Kijana Ibrahim Said, anayejiita Ustaadh, leo alikiri kosa la kumzaba kofi Mzee Ruksa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Mh. Neema Chusi. Akisoma kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Monica Mbogo, alimwambia mshitakiwa kuwa anashitakiwa kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili kwa kumpiga kofi Rais Mstaafu, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, mnamo Machi 10 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar. Mshitakiwa bila kuisumbua Mahakama, alikiri kufanya kosa hilo ambapo Hakimu anayeendesha kesi hiyo iliiahirisha kwa saa moja na hatimaye kuipiga tena kalenda kesi hiyo mpaka kesho.
HIVI NDIVYO ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI ...Ustadh Ibrahim akiwa tulii na bangili zake (pingu) ndani ya Difenda kabla hajashushwa.
SHUKA WEWEEE… ...Maafande wakimshusha Ustadh Ibrahim. SIJUWI NAPELEKWA WAPI Vijana wa usalama hawataki kujiharibia tena licha ya kumpiga pingu, wameona wasipomkwida inawezakuja aibu nyingine.
AKIWA AMESIMAMIWA NA AFANDE ...Askari wa Mahakama ya Kisutu akimlinda Ustadh baada ya kufikishwa mahakamani hapo.
AKIINGIZWA MAHAKAMANI ...Maafande wa Mahakama ya Kisutu wakimuingiza mahakamani ili kusomewe kosa lake.
ALIPOINGIZWA MAHAKAMANI ...kiwa katika pozi kabla ya kusomewa makosa yake
KIJANA UMEIDHARAULISHA IDARA YETU ...Akiwa chini ya ulinzi mkali wa wana usalama
BAADA YA KUKIRI KOSA ...Ustadh akirudishwa rumande baada ya kukiri kosa mpaka kesho atakaporudishwa tena mahakamani hapo kwa hukumu yake. PICHA: CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS/ GPL
Kutokana na kuibuka kwa tabia ya kuandika maoni yenye matusi, tumelazimika kuweka utaratibu wa kuchuja kwanza maoni (Moderation) kabla ya kuyaruhusu kusomwa na wengine. Kwa mabadiliko haya, kwa heshima na taadhima, tunawafahamisha wasomaji wetu kuwa kuanzia sasa ukituma maoni hayataonekana muda ule ule kama ilivyokuwa zamani, bali yataonekana baada ya muda, hivyo usitie shaka. Jambo muhimu la kuzingatia katika mabadiliko haya ni LUGHA. Hatutaruhusu matusi kabisa, maoni yenye matusi hayatapata nafasi ya kuonekana 'hewani'! Toeni maoini yenye nguvu za hoja, kosoeni pale tunapokosea au kusoaneni wenyewe bila kashfa wala matusi. Tunawapenda na kuwajali sana! ASANTENI! WEBMASTER!
Baba ziro mtoto sifuri Baba mmoja alikuwa akimchapa mwanae kwa kosa la kutofanya vizuri kwenye mtihani, mara mkewe akatokea na mazungumzo yalikuwa hivi: Mke: Jamani mume wangu mbona unampiga mtoto kiasi hiki nhe? Mume: Hana akili kabisa huyu Mke: Kwani kafanyaje? Mume: Kakosa swali rahisi sana kwenye mtihani ananitia aibu Mke: Swali gani? Mume: Eti hamjui Rais wa Zanzibar ni yupi Mke: Yeye kajibuje? Mume: Eti kajibu Rais ni Lipumba wakati Rais wa Zanzibar ni Mrema Mke: Ebo! We ziro na mtoto pia sifuri...
Khaa! Siri ya kijana Ibrahim said kumzaba kibao Rais Mtaafu wa awamu ya Pili, ali Hassan Mwinyi imefichuka baada ya timu ya waandishi wetu kuizamia kwa kina ishu hiyo iliyotokea ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam juzi (jumanne)...
Habari tulizozipata wakati tunajiandaa kwenda mtamboni zimeeleza kuwa, msanii wa kundi la maigizo la Kaole ambaye pia ni muigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko pamoja na mchumba wake ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara (pichani juu) wamepata ajali na kuumia vibaya...
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu ya wiki hii kwamba, hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa kimapenzi kama kusikia mpenzi wako anatembea na mtu mwingine tena ambaye huenda unamfahamu, inauma kuliko maelezo. Ambao wamewahi kusalitiwa wanayajua maumivu yake...
Mpenzi msomaji, kijana Beka anaendelea kusimulia mkasa uliomkuta huko Bububu Zanzibar ambapo babu mmoja aliyetokea kumpenda alimfundisha uchawi. Wiki iliyopita nilielezea alivyofanikiwa kutatua matatizo ya jamaa mmoja kutoka Unguja ambaye alikuwa mtu wa kwanza kumtibia baada ya kufundishwa mambo ya kichawi na uganga. Leo anaendelea kusimulia mambo aliyoendelea kukutana nayo katika maisha yake. Ungana na Mwandishi Wetu KULWA MWAIBALE aliyefanya mahojiano na kijana huyo katika kisa hiki cha kweli…
Usomi wa ngazi mbalimbali si sifa ya mtu kufaa kuwa kiongozi, dunia katika historia yake ina majina mengi ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa wasomi, lakini hatima ya uongozi wao haikutofautiana na wale ambao hawakwenda shule...
Tom anaoza kwa mapenzi mazito juu ya msichana mrembo Mayasa, mtoto wa mjini anayejua kila njia za kumdhibiti mwanaume! Kitu cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kwenda ‘kumtengeneza’ kwa Mganga wa Kienyeji ambapo baadaye Tom anakuwa hashiki wala hakamatiki kwa Mayasa.
Anampa mpaka namba za siri za kadi zake za benki, uhuru anaompa katika biashara zake unakuwa mkubwa kuliko kawaida, hata Mariam hana uhuru aliokuwa nao Mayasa. Baada ya kunogewa na penzi lake, anamnunulia nyumba kwa siri, anaifanyia ukarabati kisha anampeleka na kumkabidhi.
Katika hali ya kushangaza sana, Mayasa anamwambia Tom akubali kwenda kulala nyumbani kwake, pamoja na kwamba alikuwa akifahamu kwamba ana mke. Linakuwa jambo zito sana kwa Tom, lakini Mayasa anaendelea kumng’ang’aniza. Je, atakubali? Nini kitatokea? Ssa SONGA NAYO...