Jana jioni, Dereva wa pikipiki aliyejulikana kwa jina moja la Patrick, alikumbwa na balaa eneo la Sinza Kijiweni baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kumzidi maarifa na kuigonga gari ndogo aina ya Toyota Collora. Baada ya kuigonga gari hiyo, Bw. Patrick alianguka chini na kufikia kichwa lakini kofia ya usalama (Helmet) aliyovaa ilisaidia kulinda kichwa chake na kuumia goti la kushoto na sehemu nyingine za mwili.

...Pikipiki na gari lililopata ajali mara baada ya tukio.

DUH!!...Dereva wa pikipiki akitafakari jambo baada ya ajali.

...Wasamaria wema wakimuinua baada ya kushindwa kufanya hivyo mwenyewe.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL