arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 20.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» Aina 10 ya vyakula vinavyoo ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» Mwanafunzi apata kipigo ...
» LYATOYA ASHUKA KUTOKA J ...
» Mama Salma Kikwete: ATO ...
» MPIGIE KURA AMANDA
» Jalada la e.p.a - 46
» Pinda ahamasisha kilimo ...
» MKUTANO MKUU SIMBA WATI ...

 

NIMERUDI MZEE

photos  
NIMERUDI MZEE
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mshauri wake wa Masuala a Siasa, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, baada ya kupokelewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, akitokea London Uingereza March 18, 2009.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    (20 March 2009)
Views: 405 | Maoni (3) |

 

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0

photos  
Timu ya Uwazi Giant, inayoshiriki michuano ya NSSF, imetoa onyo kwa timu nyingine katika michuano hiyo baada ya kuishushia gharika ya mabao 10-0 timu ya IPP, katika mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Sigara Chang’ombe.

Mabao ya Uwazi Giant, yalipachikwa na mshambuliaji hatari Julius Kihampa, Festo Anan na Nuru James.
Kipigo hicho cha mwaka kilisabisha Kocha wa IPP Sebo, kuingia mitini kabla ya mchezo huo kumalizika na alipoulizwa kulikoni alikana kuifahamu IPP na kusema kuwa iliyokuwa inacheza si timu yake.

Kichapo hicho cha aibu kwa timu ya IPP, kiliwafanya wachezaji wake mahili kama Maulid Baraka Kitenge, Jimmy Charles na wengine wengi kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha.

Naye mkurugenzi wa Global Publishers ambaye ndiye mdhamini mkuu wa Uwazi Giant, Eric Shigongo alisema kuwa kama vijana wake watatwaa kombe hilo atatoa zaidi kiasi cha shilingi milioni mbili na nusu zinazotolewa na mdhamini wa mashindano hayo yaani NSSF, ambacho aliahidi kutoa hapo awali.


Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Kikosi cha Uwazi Giants, kikijiandaa kuvaana na IPP FC jana.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Kikosi cha IPP FC, wakiwa katika ukaguzi kabla ya kuvaa na Uwazi Giants, katika Uwanja wa TCC Chang’ombe jana.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Uwazi Giants wakimalizia hatua ya ukaguzi mbele ya mmoja wa wana kamati ya mashindano ya NSSF Cup, Taji Liundi (mwenye miwani).

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Wachezaji wa IPP FC (wenye jezi za njano) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Uwazi Giants, mara baada ya kumalizika kwa pambano lao jana.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Benchi la wachezaji wa akiba wa Uwazi Giants wakifuatilia kwa makini mpambano huo.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Mlinzi wa pembeni wa Uwazi Giants, Elius Kambili akitolewa nje mara baada ya kuchezewa rafu.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Mpiga picha wa Global Publishers, Issa Mnally akishangilia kwa furaha ushindi wa timu yao.

Uwazi Giant yaiadhibu IPP 10-0
Mpiga picha wa IPP, akiwa amechoshwa na magoli waliyofungwa timu yao ya IPP FC.
PICHA: MUSA MATEJA NA ISSA MNALLY /GPL
    (20 March 2009)
Views: 226 | Maoni (0) |

 

KANDA BONGOMAN: Kama nina mtoto nje ya ndoa ni bahati mbaya

ijumaa  
KANDA BONGOMAN: Kama nina mtoto nje ya ndoa ni bahati mbaya

Amani iwe kwenu wapenzi wasomaji wa gazeti hili pendwa la Ijumaa, bado tunaendelea kukutana katika kona hii ya Maswali 10 (Ten Questions) yanayowahusu watu maarufu katika kada mbalimbali...
    (20 March 2009)
Views: 798 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

GROUP SEX

ijumaa  
GROUP SEX
Na Waandishi Wetu

Katika kile kinachoonekana kwamba maadili yameporomoka, wanawake watatu (pichani mbele), wakazi wa Msasani, jijini Dar es Salaam wamebainika kuwa wanaendesha maisha yao mjini kwa kufanya mapenzi kwa wakati mmoja na mwanaume mmoja (group sex)...
    (20 March 2009)
Views: 8276 | Maoni (34) | Soma Zaidi

 

PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA

ijumaa  
PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA
Na Waandishi Wetu

Galacha wa kutiririka mistari ya Kwaya nchini, Kapteni John Damian Komba inadaiwa kuwa hivi sasa hatulii, presha ikipanda na kushuka kutokana na skendo kadhaa zinazomuandama...
    (20 March 2009)
Views: 3027 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

SILENT FOREVER (14)

hadithi za Shigongo  
Wakili maarufu jijini James Ngalo, mkewe Rachel na mtoto wao pacha mmoja Dana wameuawa kikatili nyumbani kwao Oysterbay na mtu asiyejulikana. Kwa bahati nzuri mtoto wao mwingine Dona akiwa chumbani anasikia purukushani sebuleni na kuamua kutoka. Sebuleni anamwona mtu aliyeshika bastola mkononi huku baba, mama na pacha wake Dana wakiwa chini na damu nyingi zikiwatoka.

Kwa hofu Dona anakimbia kwenda kujificha lakini muuaji anasikia vishindo na kuamua kufuatilia chumbani, anasambaratisha kabati akitumaini mtu huyo yupo ndani yake. Ni nafasi hiyo Dona anaitumia kutoka kutoka nje na kukimbia kujificha katikati ya migomba, muda mfupi baadaye anaona tochi ikimulika kwenda eneo alilojificha. Maneno pekee yanayomtoka mdomoni ni ‘Ee Mungu nisaidie.’

Dona anafanikiwa kutoka nje na kukimbilia kwa jirani anayeitwa Ndunguru ambaye anajitolea kumsaidia kumficha anamchukua mpaka shambani kwake akimwacha hapo kwa ahadi ya kurejea kuja kumwangalia. Ndunguru akiwa njiani kwenda hospitali kumwangalia mkewe ambaye ni mgonjwa wa figo anasikia tangazo kwenye redio linalotangazwa na Jeshi la Polisi juu ya mtu yeyote atakayefanikiwa kumpata mtoto Dona atapewa kitita cha shilingi milioni kumi.

Moyoni anaumia hajui nini cha kufanya amwokoe Dona ili mke wake apone au amwache Dona ili mkewe afe? Ni swali gumu lakini mwisho kabisa huku moyo ukimuuma anaamua kumsaliti Dona kwa Jeshi la Polisi bila kujua nini madhumuni ya jeshi hilo. Je, atawapeleka? Je, watamkuta Dona shambani? SONGA NAYO…
    (20 March 2009)
Views: 1013 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Ndoa kudumu au kubomoka, muamuzi ni wewe!

Mahaba  
 Ndoa kudumu au kubomoka, muamuzi ni wewe!

Nina furaha sana, maana Mungu wangu wa Mbinguni yupo pamoja nami. Nikukaribishe kwa mara nyingine katika safu yetu pendwa ambayo inazungumzia mambo mbalimbali yahusuyo haya mahusiano yetu ambayo kiukweli kama tusipoyazungumzia, basi kila kukicha kutakuwa hakuishi matatizo...
    (20 March 2009)
Views: 1399 | Maoni (7) | Soma Zaidi

 

Wachezaji Yanga wamsuta Kondic

champion ijumaa  
Wachezaji Yanga wamsuta Kondic
Na Shufaa Lyimo

Licha ya ushindi wa bao 1- 0 iliyoupata dhidi ya Timu ya Polisi Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, lakini Wachezaji wa Timu ya Yanga wamemsuta Kocha Dusan Kondic kwa kusema kuwa alitaka wafungwe hata kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati yao na Al Ahly kuanza...
    (20 March 2009)
Views: 534 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Ambani alilia penalti yake Misri

champion  
Na Mwandishi Wetu

WAKATI mashabiki na wapenzi wa Yanga wakiwa bado na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Machi 15, mwaka huu , mshambuliaji wake Boniface Ambani amesema alinyimwa penati ya wazi na mwamuzi...
    (20 March 2009)
Views: 311 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Simba mambo safi

---  
Na Mwandishi Wetu

USHINDI wa mabao 2-1 dhidi ya Moro United uliweza kuamsha furaha kwa kocha Patrick Phiri aliyethubutu kusema 'simba sasa mambo sawa',..
    (20 March 2009)
Views: 250 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jalada la E.P.A -12

hadithi za Shigongo  
Marafiki watatu Adrian, Paul na Edward wanakubaliana kwa pamoja kuwa na ndoto moja ya kuikomboa nchi ya Utaiman kutoka mikononi Wanasiasa wezi wanaoiba kila kitu na kujitajirisha huku wakiwaacha wananchi walio wengi wakiteseka kwa umasikini wa kutupwa! Vijana hawa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taiman, wanatoka familia zenye uwezo tofauti.

Adrian anatoka familia fukara ambako mama yake ambaye ni mjane alimfundisha kwamba kiini cha Maovu yote ni kupenda fedha, kwake utajiri si kitu muhimu na anakiona dhambi! Paul na Edward wanatoka familia tajiri, ambako wazazi wao waliwafundisha kwamba, maisha bila fedha hayakuwa na maana yoyote hivyo ilikuwa ni lazima maishani mwao wafanye kila kilichowezekana kujilimbikizia utajiri! Ni vijana watoto wenye ndoto moja lakini akilini mwao wakiwa na mawazo tofauti juu ya utajiri.

Wakiwa Chuo Kikuu Adrian anapata rafiki wa kike aitwaye Bernadetha, ni msichana mrembo kweli kweli, mwanafunzi wa Chuo Kikuu pia lakini upande wa Udaktari wa Binadamu! Kwa tamaa zake Edward anamtamani mpenzi wa rafiki yake na kumshawishi mpaka wakaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi uliofanyika kwa siri kubwa bila Adrian kufahamu.

Jambo hili likaendelea mpaka Edward, Paul na Adrian walipomaliza Chuo Kikuu na kumwacha Bernadetha akiendelea na masomo. Adrian akaajiriwa na Chuo kama Mhadhiri na Edward na Paul wakajiunga na Chuo Cha Sayansi ya Jamii ambako walisoma Mambo ya Uhusiano wa Kimataifa na baadaye kupelekwa kwenye Balozi za Taiman nchini Canada na Uingereza, waliporejea nchini waliajiriwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na baadaye ndipo Edward akakutana tena na Bernadetha ambaye hivi sasa ameajiriwa na shirika la PSI na kuamua kurejesha penzi lao.

Kwa mara ya kwanza Edward anamfuata Bernadetha mjini Kigomo alipokwenda kikazi, wanapanga katika hoteli moja, usiku mzima wanakumbushana mambo ya zamani na kulipokucha walianza kupanga mipango ya maisha, Edward akimshawishi Bernadetha aachane na Adrian ili yeye ndiye amuoe.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (20 March 2009)
Views: 634 | Maoni (6) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com