arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 09.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Sura ya mtu, roho ya sh ...
» Jipambe ili kuongeza mv ...
» Kinachomsumbua JK chaju ...
» Simba yatengewa Mi.100 ...
» Mtoto anayedaiwa kuuzwa ...
» Bao la Bonny, jeuri tup ...
» WITNESS: Wasanii tupige ...

 

BAISKELI INAPOONGOZA SHERIA ZA BARABARA

photos  
BAISKELI INAPOONGOZA SHERIA ZA BARABARA
Mwendesha baiskeli akiwa amesimama mbele ya magari kwenye mataa ya makutano ya Barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Kawawa eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam. Wapanda baiskeli wengi hupoteza maisha kwa kujichanganya na magari sehemu kama hizi na kwa kutojua sheria za usalama barabarani.

KWA MMACHINGA POPOTE DUKA
BAISKELI INAPOONGOZA SHERIA ZA BARABARA
Wafanyabiashara za kutembeza maarufu ‘wamachinga’ hawana hiyana, wao popote pale wanaweza kufungua duka.
Pichani, kijana huyu alinaswa na kamera yetu, leo mchana, akiendelea na biashara zake katikati ya Barabara ya Ally Hassan Mwinyi maeneo ya Namanga, jijini Dar.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
    (9 March 2009)
Views: 296 | Maoni (0) |

 

NANI ZAIDI?

ijumaa wikienda  
NANI ZAIDI?

Katika Nani Zaid, wiki hii tunao mastaa wanaong’ara katika filamu nchini, Haji Adamu na Adam Kuambiana. Wasanii hawa hawajawahi kushiriki katika Tamthilia za Luninga, lakini wametokea kujitwalia umaarufu baada ya kuingia katika Tasnia ya Filamu nchini Tanzania. Baadhi ya sinema ambazo wawili hawa wameonyesha cheche zao ni pamoja na Fake Pastors, Sauti ya Manka na Regina (Adamu Kuambina) na Jeraha la Ndoa, Miss Bongo na Quick Money (Haji Adamu).
Je, kwa maoni yako, nani zaidi? Piga kura yako sasa!.
    (9 March 2009)
Views: 436 | Maoni (4) |

 

Vancouver kuwavaa Yanga leo

champion  
Vancouver kuwavaa  Yanga leo
Na Julius Kihampa

MABINGWA wa Ligi Daraja la Kwanza ya Marekani ya Kaskazini, Vancouver Whitecaps FC, leo wanashuka katika Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam kukipiga na mabingwa wa hapa, Yanga kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki...
    (9 March 2009)
Views: 281 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

DAR AKUNA KULALA

photos  
DAR AKUNA KULALA
Licha ya leo kuwa siku ya kazi lakini nyomi la watu alfajili hii lilinaswa na kamera yetu likiselebuka katika Bonanza la Akudo Impact, lililofanyika ufukwe wa Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam.

DAR AKUNA KULALA
Viongozi wa Bendi ya TOT Respect, Badi Bakule (kulia) na Abdul Misambano walinaswa wakikomaa wenyewe jukwaani katika onyesho la bendi hiyo, lililofanyika Ukumbi wa Mango Garden leo alfajili.

DAR AKUNA KULALA
Wanenguaji wa Bendi ya Msondo Music Band, Nacho Said, ‘Mama Nzawisa’ na Queen Emmy wakiwa wamejipumzisha baada ya kazi nzito ya kutikisa kiuno katika onesho la bendi yao lililofanyika Africentre jijini Dar, usiku wa kuamkia leo.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
    (9 March 2009)
Views: 377 | Maoni (1) |

 

DUU! NAONA KANDA BONGOMANI LEO HAJI HAPA!!!.

photos  
DUU! NAONA KANDA BONGOMANI LEO HAJI HAPA!!!.
Mc wa aliyekuwa akisherehesha katika onyesho la pamoja kati ya Kanda Bongomani na FM Academia, ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Msasani Club, akiwa amekaa huku akishindwa kuamini kwamba mwanamuziki huyo kutoka Kongo kaingia mitini.

KIUNO CHAKO HICHO…..
DUU! NAONA KANDA BONGOMANI LEO HAJI HAPA!!!.
Lilian Intarnet mnenguaji mahiri wa bendi ya African Stars, ‘Twanga pepeta, akinengua sambamba na mwimbaji wa bendi hiyo Ferguson, katika onyesho lililofanyika jana katika ukumbi wa TCC Chang’ombe jijini Dar.
Picha: Issa Mnally/ GPL.
    (9 March 2009)
Views: 543 | Maoni (1) |

 

DUKA LA NGONO

ijumaa wikienda  
DUKA LA NGONO
Na Waandishi Wetu

Maskini Tanzania! Sifa mbaya ya wawekezaji wa Kichina nchini, imeendelea kuchukua nafasi pana, baada ya hivi karibuni Ijumaa Wikienda kubaini biashara ya ngono, inayoendeshwa kama duka ndani ya hoteli ya kifahari jijini...
    (9 March 2009)
Views: 4301 | Maoni (29) | Soma Zaidi

 

ANAYECHEZEA NYETI WANAWAKE APEWA KIPIGO

ijumaa wikienda  
ANAYECHEZEA NYETI WANAWAKE APEWA KIPIGO
Na Imelda Mtema

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, mwishoni mwa wiki iliyopita alitunukiwa kichapo cha nguvu kutoka kwa mwanamke mmoja mwenye hasira kali baada ya kubaini kuwa, alikuwa akimfanyia vitendo vya uasherati...
    (9 March 2009)
Views: 1994 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

(Kimya milele-11)

hadithi za Shigongo  
Upelelezi wa mauaji ya mwanamke mwendawazimu yaliendelea, polisi wakafanikiwa kukutana na mtu aitwaye James Ngalo ambaye alishuhudia mtu akitupa koti daraja la salenda usiku wa manane, walipokwenda eneo hilo walilikuta koti pamoja na panga!

Wote wakafahamu aliyetupa koti hilo ndiye aliyemuua mwanamke mwendawazimu, upelelezi ukaendelea.
James Ngalo na mkewe Rachel Msangi ni Wanasheria wanaomiliki kampuni yao binafsi iitwayo James & Rachel Advocates, ni familia yenye watoto wawili mapacha Dana mwenye mtindio wa ubongo na Dona. Walianzia shughuli zao mjini Arusha na baadaye kuhamia Dar es Salaam ambako walifungua ofisi nyingine kubwa zaidi ya Uwakili, wakiwa na mtoto wao Dana, Dona alibaki Arusha akisoma shule ya Kimataifa Arusha.

Masaa machache tu baada ya James kutoa taarifa kwa polisi, mzee aitwaye Badru Mohamed anamtembelea ofisini kwake na kudai yeye ni mfanyabiashara wa mafuta na alikuwa akihitaji ushauri wake wa kisheria, kwa sababu James alikuwa na haraka ya kwenda kumpokea mtoto wake Dona ambaye siku hiyo alikuwa akirejea kutoka shule alitaka wakutane siku nyingine lakini mzee huyo akaomba hata kama ni nyumbani amfuate usiku maana alikuwa na shida ya haraka, kwa jinsi alivyoonekana, James hakukataa, akamkaribisha nyumbani kwa chakula cha usiku.

Badala ya saa mbili usiku mzee Badru aliwasili saa tatu usiku na kufunguliwa mlango, mtoto Dona alikuwa chumbani amelala, sebuleni alikuwepo Rachel akiwa amembeba mtoto wao mwenye mtindio (Dana).

Katika hali ambayo James na Rachel hawakuitegemea kwani walishatayarisha chakula cha mgeni, walishangaa kumwona mzee Badru akichomoa bastola kwenye koti na kuanza kuwamiminia wote watatu!

Dona alisikia kelele akiwa chumbani, akanyanyuka na kuanza kutembea kwenda sebuleni, akamwona mzee mwenye bastola mkononi, taratibu akakimbia na kujificha kwenye kona pembeni kabisa ya nyumba.

Badala ya kwenda chumbani ambako mzee Badru alikwenda na kumsaka kila sehemu bila mafanikio. Dona akatoka hadi nje na kukimbia kwenye bustani ambako alijificha katikati ya migomba, baadaye akasikia hatua za mtu zikielekea eneo hilo na tochi ikimulika, alikuwa ni mzee Badru akimtafuta ili ammalizie, akafika mpaka kwenye migomba na kusimama kando yake, Dona alisikia mwili ukifa ganzi, hata sauti ya kuhema kwake aliisikia ni kubwa, kiasi kwamba mzee huyo angegeuka tu nyuma lazima angemwona na kummiminia risasi.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (9 March 2009)
Views: 1094 | Maoni (18) | Soma Zaidi

 

Shoga, kama ‘mista’ wako bahili mpe kadi nyekundu

Mahaba  
Ni wiki nyingine tofauti kabisa na wiki iliyopita ambapo tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida...
    (9 March 2009)
Views: 505 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Niliishi kuzimu miaka ishirini Part-II-20

Mikasa ya kusisimua  
Zubeda Ruvanga, mwanamke mwenye umri wa miaka 38, anasimulia mateso aliyokumbana nayo tangu akiwa mtoto. Wachawi walianza kumpa tabu za maisha tangu akiwa darasa la tatu kwenye Shule ya Msingi Mwandiga Kigoma. Wiki iliyopita alikomea pale alipoangua kilio mbele ya kundi la wachawi waliokuwa kwenye sherehe ya kumpokea kuwa malkia wao, hivyo kumchanganya Mfalme Dajani aliyewanyamazisha wachawi wote na kumuuliza Zubeda kilichokuwa kinamliza. Endelea kusoma sehemu ya pili ya mkasa huu wa kusikitisha...
    (9 March 2009)
Views: 627 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

KONDIC, PHIRI: MAXIMO Siyo

champion  
KONDIC, PHIRI: MAXIMO Siyo
Na Mwandishi

HUKU wadau mbalimbali wa soka wakidai Kocha wa Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo hafai kuendelea kukinoa kikosi hicho kutokana na kuwatenga wachezaji wake, akiwemo kiungo wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ na wa Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’, makocha wa klabu hizo nao wameunga mkono...
    (9 March 2009)
Views: 676 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Simba yashusha tambo Ligi Kuu

champion  
Na Chausiku Omar

KOCHA Mkuu wa Timu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri, ameshusha tambo zake Ligi Kuu ya Vodacom kwa kudai kuwa, hakuna timu itakayoweza kukizuia kikosi chake kushika nafasi ya pili kwa kuwa anaiandaa kwa kazi hiyo...
    (9 March 2009)
Views: 218 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Al Ahly yaipa nafasi Yanga

champion  
Na Julius Kihampa

KLABU ya Al Ahly ya Misri inazidi kubanwa mbavu na kuurahisisha mchezo wao dhidi ya Yanga baada ya kwenda sare ya bila kufungana na Timu ya Polisi ya huko ikiwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo juzi huku kiungo wao wa kutumainiwa Mohammed Barakat akilimwa kadi nyekundu...
    (9 March 2009)
Views: 227 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jarida la EPA -7

hadithi za Shigongo  
Padri anaamua kumsaidia Adrian kusoma kwani amegundua kilichomo ndani yake, hakuwa mtoto wa kawaida! Msaada wake unakuwa ni kumpeleka kwenye Shule ya Seminari iitwayo Kiparato ambako anaanza darasa la kwanza, huko anakutana na watoto wengi wa matajiri kwani shule hiyo inaheshimika na watu wenye uwezo pamoja na viongozi hupeleka watoto wao hapo kupata elimu bora.

Miongoni mwa watoto aliokutana nao kwenye shule hiyo, tena kwenye darasa lake ni Edward, huyu ni mtoto wa mfanyabiashara aitwaye Lonjino ambaye kwake fedha ni kila kitu! Mtoto huyu amelelewa katika mazingira ya fedha, mazungumzo nyumbani kwao kila siku yanahusu fedha na wazazi wake kumwambia kabisa akikua ni lazima atafute utajiri na mbegu hiyo imepandikizwa ndani ya kichwa cha Edward.

Mtoto mwingine ambaye Adrian amekutana naye kwenye darasa lake ni Paul Kitumbi, pia mtoto wa tajiri, naye fedha maishani mwake ni kila kitu, anafahamu amekuja shuleni kusoma ili akimaliza Chuo Kikuu arejee nyumbani kusimamia shughuli za baba yake kwani yeye pekee ndiye mtoto wa kiume kwenye familia hiyo!

Adrian amezungukwa na matajiri, anajisikia mnyonge mbele ya wenzake na hana rafiki hata mmoja, ni aidha anatengwa au anajitenga mwenyewe. Hii inamfanya kila siku awakumbuke mama na dada yake Adventina aliowaacha kwenye dhiki kubwa, anaapa kusoma mpaka afanikiwe na kuikomboa familia yake.
Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
    (9 March 2009)
Views: 608 | Maoni (4) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com