arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 02.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Niligeuka mwanamke, nik ...
» Maofisa habari waonywa ...
» Jamani nilianzia huku!
» Walimu watofautiana kwe ...
» Ze Comedy waua!
» RAIS WA NIGERIA ATAKIWA ...
» Nampenda mume wa shoga ...

 

KADA CCM ABAMBWA NA KADI KIBAO ZA CHADEMA OFISINI

uwazi  
KADA CCM ABAMBWA NA KADI KIBAO ZA CHADEMA OFISINI
Na Musa mateja

MWENYEKITI wa Serikali za Mitaa (CCM), Mbezi Juu jijini Dar es Salaam, Osward Mwasuka, hivi karibuni amewafedhehesha wanachama wenzake wa CCM baada ya kukutwa na kadi zaidi ya mia moja za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ofisini kwake...
    (2 March 2009)
Views: 578 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Faili laibwa Mahakamani

uwazi  
Faili laibwa Mahakamani
Na Mwandishi Wetu

UMEKUWA na utata mkubwa ndani ya Mahakama Kuu kufuatia kupotea kwa faili la kesi namba 124/2003 iliyofunguliwa na Bw. Omary Shabani, mkazi wa Kariakoo jijini Dar es salaam kupinga ugawaji wa mirathi namba 237/97 uliofanywa na hakimu mfawidhi mahakama ya mwanzo, Kariakoo...
    (2 March 2009)
Views: 658 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

TUKO KWENYE BASI, DEREVA AMEBONYEZA AUTOPILOT?

Pasua Jipu  
NAMSHUKURU Mungu kwa yote anayonitendea na jinsi anavyonisimamia kupita katika mapito yangu ya kila siku. Hili aliliahidi mwenyewe tangu mwanzo katika kitabu chake cha Zaburi 23 …katika bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya maana yeye huniuisha nafsi yangu na kuniongoza”...
    (2 March 2009)
Views: 305 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

THE BLOOD DEAL - 35

hadithi za Shigongo  
Priscilla ni msichana mrembo na tajiri kupita kiasi, mali zake zinawashangaza wengi na kamwe hakuthubutu kutoa siri ya mafanikio yake, maishani mwake hakuonekana na mwanaume zaidi ya wafanyakazi wake, hilo pia liliwashangaza watu wengi na kushindwa kuelewa kwanini hakuwa na mwanaume wa kumfariji baada ya kazi nzito za kutwa, alionekana msiri asiyetaka watu wafahamu maisha yake.

Siku zote alionekana akiendesha magari ya kifahari na kuyabadili, wengi walidhani huenda utajiri wake ulitokana na mwanaume tajiri mume wa mtu hivyo kukutana kwa siri, pamoja na hayo ana siri nzito inayoendelea kudumu kichwani mwake.

Msichana huyo pamoja kuwa na uzuri na utajiri wa kumfanya aogopwe na wanaume wengi, bado angali alikuwa bikra, wanaume wengi walimuogopa sababu ya utajiri wake.

Magari ya kifahari aina ya Ferrari, H3 Hummer, Mercedes Benz, Land Cruiser, BMW, Range Rover Vogue ndiyo magari aliyokuwa akitembelea msichana huyu. Lakini siku chache akiwa kwenye mataa ndani ya gari lake aina ya Ferrari kibanda wazi anajikuta akiingia mikononi mwa mlemavu Muddy ambaye sasa ameachana na kazi ya kuua wanawake na kuwakata nyeti zao na kuamua kuwa ombaomba baada ya kuishiwa, mlemavu huyo mnyonge mwenye umbile dogo ni katili kuliko anavyoonekana kwa macho hilo hakulijua Priscilla.

Wanaungana kuwa wapenzi na maisha ya Muddy yanabadilika sana, anahamia nyumbani kwa Priscilla, baadaye wanaondoka kwenda London nchini Uingereza kwa ajili ya kula raha za dunia. Wakiwa nchini humo ndipo jambo moja linapomshtua Muddy alipogundua Priscilla ametumiwa ujumbe kupitia barua pepe kuwa zinahitajika damu lita elfu tano za kundi O elfu tatu, AB elfu moja mia tano na B lita mia tano, akisisitizwa afanye haraka pesa zake zipo tayari. Muddy anapomaliza kusoma ujumbe huo jasho linamtoka na kuanza kusumbuliwa na hisia za kuuawa akilini mwake akijiuliza kwanini siku zote mpenzi wake alikuwa akimlazimisha kula mboga za majani?

Je, Priscilla ni nani na kwanini ameandikiwa ujumbe huo? Kazi yake inayomfanya awe tajiri ni nini? Fuatilia historia ya Priscilla...
    (2 March 2009)
Views: 1009 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

NILIMUUA MUME WANGU NIOLEWE NA TAJIRI - 12

Mikasa ya kusisimua  
Ndani ya ndoa kuna siri nyingi ambazo si rahisi kuzibaini kwa macho wala maneno, Shakila ni mwanamke katili licha ya kuubwa na sura nzuri inayowavutia wanaume wengi, ndani ya ndoa yake anaishi kwa muda wa miaka mitatu bila mtoto ndipo anapowatesa watoto aliowakuta katika familia akiwapiga kila leo. Kitu kinachomkosesha raha ni jinsi gani angemuua mumewe ili kuolewa na tajiri. Siku moja anamualika mpenzi wake ambaye ni tajiri nyumbani anapoishi na mumewe na ndipo anafumaniwa na mama yake mzazi, mshenga na mumewe, hata hivyo anadiriki kujitetea kuwa hajaolewa na wazazi wake wanamlazimisha kuolewa na mwanaume asiyempenda. Hapo ndipo mumewe anapoandika talaka na kuiweka mezani kwa ajili ya kuachana na mkewe ili akaolewe na tajiri, mwarabu. Je, nini kitaendelea? Fuatilia....


    (2 March 2009)
Views: 1135 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

KESI YA MARANDA YASHIKA KASI

photos  
KESI YA MARANDA  YASHIKA KASI

Bw. Salum Kisai ambaye ni shahidi wa sita katika kesi ya ufisadi wa zaidi ya Sh.Bilioni moja kutoka kwenye akaunti ya malipo ya nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), inayomkabili aliyekuwa Mweka Hazina wa CCM, Mkoa wa Kigoma, Rajabu Shaban Maranda na binamu yake Farijala Husein, leo amekiri kuwa alichukua maelezo ya onyo kutoka kwa Bw.Maranda akiwa anaumwa.

Hatahivyo, Kisai aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Cypriana Willia, kwamba pamoja na kuchukua maelezo hayo lakini alimpa haki zote za msingi Maranda ikiwa ni pamoja na muda wa kupumzika kabla ya kuanza kutoa maelezo yake.

Kesi hiyo itaendelea tena kesho ambapo upande wa mashitaka unatarajia kuleta shahidi wa mwisho katika kesi hiyo. Pia upande wa utetezi unatarajia kuleta shahidi wake ili kuthibitisha kuwa ni kweli Maranda aliandika maelezo ya onyo akiwa hoi.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL
    (2 March 2009)
Views: 333 | Maoni (2) |

 

MWANADADA AWANIA KITI CHA MINTANGA

photos  
Mwanadada Joan Melkion Minja, leo ametangaza kugombea kiti cha Urais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini, ‘BFT’ kilichokuwa kikikaliwa na Alhaji Shaaban Mintanga, anayeozea Mahabusu akidaiwa kubambwa na madawa ya kulevya.

MWANADADA AWANIA KITI CHA MINTANGA
Bi. Joan (kushoto) akimwaga sera zake kwa Waandishi wa Habari katika Ukumbi Idara ya Habari ‘MAELEZO’ leo mchana, ambazo amedai atazitekeleza baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 14, mwaka huu. Kushoto ni mwanamasumbwi wa muda mrefu Willy Isangula.

NGOJA TUJIACHIE KWA RAHA ZETU.
MWANADADA AWANIA KITI CHA MINTANGA
Mama huyu na watoto wake walinaswa na kamera yetu leo mchana wakiwa wamejiachia kwa raha zao kando ya barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL.
    (2 March 2009)
Views: 362 | Maoni (1) |

 

DUH! DEREVA ‘MDEBWEDO’ AVAMIA KITUO CHA MABASI

photos  
DUH! DEREVA ‘MDEBWEDO’ AVAMIA KITUO CHA MABASI
Jamaa wakishangaa gari ndogo aina ya Starlet, T.132 AWQ, lililovaa kituo kidogo cha abiria na kumjeruhi vibaya mwanafinzi aliyekuwa kituoni hapo akisubiri usafiri maeneo ya Victoria Barabara ya Ally Hassan Mwinyi jijini Dar.

DUH! DEREVA ‘MDEBWEDO’ AVAMIA KITUO CHA MABASI
Mashuhuda wakiangalia jinsi gari hiyo ilivyobeba kituo hicho

DUH! DEREVA ‘MDEBWEDO’ AVAMIA KITUO CHA MABASI
Inaonekana ikiwa imezama kabisa ndani ya kituo hicho sehemu ya mbele.
Picha na Paul Sifael na Musa Mateja/GPL.
    (2 March 2009)
Views: 289 | Maoni (0) |

 

AKUDO YAJA NA MTINDO WA ROBBOT

photos  
AKUDO YAJA NA MTINDO WA ROBBOT
Wadau wa burudani wakiserebuka kwa mtindo mpya wa bendi ya Akudo Impact uitwao ‘Robbot’ ambao ulitambulishwa katika Bonanza lililofanyika Ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.(pichani) mashabiki waliofurika kwenye bonanza hilo wakicheza ‘kirobotiroboti’.

MABITOZI WA KIKONGO KWA MISIFA!
AKUDO YAJA NA MTINDO WA ROBBOT
Rais wa bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ Christian Bella akimwonesha mwandishi wetu mkufu wake wa madini ya shaba.

NGOJA NISEREBUKE KIBOSIBOSI
AKUDO YAJA NA MTINDO WA ROBBOT
Mwanamuziki wa Bendi ya TOT Respect, Rashid Mwezingo akijimwaya kibosibosi na tai yake shingoni katika onesho la bendi hiyo lililofanyika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL.
    (2 March 2009)
Views: 560 | Maoni (2) |

 

DUH!

ijumaa wikienda  
DUH!
Na Mwandishi Wetu

Warembo wenye majina makubwa nchini, Miss Ilala namba tatu mwaka 2005, Jacqueline Patrick, Miss Tanzania namba tano 2006, Irene Uwoya na Miss Tanzania 2nd runner up 2007, Queen David wameingia kwenye skendo ya kulala na mwanaume mmoja....

    (2 March 2009)
Views: 2693 | Maoni (21) | Soma Zaidi

 

Liyumba afanyiwa kitu mbaya Gerezani

ijumaa wikienda  
Liyumba afanyiwa kitu mbaya Gerezani
Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Bosi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mr. Amatus Liyumba ambaye anakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi ya Serikali, ameanza kuonja jiwe lenye joto baada ya kudaiwa ‘kusimangwa’ na baadhi ya mahabusu wa gereza la Keko ‘anakoishi’ kwa sasa....
    (2 March 2009)
Views: 1877 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Shenazi hajafa?

ijumaa wikienda  
Shenazi hajafa?
Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa muigizaji na mnenguaji ‘alwatan’ nchini, Marehemu Shenazi Salum anawapa wakati mgumu baadhi ya watu wake wa karibu kwa kuwatokea mara kwa mara, hivyo kuzusha imani kuwa bado yu hai...
    (2 March 2009)
Views: 1496 | Maoni (9) | Soma Zaidi

 

Niliishi kuzimu miaka ishirini Part-II-19

Mikasa ya kusisimua  
Zubeda Ruvanga, mwanamke mwenye umri wa miaka 38, anasimulia mateso aliyokumbana nayo tangu akiwa mtoto. Wachawi walianza kumpa tabu za maisha tangu akiwa darasa la tatu kwenye Shule ya Msingi Mwandiga Kigoma. Wiki iliyopita aliishia pale Mfalme Dajani alipofurahi kusikia habari kuwa Zubeda ameridhia kuwa mchawi, baada ya kushawishiwa na Sikuzania. Endelea kusoma…
    (2 March 2009)
Views: 705 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Wivu ni chachandu ya mapenzi-3

Mahaba  
Mungu aliyemfanya Adam kuwa binadamu wa kwanza kisha akamtengeneza Hawa kuwa wa pili wake, ndiye huyo huyo anayewezesha mimi na wewe tukutane katika safu hii ya XXL tunayoipenda. Tumshukuru kwa kila jema analolitenda kwetu...
    (2 March 2009)
Views: 430 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

SILENT FOREVER - 9

hadithi za Shigongo  
James na Rachel wanaamua kuhamia jijini Dar es Salaam ambako pia kuna tawi la ofisi yao ya uwakili, huko ndiko wanamfahamu mwanamke mwendawazimu aitwaye Hilda na mtoto wake Bahati, haukupita muda mrefu sana baada ya hapo wakasikia mwanamke huyo ameuawa kwa kukatwa na panga na polisi walikuwa wakimtafuta muuaji kwa udi na uvumba.

Kwa kumbukumbu zake James usiku ambao Hilda aliuawa, yeye na mke wake walikuwa wakitoka hoteli ya New Afrika kwenye sherehe, walipofika kwenye daraja la salenda waliona gari limeegeshwa kando ya barabara, wakafikiri ni mtu amepatwa na tatizo, bila woga wakasimamisha gari lao na James kushuka kuanza kutembea kulifuata gari hilo, mbele alimwona mtu akivua kitu kama koti jeusi na kulitupa darajani na alipomsalimia hakuitikia, akahisi kuna kitu.

Alichofanya James ni kwenda kwenye daraja hilo siku iliyofuata na kukuta kuna koti jeusi lililolowa damu likiwa limetupwa ndipo akaamua kwenda ofisini kwake ambako alipiga simu polisi na kuwapa taarifa juu ya alichokishuhudia, pamoja wakaenda tena mpaka darajani na kulikuta koti pamoja na panga, polisi wakashukuru kwamba hatimaye wangeweza kumpata muuaji kwa kupima alama za vidole na DNA, walikuwa na uhakika kabisa mtu aliyetupa koti hilo ndiye aliyewakata Hilda na mwanae mapanga na kufanikiwa kumuua Hilda.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (2 March 2009)
Views: 978 | Maoni (10) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com