Aliyekuwa Mbunge wa Busanda mkoani Mwanza (CCM), Mh. Faustine Rwilomba, aliyefariki juzi nchini India, leo ameagwa katika Kanisa la Mtakatifu Peter, Oysterbay jijini Dar es Salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kanisani hapo. Mtandano wenu ulikuwepo kunasa tukio hili la msiba.
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Faustine wakiliingiza kanisani kwa ajili ya ibada ya mazishi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda, akimuaga marehemu Faustine.
Dada wa marehemu, Bi. Benadeta, akilia kwa uchungu wakati akimuaga marehemu kaka yake.
Mtoto wa marehemu, Frednand, nae alipata nafasi ya kumuaga baba yake mpendwa.
Waombolezaji wakijiandaa kumpeleka marehemu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya ibada, tayari kwa safari ya Mwanza.
Maafande wakitoa jeneza la marehemu tayari kwa safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege.
Mwandishi wetu, Christopher Lissa, akifanya mahojiano mafupi na waziri wa zamani Mh. Mramba kuhusu alivyomfahamu marehemu. PICHA :CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS /GPL
Kabla ya kupata uhuru wetu hapo awali tulikuwa na vyama vingi vya kupigania haki za wafanyakazi lakini si vyama vya siasa.Chama cha TANU kilichokuwa hapo awali chama cha wafanyakazi kilikuja kujeuka na kuwa chama cha siasa ambapo sera za waasisi wake ndio zilizotuletea uhuru. Baada ya kupata uhuru nchi yetu chini ya chama hiki kimoja cha siasa kilijaribu kuiga mbinu mbalimbali katika kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli.Tuliona jinsi sera kama ya ujamaa jinsi ilivyoshindwa kukabili shida za taifa letu kwa wakati ule.Rais wetu kwa wakati ule Mwalimu Nyerere alisisitiza kuwa Tanganyika ilihitaji chama kimoja cha siasa kwa sababu mbalimbali. Taifa letu lilikuwa changa na lilihitaji mwongozo dhabiti na watu wenye kujitolea ili kuliongoza na hivyo vya vya siasa kwa wakati ule vingeleta malumbano na mgawanyiko katika jamii hivyo kukwamisha juhudi za maendeleo.Nyerere alisistiza kuwa TANU hakikuwa chama cha siasa chenye kupigania maslahi flani ya kisiasa bali kilikuwa ni chama cha wananchi ambacho kilikuwa na madhumuni ya kuwaletea watanganyika maendeleo ya kweli.Aliendelea kusisitiza kuwa hata mwanzo wa chama cha TANU maslahi yake yalikuwa kupigania haki za wafanyakazi nahivyo ilkuwa vigumu kwa viongozi wa TANU kuanza kulumbana juu ya masuala ya siasa kwani dhumuni lao lilikuwa kuwaletea Watanganyika maendeleo. Katika kipindi cha utawala wa Mwalimu tuliona Tanzania ikifanya vizuri katika nyanja ya elimu na hivyo kuongeza idadi ya watanzania wanaoweza kusoma ikikuwa mpaka kufikia asilimia 80% na hivyo kufanya Tanzania kuingia katika nchi chache barani Africa zenye idadi kubwa ya watu wenye uwezo wa kusoma na kuandika.Pia katika uchumi wetu tuliona bei za vyakula ikiwa ndogo na chakula kilikuwa cha kutosha.Hata Hivyo sera za baba wa taifa hili ambazo zilikuwa za kuwaletea watanzania mandeleo ya kweli zilishindwa kufanya kazi kama ilivyotajiriwa na hivyo kufanya baba wa taifa hili aachie madaraka bila choyo na kuwapa watanzania wengine watuongoze katika juhudi za kutulea maendeleo ya kweli. Tukirudi katika hali ya sasa tunaona kuwa wale ambao baba wa Taifa hili aliwaamini na kuweka dhamana ya Watanzania wamekuwa walafi wa madaraka na wenye choyo huku wakijinufaisha wenyewe na mali za Watanzania .Tumeshuhudia hivi karibuni kesi mbalimbali za ufisadi zikirindima katika nchi yetu na malumbano ya kisiasa yakichukua mkondo mpya. Hapo awali Mwalimu alisisitiza kuwa vyama vingi vya siasa ni mzigo kwa taifa lolote changa.Hata hivyo Tanzania yenye kusifika kwa amani na busara za viongozi wake ilifuata mfumo wa democrasia na kuruhusu vyama vingi vya siasa. Vyama hivi vya siasa vimekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha malumbano na migogoro mingi ya kisiasa. Hali hii inaweza katafsiriwa kuwa ni uroho wa madaraka walionao wanasiasa wetu ambao huja na kuomba kura zetu kisha baadae kuanza kutafuna fedha za wananchi walewale waliowachagua. Raisi wetu ambaye anajitahidi kuliongoza taifa hili changa kwa uwazi na democrasia amekuwa akilaumiwa kwa kutoleta maendeleo ya kweli na baadhi ya wapinzani. Watanzania ambao wamekata tamaa wamekuwa wakiweka imani kubwa katika viongozi wao bila ya kujituma na baadae kuwalaumu kwa kutowaletea maendeleo. Sasa hivi ni muda wa watanzania kuamka na kutafakari hali ya sasa na kushirikiana na viongozi wetu katika juhudi za kujiletea maendeleo. Huu si muda wa kuanza kutilia mkazo masuala yasiyo na maana kama kuwekeza nguvu zote katika kufichua mafisadi huku tukisahau kuwa umaskini wetu bado uko pale pale. Sisemi kuwa tuache kuwafichua hawa mafisadi ila tusijisahau kuwa bado tuko katika taifa changa na nguvu zetu zinatakiwa ziegemee katika kujiletea maendeleo. Basi ndugu zangu Watanzania tuamke na tujiletee maendeleo ya kweli ambayo yanaanzia katika elimu huku tukikumbuka msemo wa baba wa taifa "Anayetembea inchi kwa inchi atafika alipodhamiria bali anayeruka anaweza kufika anapofika lakini akafika akiwa mlemavu wa viungo"
Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutoka rumande alikoswekwa kwa kosa la kuharibu mali, Mama yake mzazi, Bi. Mariam Sepetu ameibuka na kutoa siri za mwanae kwa kudai kuwa, bintiye basi tena amerogwa kiasi cha kumfanya afanye maamuzi ambayo siyo sahihi...
Miss Ilala namba 2, mwaka 2002, Mbiki Msumi, hivi karibuni, amepigwa ndoa kwa siri, Risasi Mchanganyiko limebaini. Taarifa kutoka kwa chanzo chetu, zinadai kuwa, ndoa hiyo ilitawaliwa na usiri mzito ambapo hata marafiki na baadhi ya ndugu wa karibu hawakualikwa...
Ndoa ya msanii Juma Kiwoholo ‘Sajuki’ imeingia nuksi baada ya wapendanao hao kupata ajali mbaya siku chache kabla ya harusi yao, ambapo mpenzi wake Wastara Juma, amekatika mguu...
Umeibuka ugonjwa mpya katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ugonjwa huu unaitwa Chinese Encephalitis, ukienezwa na Mbu aitwaye AnophelenX, ni ugonjwa hatari ambao mpaka hivi sasa hauna tiba wala kinga na umekwishaua idadi ya watu elfu moja na mia mbili nchini Kongo. Taarifa ambazo CNN wametangaza muda mfupi uliopita ni kwamba tayari ugonjwa huo unavuka Ziwa Tanganyika kuingia Tanzania ambako unatarajiwa kuua idadi kubwa ya watu.
Hali hii imesababisha hofu kubwa na watu wengi wenye fedha zao wameanza kupanda ndege kuikimbia Tanzania wakiwaacha watu masikini wafe hii ni habari ya kusikitisha, hofu kubwa imetanda kila sehemu ya Tanzania. Jacob Steven ni mchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mume wa Angela na wana mtoto mmoja mzuri aitwaye Natalia ambaye kila mtu aliyemwona anahisi atakuja kuchukua hata taji la Urembo wa dunia, familia yao ni yenye furaha.
Taarifa alizoziona kwenye runinga zimemshtua sana Jacob, naye anafikiria kuondoka nchini kwenda kujificha Uingereza mpaka hali itakapotulia. Ameamua kuandika barua ya kuomba likizo, alipoimaliza tayari ni saa kumi na moja jioni, saa za kazi umekwishakupita hawezi kuiwakilisha barua yake kwa bosi mpaka siku inayofuata.
Muda huo huo anapokea simu kutoka kwa mke wake Angela ambaye anampa taarifa kuwa mtoto wao Natalia ana homa kali! Taarifa hizi zinazidi kumchanganya Jacob ambaye mara moja anaamua kwenda nyumbani, huko wanamchukua mtoto na kumpeleka hospitali ya Dk. Pandya, bingwa wa matatizo ya watoto wadogo. Jambo la kwanza ambalo daktari huyo anafanya ni kumpima Natalia joto kabla hajaendelea na mambo mengine. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
...mnamalizanaje na mpenzi wako? Uwanja wa Mahaba ni mpana sana, lengo lake likiwa moja tu, kuzungumzia mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano na mapenzi ili mwisho wa siku walio katika uhusiano waendelee kufaidi na siyo kupata machungu...