekana kwa nyuma dereva huyo akiwa amepigwa Tanganyika Jeck akielekea Polisi.
Kijana huyu alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam akiwa amejiinamia na akionekana kuwa na mawazo mengi.Hata hivyo haikueleweka mara moja masaibu yaliyomfika.
NANI KASEMA VIJANA BONGO WANAJIBWETEKA? Mshkaji huyu ambaye anafanya biashara ya kuuza mashuka akikata mitaa kusaka wateja maeneo ya Kinondoni.
MTAJI WA MASIKINI NGUVU ZAKE MWENYEWE! Dili kusaka Mahela! Ndiyo msemo ambao vijana wengi wanautumia ndani ya Bongo.Pichani msela akiwa amejitwisha matenga kibao ambapo haikueleweka kama anayauza au alikuwa akiyapeleka sehemu kwa ajili ya kufanyia biashara.
Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili. Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa, mawili ni ya kusababisha vifo na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote. Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu ambapo kigogo huyo anapeta nje kwa dhamana ya shilingi Milioni moja chini ya mdhamini mmoja.
Chenge akifikishwa mahakamani leo chini ya ulinzi mkali.
Kamishna wa usalama barabarani Mkoa maalum wa kipolisi wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam Peter Kivuyo aliongoza msafara wa kumfikisha Chenge Mahakamani hapo.
Mke wa Chenge akiingia Mahakamani hapo akiwa na wapambe wake.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na walimu wa shule za Msingi za Mbarali baada ya kutembelea Skimu ya Southern Highlands Estate zamani ikiitwa Mabarari akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya March 28, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph, (katikati) akiwajibika jukwaani leo alfajiri ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam, kulia waliokaa ni waimbaji wa kundi hilo na kushoto ni wanenguaji wa kiume wa kundi hilo. PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL.
Gari la Askari Magereza likiwa limepinduka katika maeneo ya Tabata Bima leo asubuhi, lilikuwa likitokea Gereza la Segerea, likiongoza basi lililokua na mahabusu kwenda mahakama mbali mbali. Picha: Makogoro oging'.