Timu ya soka ya Yanga jana ilicheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na timu ya soka ya Vancouver Whitecaps, kutoka Canada na kuifunga mabao 3-0.
Wachezaji wa Timu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, wakisalimiana na mashabiki wao wachache wanaoishi nchini, ambao walijitokeza kuwashangilia.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la tatu, lililofungwa na Mike Barasa, aliyenyoosha mikono juu.
Mshambuliaji wa Timu ya soka ya Yanga, Benny Mwalala, akimtoka beki wa timu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Taifa.
Wacanada wanaoishi nchini wakiwa uwanjani kuishangilia timu yao ya Vancouver Whitecaps, wakati ikipambana na timu ya soka ya Yanga ya Tanzania. PICHA: ISSA MNALLY /GPL.
MREMBO mmoja mkazi wa Yombo Kisiwani ,manispaa ya Ilala ,jijini Dar es salaam aliyejulikana kwa jina la Salome, ametajwa katika ujumbe wa maandishi kuwa ndiye aliyesababisha kijana, Atupele Mwakaboko (25), ajiue kwa kujinyonga ndani ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Kasulu maeneo ya Buguruni wiki iliyopita baada ya kupewa mimba...
UGONJWA wa Pumu uliomuua Mwandishi na Mtangazaji wa ITV/Radio One, Rehema Mwakangale, unatajwa kuwa wa hatari na utawamaliza watu wengi, hasa wale wanaotumia muda mwingi kukaa kwenye kiyoyozi (Air Conditioner) na hali ya ubaridi...
HAJA ya Shirika la Umeme nchini, TANESCO kununua mitambo ya kuzalisha umeme kutoka Kampuni ya Dowans, imeelezwa kuwa mkakati wa kifisadi uliolenga kuwanufaisha vigogo walioshiriki kikamilifu kuingiza kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond LLC na baadaye kuirithisha ile ya Dowans wakati taifa likiwa kwenye mgogoro mkubwa wa nishati ya umeme mwaka 2007...
TULIPATA uhuru wetu mwaka 1961 bila shaka kwa waliokuwepo siku hiyo wanakumbuka vizuri jinsi matumaini ya Watanganyika yalivyochipuka upya, kwamba Mkoloni sasa alikuwa anaondoka na kuwaacha wakijiamria mambo yao wao wenyewe! Hata kwa mimi ambaye sikuwepo siku hiyo naweza kuhisi ilikuwa ni siku ya furaha kiasi gani kwa watu ambao kwa muda mrefu walikuwa wamengandamizwa na mtu mweupe na sasa ilikuwa imefika siku ya kujitawala wenyewe...
Priscilla anatoroshwa ndani ya danguro la Lightness na mwanaume mzungu aitwaye Jimmy na kusafirishwa hadi Humberg nchini Ujerumani, hakujua anapelekwa kufanya nini, akilini anaamini kusudio la kuumbwa kwake ni kuteseka siku zote za maisha yake. Mwili wake unatetemeka kwa woga na hajui atafanyiwa ukatili gani. Jimmy anamfundisha jinsi ya kutumia vifaa ikiwemo kufungua milango, kutumia koki za maji na baadhi ya vifaa vya umeme. Saa tisa usiku mlango wa chumbani kwake alipolala unafunguliwa akaingia Jimmy, muda mfupi wakati wanaongea akaingia mwanaume mwingine anayeitwa Miloslov Laurence, jambo linalomtisha zaidi ni kitendo cha Jimmy kutoka bila kumtambulisha vizuri na kumuacha mwanaume huyo chumbani. Je, mwanaume huyo ni nani? SONGA NAYO...
Katika ndoa nyingi kuna siri ambazo si rahisi kuzibaini kwa macho wala maneno, Shakila ni mwanamke katili licha ya kuubwa na sura nzuri inayowavutia wanaume wengi, ndani ya ndoa yake ameishi na mumewe kipindi cha miaka mitatu bila mtoto ndipo anapowatesa watoto aliowakuta ndani ya familia akiwapiga kila leo. Kitu kinachomkosesha raha ni jinsi gani angemuua mumewe ili kuolewa na tajiri.
Siku moja anamualika mpenzi wake mwenye asili ya kiarabu nyumba anapoishi na mumewe na ndipo anafumaniwa na mama yake mzazi, mshenga na mumewe, hata hivyo anadiriki kujitetea kuwa hajaolewa na wazazi wake wanamlazimisha kuolewa na mwanaume asiyempenda. Hapo ndipo mumewe anapoandika talaka na kuiweka mezani kwa ajili ya kuachana na mkewe ili akaolewe na tajiri, mwarabu.
Baadaye mumewe anamkabidhi talaka tatu hali ambayo inamshutua sana mama yake mzazi na kujaribu kumbembeleza mkwe wake asichukue uamuzi huo, mumewe anamsamehe na kuanza maisha mapya yaliyojaa mapenzi moto moto. Miezi miwili baadaye Shakila anapokea meseji kutoka kwa Saidi akimtaka watoroke kwenda Uarabuni. Je, nini kitaendelea? Fuatilia....