arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 05.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» ‘MAREHEMU’ AFUFUKA
» `Nyayo ya damu- 2
» Historia huyahukumu map ...
» KUTAFUTA MAISHA KUMENIF ...
» (SIMULIZI ZA CHUMBANI) ...
» Ijue dawa ya simanzi ya ...
» GLOBAL PUBLISHERS YAANZ ...

 

Bellah: MISS RUVUMA: MIMI SIYO CHANGUDOA

ijumaa  
Bellah: MISS RUVUMA: MIMI SIYO CHANGUDOA

HIVI karibuni amekuja kwa kasi sana katika anga za ma-Miss ambao wanatamkika.
Anaitwa Isabellah Mpanda, amewahi kuwa Miss Ruvuma mwaka 2005. Pia alifanikiwa kushiriki Miss Tanzania na kuingia hatua ya Kumi Bora au Top Ten...
    (5 March 2009)
Views: 989 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

MTIKISIKO

ijumaa  
MTIKISIKO
Mariam Mndeme na Amina Salim

MENEJA wa mradi mmoja mkubwa nchini, anayejulikana kwa jina la Patrick Lutu, mkazi wa Kimara jijini Dar, hivi karibuni alijikuta ‘akikosa pumzi’ baada ya kumfumania mkewe mdogo anayejulikana kwa jina la Maria Zakayo...
    (5 March 2009)
Views: 1528 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

WEMA: Najuta kumfahamu Kanumba

ijumaa  
WEMA: Najuta kumfahamu Kanumba
Musa Mateja na Edna Katabalo

MTIKISIKO uliomkumba Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu baada ya kuburuzwa kwenye Mahakama ya Kinondoni juzi kisha kuswekwa mahabusu katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam umemfanya mnyange huyo ‘amkinai’ aliyekuwa mpenzi wake, Steven Charles Kanumba...
    (5 March 2009)
Views: 7540 | Maoni (42) | Soma Zaidi

 

Kimada aitikisa ndoa ya Richard!

ijumaa  
Kimada aitikisa ndoa ya Richard!
Na Waandishi Wetu

NDOA ya Big Brother Africa II (BBA II) Richard Bezuidenhout inadaiwa ipo katika mtikisiko baada ya kuwepo kwa uvumi kwamba staa huyo ana uhusiano usiofaa na mwanamitindo Belina Mgeni...
    (5 March 2009)
Views: 1879 | Maoni (9) | Soma Zaidi

 

House girl! ...Ni kweli hupindua mama wenye nyumba?

Mahaba  
House girl!  ...Ni kweli hupindua mama wenye nyumba?

Mungu atusaidie sana! Lazima tuombe msaada wake maana ni kweli hatuwezi kufanya kitu chochote bila ya msaada wa yeye aliyetuumba kwa mfano wake...
    (5 March 2009)
Views: 833 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

SILENT FOREVER (10)

hadithi za Shigongo  
Mwanamke mwendawazimu Hilda na mwanae Bahati, ambao wanaishi mtaani maeneo ya Posta, wanavamiwa usiku na mtu asiyejulikana ambaye bila huruma anawakatakata kwa mapanga na kuondoka alipoamini wamekufa! Miili yao inagundulika alfajiri na kukimbizwa hospitali ambako inathibitika kwamba Hilda amekwishakufa lakini mwanae bado anahema na juhudi za kuokoa maisha yake zinafanyika mpaka anapona.

Baada ya hapo mtoto huyo alichukuliwa na kituo cha kulea watoto Yatima cha Msimbazi ambako aliishi mpaka kutimiza miaka kumi na nane akiamini hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao, hakuwa na kumbukumbu yoyote, akiamini sista Florentina ndiye alikuwa mama yake mzazi.

Sista Florentina anamwita siku moja na kumwambia tayari ametimiza umri wa kuishi kituoni, anaweka kila kitu kuhusu maisha ya Bahati wazi, anaufahamu ukweli ambao hakuwahi kuujua. Roho inamuuma, Bahati analia lakini hilo halibadilishi uamuzi wa sista.

Siku iliyofuata anaondoka na mizigo yake hadi maeneo ya Posta ambako anaanza maisha ya kuishi kwenye boti, akishirikiana na vijana wengine aliowakuta huko, kazi yao ikiwa ni kuuza dawa za kulevya na kuiba vifaa vya magari ambavyo walivipeleka kwa kiongozi wao Don, Bahati akawa mhalifu, akasahau kila kitu kuhusu maisha ya kituoni na Sista Florentina.

Kwa kumbukumbu zake James usiku ambao Hilda aliuawa, yeye na mke wake walikuwa wakitoka hoteli ya New Afrika kwenye sherehe, walipofika kwenye daraja la Salenda waliona gari limeegeshwa kando ya barabara, wakafikiri ni mtu amepatwa na tatizo, bila woga wakasimamisha gari lao na James kushuka kuanza kutembea kulifuata gari hilo, mbele alimwona mtu akivua kitu kama koti jeusi na kulitupa darajani na alipomsalimia hakuitikia, akahisi kuna kitu.

Alichofanya James ni kwenda kwenye daraja hilo siku iliyofuata na kukuta kuna koti jeusi lililolowa damu likiwa limetupwa ndipo akaamua kwenda ofisini kwake ambako alipiga simu polisi na kuwapa taarifa juu ya alichokishuhudia, pamoja wakaenda tena mpaka darajani na kulikuta koti pamoja na panga, polisi wakashukuru kwamba hatimaye wangeweza kumpata muuaji kwa kupima alama za vidole na DNA, walikuwa na uhakika kabisa mtu aliyetupa koti hilo ndiye aliyewakata Hilda na mwanae mapanga na kufanikiwa kumuua Hilda.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (5 March 2009)
Views: 859 | Maoni (13) | Soma Zaidi

 

Boban: Maximo mbinafsi, mnafiki na mwongo

champion ijumaa  
Boban: Maximo mbinafsi, mnafiki na mwongo
Na Shufaa Lyimo

KIUNGO mshambuliaji wa Timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ ametoboa siri nzito ya kutoelewana kwake na Kocha wa Stars Mbrazil, Marcio Maximo kuwa ni; “Ubinafsi, Uongo, Unafiki na Gubu” wa kocha huyo...
    (5 March 2009)
Views: 901 | Maoni (9) | Soma Zaidi

 

Ambani aendelea kutikisa nyavu China

champion ijumaa  
Na Mwandishi Wetu

MUDA mfupi baada ya kutua katika Klabu ya Zhejiang Greentown FC, mshambuliaji hatari wa Yanga, Boniface Ambani ameifungia timu hiyo bao moja na kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi...
    (5 March 2009)
Views: 465 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Banka aahidi makubwa Simba

champion ijumaa  
Na Khadija Mngwai

KIUNGO mshambuliaji wa Timu ya Simba, Mohamedi Banka ‘Figo’ amesema mazoezi yanayotolewa na Kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri ni ya kiwango cha hali ya juu ambayo yatasababisha kupata ushindi katika ligi inayotarajia kuendelea hivi karibuni...
    (5 March 2009)
Views: 226 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jalada la E.P.A -6

hadithi za Shigongo  
Mtoto Adrian anatoka katika familia ya masikini kupindukia, yeye na dada yake Adventina wanalelewa na mama yao, hawakuwahi kumwona baba katika maisha yao na hawajui historia yake kwani mama yao hajawasimulia. Adventina ni mwanafunzi wa darasa la kwanza kwenye shule iliyoko umbali wa kilometa kumi na tano kutoka nyumbani kwao. Adrian hasomi lakini anatarajiwa kuingia darasa la kwanza mwaka ujao.

Familia hii inaishi kwa msaada wa Kanisa Katoliki, mara kwa mara wanapokuwa na shida huenda Parokiani na kumwomba Padri awasaidie. Mara ya mwisho walipokwenda wanakutana na Padri ambaye baada ya kuwasikiliza shida yao anaanza kumuuliza Adrian maswali ya hesabu na kushangazwa na uwezo ambao mtoto huyo alikuwa nao ingawa bado hata darasa la kwanza hajaanza!

Padri anaamua kumsaidia Adrian kusoma kwani amegundua kilichomo ndani yake, hakuwa mtoto wa kawaida! Msaada wake unakuwa ni kumpeleka kwenye shule ya seminari iitwayo Kiparato ambako anaanza darasa la kwanza, huko anakutana na watoto wengi wa matajiri kwani shule hiyo inaheshimika na watu wenye uwezo pamoja na viongozi hupeleka watoto wao hapo kupata elimu bora.

Miongoni mwa watoto aliokutana nao kwenye shule hiyo, tena kwenye darasa lake ni Edward, huyu ni mtoto wa mfanyabiashara aitwaye Lonjino ambaye kwake fedha ni kila kitu! Mtoto huyu amelelewa katika mazingira ya fedha, mazungumzo nyumbani kwao kila siku yanahusu fedha na wazazi wake kumwambia kabisa akikua ni lazima atafute utajiri na mbegu hiyo imepandikizwa ndani ya kichwa cha Edward.

Mtoto mwingine ambaye Adrian amekutana naye kwenye darasa lake ni Paul Kitumbi, pia mtoto wa tajiri, naye fedha maishani mwake ni kila kitu, anafahamu amekuja shuleni kusoma ili akimaliza Chuo Kikuu arejee nyumbani kusimamia shughuli za baba yake kwani yeye pekee ndiye mtoto wa kiume kwenye familia hiyo!

Adrian amezungukwa na matajiri, anajisikia mnyonge mbele ya wenzake na hana rafiki hata mmoja, ni aidha anatengwa au anajitenga mwenyewe. Hii inamfanya kila siku awakumbuke mama na dada yake Adventina aliowaacha kwenye dhiki kubwa, anaapa kusoma mpaka afanikiwe na kuikomboa familia yake.
Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO...
    (5 March 2009)
Views: 561 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI

photos  
Baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu leo aliibua varangati kubwa mahakamani hapo baada ya kumkataa laivu mama yake mzazi aitwaye Bi.Mariam Sepetu.
Wema alifanya kituko hicho na kuwaacha midomo wazi mamia ya watu waliokuwa mahakamani hapo muda mfupi baada ya kutoka nje ya mahakama ambapo alijinasua mikononi mwa mamayake kwa hasira na kuanza kumtafuta mpenzi wake aitwaye Yusuf Jumbe.
Kitendo hicho kilimpandisha ghadhabu kubwa mama yake pamoja na ndugu wengine ambao waliamua kumfuata binti huyo ili kumnasua kutoka mikononi mwa mpenzi wake.
“Nini hebu niachieni huko!Nyie vipii mbona mnanilazimisha kuondoka katika utaratibu nisiyouelewa?” Wema alisikika aking’aka wakati ndugu zake walipomvamia na kumpora kinguvu kutoka kwa Jumbe kisha kumuingiza ndani ya gari na kuondoka naye.
Wema ameachiwa nje kwa dhamana lakini mtuhumiwa mwenzake aitwaye Asha Jumbe amerudisha rumande Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuharibu gari la muigizaji mahili wa filamu nchini Steven Kanumba.

KAZA MWENDO SONGA MBELE HUKO! USITULETEE ZA KIMISS HAPA!
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Pichani, Wema Sepetu akiwa chini ya ulinzi mkali akiingizwa Mahakamani kwa ajili ya kuwekewa dhamana.

MBELE YA PILATO
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Wema Sepetu akiwa na mtuhumiwa mwenzake Asha Jumbe mahakamani leo.

WEMA, HIVI KWANINI LAKINI?
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Hashimu Lundenga akiteta jambo na mama mzazi wa Wema Sepetu nje ya mahakama wakipanga namna ya kumwekea dhamana.

NIMEKOMA JAMANI NISAMEHENI

WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Wema akipelekwa tena rumande kuchukua mazagazaga yake baada ya kuachiwa kwa dhamana.

HATIMAYE KICHEKO!
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Wema akiwa na mama yake mzazi Bi.Mariamu Sepetu wakitoka mahakamani mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.

JELA KUKOJE?
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Wema akihojiwa na mapaparazi muda mfupu baada ya kuachiwa, ambapo aliongelea mambo aliyokutana yayo a lupango alikokuwa anasota kwa siku kadhaa na kudai kuwa aliweza kuhimili mikikimikiki ya gerezani.

NGOJA NISUBIRI KIFAA CHANGU!
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Mpenzi wa Wema, Yusufu Jumbe (anayekunywa maji) akiwa amebana kona nje ya mahakama na washikaji zake akimsubiri Wema aachiwe kwa dhamana.

MREMBO KIMEOOOOOO!
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Umati wa watu ukiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kushuhudia vimbwanga alivyokuwa akifanya mrembo wao Wema Sepetu ambapo wengi wao walionekana kufedheheshwa na udhalilishaji ambao Wema alimfanyia mama yake mzazi.Watu hao walisikika wakimzomea mrembo huyo.

WAKATIMUA!
WEMA SEPETU AMKANA MAMA YAKE HADHARANI
Ndugu na jamaa wakiwa wamemuingiza Wema kinguvu kwenye gari hili kisha wakaondoka mahakamani hapo.

PICHA: CHRISTOHER LISSA NA MUSA MATEJA.
    (5 March 2009)
Views: 6529 | Maoni (46) |

 

VUNJA MBAVU

Vichekesho na Udaku  
VUNJA MBAVU
ZE NO IS NOT RICHABO
Kuna jamaa mmoja hivi juzi aliwaacha watu hoi maeneo ya Posta jijini Dar baada ya kujaribu kupiga simu ya mkononi kumpigia swahiba wake lakini simu ya jamaa yake ilikuwa haipatikani ila simu ilipomjibu jamaa huyo kuwa “Namba ya simu uliyopiga kwa sasa haipatikani tafadhali jaribu tena baadaye”. Ndipo jamaa alipoonekana akijibu simu hiyo kwa “We mpumbavu nini unanifanya mimi sina akili sio kama hii simu haipatikani mbona wewe umepokea sasa hebu mpe simu mwenye simu niongee nae bwege wewe.
Watu waliokuwa karibu na jamaa huyo walivunjika mbavu kwa ajili ya kucheka...[center]


    (5 March 2009)
Views: 572 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

MTOTO WA WAZIRI

Amani  
MTOTO WA WAZIRI
Na Waandishi Wetu

Mtoto wa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt. Makongoro Mahanga aitwaye Nickson Mahanga, amefanya unyama wa mwaka kwa kumpiga kwa chupa muuza mihogo Abdulrahman Haus Kapolo, hadi kuzimia...
    (5 March 2009)
Views: 1423 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Wema agombewa gerezani

Amani  
Wema agombewa gerezani
Na Mwandishi Wetu

Nyepesi nyepesi tulizozipata wakati tunakwenda mtamboni zimedai kuwa, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye juzi (Jumanne) alipelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea, amejikuta akigombewa na baadhi ya wanawake waliopo gerezani hapo huku kila mmoja akitaka kujenga ushoga naye...
    (5 March 2009)
Views: 3278 | Maoni (18) | Soma Zaidi

 

Ndanda Kosovo mbaroni kwa wizi

Amani  
Ndanda Kosovo mbaroni kwa wizi
Na Musa Mateja

Mwanamuziki wa muziki wa dansi hapa nchini, Ndanda Kosovo, jana (Jumatano), alitiwa mbaroni, Makao Makuu ya Polisi, jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya muziki...
    (5 March 2009)
Views: 984 | Maoni (4) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com