Na Shufaa Lyimo Katika hali inayofananishwa kwamba ni sawa na biashara za kimachinga, Kocha Mkuu wa Timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, Mbrazil Neider dos Santos amesema sasa ana kazi moja ya kuzitembeza CD za wachezaji wake nchi mbalimbali kwa lengo la kuwatafutia soko la kucheza soka la kulipwa...
Eunice Macha na Chausiku Omar B AADA ya Timu ya Simba kupigishwa kwata la ‘kufa mtu’ na Kocha wao Mkuu Mzambia Patrick Phiri, Jumatano wiki hii itapimana nguvu na Miembeni ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam....
Mtoto Adrian anatoka katika familia ya masikini kupindukia, yeye na dada yake Adventina wanalelewa na mama yao, hawakuwahi kumwona baba katika maisha yao na hawajui historia yake kwani mama yao hajawasimulia. Adventina ni mwanafunzi wa darasa la kwanza kwenye shule iliyoko umbali wa kilometa kumi na tano kutoka nyumbani kwao. Adrian hasomi lakini anatarajiwa kuingia darasa la kwanza mwaka ujao. Familia hii inaishi kwa msaada wa Kanisa Katoliki, mara kwa mara wanapokuwa na shida huenda Parokiani na kumwomba Padri awasaidie.
Mara ya mwisho walipokwenda wanakutana na Padri ambaye baada ya kuwasikiliza shida yao anaanza kumuuliza Adrian maswali ya hesabu na kushangazwa na uwezo ambao mtoto huyo alikuwa nao ingawa bado hata darasa la kwanza hajaanza! Padri anaamua kumsaidia Adrian kusoma kwani amegundua kilichomo ndani yake, hakuwa mtoto wa kawaida! Msaada wake unakuwa ni kumpeleka kwenye shule ya seminari iitwayo Kiparato ambako anaanza darasa la kwanza, huko anakutana na watoto wengi wa matajiri kwani shule hiyo inaheshimika na watu wenye uwezo pamoja na viongozi hupeleka watoto wao hapo kupata elimu bora.
Miongoni mwa watoto aliokutana nao kwenye shule hiyo, tena kwenye darasa lake ni Edward, huyu ni mtoto wa mfanyabiashara aitwaye Lonjino ambaye kwake fedha ni kila kitu! Mtoto huyu amelelewa katika mazingira ya fedha, mazungumzo nyumbani kwao kila siku yanahusu fedha na wazazi wake kumwambia kabisa akikua ni lazima atafute utajiri na mbegu hiyo imepandikizwa ndani ya kichwa cha Edward. Mtoto mwingine ambaye Adrian amekutana naye kwenye darasa lake ni Paul Kitumbi, pia mtoto wa tajiri, naye fedha maishani mwake ni kila kitu, anafahamu amekuja shuleni kusoma ili akimaliza Chuo Kikuu arejee nyumbani kusimamia shughuli za baba yake kwani yeye pekee ndiye mtoto wa kiume kwenye familia hiyo! Adrian amezungukwa na matajiri, anajisikia mnyonge mbele ya wenzake na hana rafiki hata mmoja, ni aidha anatengwa au anajitenga mwenyewe. Hii inamfanya kila siku awakumbuke mama na dada yake Adventina aliowaacha kwenye dhiki kubwa, anaapa kusoma mpaka afanikiwe na kuikomboa familia yake. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
Bendi ya Africa Stars 'Twanga Pepeta International’ usiku wa kuamkia leo, imewaomba radhi wapenzi wake wa Bonanza la pale Leaders Club na usiku pale TCC Club Chango'mbe kuwa usiku huo ilikuwa ikisafiri kuelekea mkoani Kilimanjaro kuburudisha kwenye mbio za Marathon. Pichani mwanamuziki wa bendi hiyo Luiza Nyoni, akiongoza wanenguaji katika makamuzi ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, jijini Dar. PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
Ilikuwa mchana wa jua la 'utosini' wakati mpiga picha wetu alipowafotoa jamaa hawa wakiwa 'zero distance' mitaa ya Aggrey katikati ya eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam....ni mambo ya malavi Davi hayo!!. Picha:Issa Mnally