arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 11.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» JIDE HOI
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» HUKUMU YA BABU SEYA!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» MHE. SITTA KUNG’OKA
» Yanga mpya hii hapa
» Miss Utalii
» Masanja Mkandamizaji n ...
» TUZO ZA MADENTI
» NILIMUUA MUME WANGU NIO ...
» Bahati nasibu ya jishin ...

 

ZIARA YA PINDA DAR KIBOKO!

photos  
Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda leo ameanza ziara mkoani Dar es Salaam, ambapo amekagua masoko wilayani Ilala.
Akiwa katika Soko kuu la Kariakoo, Waziri Mkuu alionesha kutoridhishwa na uendeshaji wa soko hilo kwa kile alichodai linaendeshwa kwa hasara. Katika kuonesha kuwa Waziri Pinda ni kiboko, alikuwa akiwahoji watendaji wa masoko hayo ‘Laivu’ ambapo wengi walijikuta wakishikwa na kigugumizi cha kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha. Ziara hiyo inaendelea kesho katika Wilaya za Temeke na Kinondoni ambapo itahitimishwa katika ukumbi wa Arnatoglou Ilala kwa ajili ya majumuisho.

ZIARA YA PINDA DAR KIBOKO!
Waziri Mkuu (Mwenye mawani) akiongea na mmoja wa wafanyabiashara ndani ya soko la Kariakoo.

ZIARA YA PINDA DAR KIBOKO!
Waziri Mkuu akiongea na mwanamama muuza matunda ndani ya soko la Kariakoo shimoni.
PICHA:CHRISTOPHER LISSA/GPL.
    (11 March 2009)
Views: 208 | Maoni (3) |

 

RAMA MLA WATU ACHARUKA KORTINI

photos  
RAMA MLA WATU ACHARUKA KORTINI
Mtuhumiwa wa mauaji, Bwana mdogo Ramadhani Selemani ( wapili kutoka kushoto) akiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu leo. Rama alizua varangati kubwa mahakamani hapo dhidi ya wapiga picha na kuiomba mahakama hiyo kuwazuia waandishi wa habari kufuatilia kesi yake.

MAMA RAMA SASA MAMBO SAFI GEREZANI
RAMA MLA WATU ACHARUKA KORTINI
Mama mzazi wa Ramadhani Selemani (kushoto) anaonekana kunawiri kiasi cha kushangaza watu tokea aliposwekwa rumande pamoja na mwanaye kwa kesi ya mauaji, ambapo mwanaye alibambwa akila kichwa kibichi cha mtoto maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam mwaka jana.
PICHA :CHRISTOPHER LISSA/GPL.
    (11 March 2009)
Views: 850 | Maoni (7) |

 

ALIYEMZABA KOFI MZEE RUKSA APIMWA AKILI.

photos  
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alizungumzia ishu ya Ustaadh Ibrahim Said au maarufu kama Sultan, anayeshikiliwa na Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa kosa la kumshambulia hadharani kwa kumpiga kofi Rais Mstaafu, wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi jana.

Mpaka kufikia leo saa saba mchana, Kova amesema kijana huyo bado alikuwa akiendelea kupimwa akili na wataalamu wa magonjwa ya akili wa hospitali hiyo kabla ya kumfikisha mahakamani.

Ustaadh huyo alimzaba kofi Mzee Ruksa wakati akihutubia Baraza la Maulid ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee Machi 10, mwaka huu (Siku ya Jumanne).

ALIYEMZABA KOFI MZEE RUKSA APIMWA AKILI.
Kamanda Kova akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake.
PICHA :RICHARD BUKOS /GPL.
    (11 March 2009)
Views: 417 | Maoni (5) |

 

PRAVEN KIZIMBANI TENA LEO

photos  
Jamaa anayeshikiliwa kwa kudaiwa kumuua mwenzake, Vinoth Praven pamoja na mkewe Komal Katakia leo, walipandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako kesi yao iliahirishwa mpaka Machi 23 wakati uchunguzi bado unaendelea.

PRAVEN KIZIMBANI TENA LEO
Vinoth akiwa Mahakamani leo.

PRAVEN KIZIMBANI TENA LEO
Bi.Komal naye akiwa Mahakamani leo.
PICHA:RICHARD BUKOS /GPL.
    (11 March 2009)
Views: 350 | Maoni (6) |

 

MABONDIA MAARUFU KUTWANGANA MACHI 28

photos  
Mabondia maarufu hapa nchini Kalama Nyilawila, Hussein Chiwa, wanatarajiwa kupambana katika Ukumbi wa Luxury Pub Temeke jijini Dar, Machi 28 mwaka huu katika pambano la Kg 72 (Middle) round 10.

RAIS WA T.P.B.O
MABONDIA MAARUFU KUTWANGANA MACHI 28
Rais wa chama cha ngumi za kulipwa T.P.B.O Yasin Abdalah, ‘Ustaadh’ akitangaza rasmi kwa wanahabari kuwepo mpambano huo.

UTAJUTA KUNIFAHAMU
MABONDIA MAARUFU KUTWANGANA MACHI 28
Bondia Hussein Chiwa (kushoto) na Karama Nyilawila, wakitambiana wakati wa utambulisho wa pambano lao Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, katikati ni promota wa pambano hilo William Ng’ingo.
PICHA:RICHARD BUKOS /GPL.
    (11 March 2009)
Views: 244 | Maoni (1) |

 

vichekesho!

---  
[
b]1) Mtoto mmoja alikuwa akipenda kutaniwa na bibi yake kwa kumwita" mme wangu" kumbe neno hilo lilimkaa sawa kichwani. siku moja alikurupuka na kumwendea baba yake. Maongezi yao yakawa hivi:
Mtoto: Baba mi nataka kuoa!
Baba: Sasa una mchumba tayari?
Mtoto: si nitamuowa Bibi!?!!
Baba: Ha! umuowe mama yangu?
Mtoto: we si ulimuowa mama yangu??
Mzee akachanganyikiwa. duh ilikuwa kali hiyo.[/b]..

[
i]2. Vichaa wawili walikuwa jijini Bongo wakiyaangalia majengo marefu yaliyokuwa yamejengwa hapo!
Baadaye wakaliona ghorofa moja zuri sana, basi wakajadiliana walihamishie maeneo ya baharini. "poa!" wakakubaliana
wakalisukuma wee hadi jasho kuwatoka, wakaamuwa wavuwe mashati ili wajisikie bomba kisha wakaendelea na zoezi la kulihamisha jumba hilo. kumbe baadaye walikuja watoto na kuchukuwa zile shati bila jamaa kugundua hilo,
baada ya saa nzima vichaa hao wakiwa wameshikilia kuta za jengo hilo mmoja akageuka nyuma na kusema:
"kazana bwana kazana tumelifikisha mbali sana!!"
"Kwani vipi mwenzangu?"
"si unaona hata nguo tumeshaziacha mbali sana hazionekani hata kidogo!" hadi usiku walikuwa bado wakilisukuma!
Duh Vichaa wengine!!
[/[/i]
color]
na Eric Esron Mungere
+1-402-686-1128
erryesron@yahoo.co.uk
United States[/right][/b][/i]
    (11 March 2009)
Views: 262 | Maoni (0) |

 

Machangudoa wa Kichina...

risasi mchanganyiko  
Machangudoa wa Kichina...
Na Mwandishi Wetu

Unapokwenda Msasani kwa Nyerere kupitia barabara inayotokea Sayansi kuelekea Baa maarufu ya Rose Garden, mbele kuna kibao kulia kimeandikwa SINO A, RECREATIONAL CLUB, Chinese Massage & Hotel na kukuelekeza kuingia kushoto ili kuikuta hoteli hiyo...
    (11 March 2009)
Views: 2859 | Maoni (20) | Soma Zaidi

 

Wema Sepetu ameathirika!

risasi mchanganyiko  
Wema Sepetu ameathirika!
Musa mateja na Christopher Lissa

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Anko Hashimu Lundenga, ameelezea kusikitishwa kwake na matukio yanayomkumba Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (20) na kudai kuwa, ni vema Mnyange huyo akapimwa ili kujua endapo ameathirika na dawa za kulevya, hivyo kurahisisha zoezi la kumrekebisha...
    (11 March 2009)
Views: 2670 | Maoni (24) | Soma Zaidi

 

ASHA BARAKA ACHECHEMEA

risasi mchanganyiko  
ASHA BARAKA ACHECHEMEA
Na Issa Mnally

Hali ya kiafya ya Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, bado ni tete baada ya kurejea nchini akitokea Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu ya mguu, ambapo sasa anachechemea...
    (11 March 2009)
Views: 1121 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Msitu wa Pande-3

hadithi za Shigongo  
Umeibuka ugonjwa mpya katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ugonjwa huu unaitwa Chinese Encephalitis, ukienezwa na Mbu aitwaye AnophelenX, ni ugonjwa hatari ambao mpaka hivi sasa hauna tiba wala kinga na umekwishaua idadi ya watu elfu moja na mia mbili nchini Kongo. Taarifa ambazo CNN wametangaza muda mfupi uliopita ni kwamba tayari ugonjwa huo unavuka Ziwa Tanganyika kuingia Tanzania ambako unatarajiwa kuua idadi kubwa ya watu.

Hali hii imesababisha hofu kubwa na watu wengi wenye fedha zao wameanza kupanda ndege kuikimbia Tanzania wakiwaacha watu masikini wafe hii ni habari ya kusikitisha, hofu kubwa imetanda kila sehemu ya Tanzania. Jacob Steven ni mchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mume wa Angela na wana mtoto mmoja mzuri aitwaye Natalia ambaye kila mtu aliyemwona anahisi atakuja kuchukua hata taji la Urembo wa Dunia, familia yao ni yenye furaha.

Taarifa alizoziona kwenye luninga zimemshtua sana Jacob, naye anafikiria kuondoka nchini kwenda kujificha Uingereza mpaka hali itakapotulia. Ameamua kuandika barua ya kuomba likizo, alipoimaliza tayari ni saa kumi na moja jioni, saa za kazi umekwishakupita hawezi kuiwakilisha barua yake kwa bosi mpaka siku inayofuata.

Muda huo huo anapokea simu kutoka kwa mke wake Angela ambaye anampa taarifa kuwa mtoto wao Natalia ana homa kali! Taarifa hizi zinazidi kumchanganya Jacob ambaye mara moja anaamua kwenda nyumbani, huko wanamchukua mtoto na kumpeleka Hospitali ya Dk. Pandya, Bingwa wa Matatizo ya Watoto Wadogo. Jambo la kwanza ambalo daktari huyo anafanya ni kumpima Natalia joto kabla hajaendelea na mambo mengine.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO….
    (11 March 2009)
Views: 772 | Maoni (9) | Soma Zaidi

 

Nataka kichwa cha mwanangu-21

Mikasa ya kusisimua  
Maisha ya Mzee Muddy yanatawaliwa na mabalaa, sasa nyumba nzima imezimia na wote wanatokwa na damu kila sehemu ya miili yao.
Mzee Muddy anapelekwa baharini, akiwa huko anapewa adhabu ya kifo, anazamishwa baharini. Je, nini kitatokea? Mwandishi wetu JOSEPH SHALUWA anaendelea...
    (11 March 2009)
Views: 845 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Migogoro, malumbano na ugomvi! ...mnamalizanaje na mpenzi wako?

Mahaba  
Migogoro, malumbano na ugomvi! ...mnamalizanaje na mpenzi wako?

Hili ni Darasa la Maisha, kwa mara nyingine tena nakualika hapa ili tuweze kubadilishana mawazo kuhusu haya mahusiano yetu. Ninayekupa kadi ya kujumuika nami hapa ni mimi Joseph Shaluwa ambaye wasaa kama huu pia hupatikana katika magazeti ndugu na hili Ijumaa pamoja na Risasi Jumamosi...
    (11 March 2009)
Views: 572 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

Al Ahly yaihofia Yanga

champion  
Al Ahly yaihofia Yanga
NA WAANDISHI WETU

KISHINDO! Baada ya kuboronga katika michezo yake mine mfululizo ya Ligi Kuu ya Misri, Kocha wa Al Ahly Manuel Jose de Jesus ameanza kupata hofu kuhusu pambano lake dhidi ya Yanga la Ligi ya Mabingwa Afrika linalotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo...
    (11 March 2009)
Views: 433 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

Phiri amjia juu Boban

champion  
Na Adolph Balingilaki

NIDHAMU? Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri (pichani) amemjia juu mchezaji tegemeo wa timu hiyo, Haruna Moshi ‘Boban’ kwa kitendo cha kuchelewa kuripoti kambini na kumtaka afanye hivyo haraka...
    (11 March 2009)
Views: 452 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

... Maximo: Nina siri yake

champion  
Na Shufaa Lyimo

SIRI SIRINI! Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema ana siri nzito ya mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ na endapo ataitoa mchezaji huyo anaweza kuhama hata nchi...
    (11 March 2009)
Views: 645 | Maoni (0) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com