Hivi ndivyo Jahazi Morden taarab, walivyo pagawishi shoo ya kuinadi Bahati Nasibu ya Jishindie Pajero inayoendeshwa na Global Publishers ndani ya ukumbi wa Millenium Pub, Mbagala mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mpiga gitaa wa Jahazi Morden Taarab akizikoga nyoyo za mashabiki waliofurika ukumbi hapo.
Shabiki wa Jahazi 'Wana Nakshi Nakshi' akitoa uvivu katika jukwaa hilo baada ya kupandwa na mzuka.
Wafanyakazi hawa ambao husafisha mazingira walinaswa na kamera yetu Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana, wakizoa taka bila kuwa na vifaa vya kufanyia kazi hiyo kiusalama, kama vile mavazi, mabuti n.k PICHA:RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL.
Kundi la TMK Wanaume Halisi likiongozwa na Juma Kassim, ‘Sir Nature’ leo wametangaza kuzindua albam yao mpya iitwayo, ‘Tugawane umaskini’, ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Machi 20 mwaka huu. Katika uzinduzi huo kundi hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo Ferouz, Maunda Zorro na wengineo.
Sir Nature akifurahia jambo wakati wa mkutano na wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo Jijini Dar es Salaam leo.
FEROUZ NDANI YA TUGAWANE UMASKINI Mtoto wa Temeke Juma Kassim, ukipenda muite, Sir Nature, Kibra, Kiroboto, Mulah nk. (Kushoto) akiwa na mkali mwenzake Ferouz ambaye amethibitisha kusindikiza uzinduzi huo.
LUTENI KARAMA AAHIDI KUFANYA MAMBO Msanii wa TMK Wanaume Halisi, Luteni Karama, akiwapa wanahabari vionjo vipya atakavyochagiza siku hiyo.
WANAUME HALISI WAONGEZA NGUVU Katika mkutano huo Sir Nature, amemtambulisha msanii mpya wa kundi hilo aitwae KG Sun.
MABAGA FRESH AJIUNGA TMK HALISI Msanii wa Mabaga Fresh, Jumanne Shaban, maarufu kama Kubwa la maadui naye ametangaza kujiunga na kundi la TMK Wanaume Halisi.
KUNDI LA MAANGAMIZI SIKU YA UZINDIZI Hawa ni baadhi wa wasanii wanaotarajiwa kufanya makamuzi ya kufa mtu katika uzinduzi huo. PICHA:RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL.
Rais Jakaya Kikwete akiteta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mkuu wa Majeshi , Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) na Inspekta Jenerali wa Polisi , Said Mwema (wapili kulia) kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kuondoka kwenda Uingereza March 15, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watawa wa Shirika la Mabinti wa Maria Immaculate, (Daughters of Mary Immaculate) wakati alipokwenda kwenye Kituo cha kilichopo Luguluni nje kidogo ya Jiji kushiriki katika sherehe za siku ya Mwanamke, zilizoandaliwa na kituo hicho March 14, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mwanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Luiza Nyoni, akimpa pole Mkurugenzi wake Asha Baraka aliyerejea hivi karibuni akitokea nchini Uingereza huku akichechemea kwa maumivu ya mguu mara baada ya kukutana naye kwenye onesho la Bendi hiyo lililofanyika Mango Garden jijini Dar.
Asha Baraka akichechemea
Wanamuziki wa ‘Twanga’ Charles Baba (kushoto) na Kalala Junior nao wakimpa pole Asha Baraka.
Wanamuziki wa Twanga wakiwajibika jukwaani usiku wa kuamkia jana. Kutoka kulia ni Aisha Madinda, Luiza Nyoni na Kalala Junior.
Baada ya kutangazwa kuwa Bendi ya DDC Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde ngoma ya ukae’ imekufa, viongozi wa bendi hiyo leo alfajiri wamewashutumu wanaowatangazia hivyo na kufafanua kwamba, katika bendi hiyo lililoondelewa ni neno DDC, baada ya shirika hilo kujitoa lakini kila kitu kinaendelea kama kawaida. Pichani mwanamama akimnong’oneza jambo mwanamuziki wa bendi hiyo Hassan Bitchuka katika onesho lililofanyika katika Ukumbi wa DDC Kariakoo jana usiku.
Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini Shaaban Dede akiserebuka mbele ya mmoja wa wanenguaji wa bendi hiyo.
Mnenguaji wa bendi ya Akudo Impact Chips Kuku akicheza kwa madaha mbele ya mtangazaji maarufu Ben Kinyaiya katika Bonanza la Bendi hiyo lililofanyika ufukwe wa Msasani Club.
Bendi ya TOT Respect nayo leo alfajiri ilinaswa ikifanya makamuzi kama anavyoonekana pichani mnenguaji mahiri wa bendi hiyo Otilia Boniface akiongoza safu ya ushambuliaji. PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/ GPL
Ishu ya wawekezaji wa Kichina kuanzisha duka la ngono Mikocheni, Dar es Salaam imechukuliwa ‘vere sirias’ na Jeshi la Polisi na sasa ‘faili’ la kesi yao limetinga Uhamiaji...
Msanii wa maigizo na filamu nchini, Tamlina Mohammed Poshi maarufu Amanda, anadaiwa kufanya ‘mapinduzi’ kwenye ndoa ya mmiliki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka kwa kumchukua aliyekuwa mumewe, Khamis Bwela na wanatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni, Ijumaa Wikienda limeinyaka...
Wakili maarufu jijini James Ngalo, mkewe Rachel na mtoto wao pacha mmoja Dana wameuawa kikatili nyumbani kwao Oysterbay na mtu asiyejulikana. Kwa bahati nzuri mtoto wao mwingine Dona akiwa chumbani anasikia purukushani sebuleni na kuamua kutoka. Sebuleni anamwona mtu aliyeshika bastola mkononi huku baba, mama na pacha wake Dana wakiwa chini na damu nyingi zikiwatoka.
Kwa hofu Dona anakimbia kwenda kujificha lakini muuaji anasikia vishindo na kuamua kufuatilia chumbani, anasambaratisha kabati akitumai mtu huyo yupo ndani yake. Ni nafasi hiyo Dona anaitumia kutoka nje na kukimbia kujificha katikati ya migomba, muda mfupi baadaye anaona tochi ikimulika kwenda eneo alilojificha. Maneno pekee yanayomtoka mdomoni ni ‘Ee Mungu nisaidie’
Dona anafanikiwa kutoka nje na kukimbilia kwa jirani anayeitwa Ndunguru ambaye anajitolea kumsaidia kumficha anamchukua mpaka shambani kwake akimwacha hapo kwa ahadi ya kurejea kuja kumwangalia. Ndunguru akiwa njiani kwenda hospitali kumwangalia mkewe ambaye ni mgonjwa wa figo anasikia tangazo kwenye redio linalotangazwa na Jeshi la Polisi juu ya mtu yeyote atakayefanikiwa kumpata mtoto Dona atapewa kitita cha shilingi milioni kumi. Moyoni anaumia hajui nini cha kufanya amwokoe Dona ili mke wake apone au amwache Dona ili mkewe afe? Ni swali gumu lakini mwisho kabisa huku moyo ukimuuma anaamua kumsaliti Dona kwa Jeshi la polisi bila kujua nini madhumuni ya jeshi hilo. Je, Atawapeleka? Je, watamkuta Dona shambani? SONGA NAYO…
Uzima wa afya nilionao ni majaliwa ya Mola. Namshukuru kwa kuwa yeye ndiye kila kitu katika mzingo wa maisha yangu. Zilipita sekunde mara dakika, baadaye saa na siku, sasa ni wiki nyingine ndani ya XXL, Anti Samah nakualika kwa mara nyingine...
Zubeda Ruvanga, mwanamke mwenye umri wa miaka 38, anasimulia mateso aliyokumbana nayo tangu akiwa mtoto. Wachawi walianza kumpa tabu za maisha tangu akiwa darasa la tatu kwenye Shule ya Msingi Mwandiga Kigoma. Wiki iliyopita alikomea pale alipokuwa makaburini na Sikuzani ambaye alikuwa akimuonesha mambo mbalimbali ya kichawi, ikiwemo kumtoa maiti kaburini na kumuweka juu ya kaburi bila kulichimba. Endelea kusoma sehemu ya pili ya mkasa huu wa kusikitisha...
Hatimaye hujuma nzito iliyofanywa na Mabingwa wa Afrika, Timu ya Al Ahly ya Misri, jana ilisababisha Yanga kuchapwa mabao 3-0, kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika uliopigwa katika Uwanja wa Cairo...
HUKU leo ikishuka katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuvaana na Moro United kwenye kinyang’anyiro cha Ligi Kuu ya Vodacom, Kocha Mkuu wa Timu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri,(pichani) amekatishwa tamaa na safu yake ya ulinzi kutokana na kucheza chini ya kiwango wiki iliyopita...
Usajili wa mchezaji Boniface Ambani kwenda kucheza katika Timu ya Zhejiang Greentown FG ya China huenda ukawa kama ulivyoshindikana ule wa mwenzake Mrisho Ngassa, aliyetakiwa na Klabu ya Lov-Ham ya Norway baada ya kudaiwa kuwa Mfadhili Mkuu, Yusuf Manji ameikataa 'ofa' ya Wachina hao...
Miongoni mwa watoto aliokutana nao kwenye shule hiyo, tena kwenye darasa lake ni Edward, huyu ni mtoto wa mfanyabiashara aitwaye Lonjino ambaye kwake fedha ni kila kitu! Mtoto huyu amelelewa katika mazingira ya fedha, mazungumzo nyumbani kwao kila siku yanahusu fedha na wazazi wake kumwambia kabisa akikua ni lazima atafute utajiri na mbegu hiyo imepandikizwa ndani ya kichwa cha Edward.
Mtoto mwingine ambaye Adrian amekutana naye kwenye darasa lake ni Paul Kitumbi, pia mtoto wa tajiri, naye fedha maishani mwake ni kila kitu, anafahamu amekuja shuleni kusoma ili akimaliza Chuo Kikuu arejee nyumbani kusimamia shughuli za baba yake kwani yeye pekee ndiye mtoto wa kiume kwenye familia hiyo!
Adrian amezungukwa na matajiri, anajisikia mnyonge mbele ya wenzake na hana rafiki hata mmoja, ni aidha anatengwa au anajitenga mwenyewe. Hii inamfanya kila siku awakumbuke mama na dada yake Adventina aliowaacha kwenye dhiki kubwa, anaapa kusoma mpaka afanikiwe na kuikomboa familia yake. Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…