arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 21.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» Kondic, nyota saba kuik ...
» Msanii Jumba la dhahabu ...
» SHEREHE ZA MAULID KUFAN ...
» MIZIMU YANGU (MY GHOSTS ...
» ALAANIWE YEYOTE ANAYEPA ...
» Chinjachinja ya Simba l ...
» Mtawa kizimbani, adaiwa ...

 

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI

photos  
Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassimu,’Nature’ na Ferouz Mrisho, ‘Ferouz’ usiku wa kuamkia leo wamekonga nyoyo za wanazi wa burudani jijini Dar es Salaam, baada ya kutwanga shoo kali ya uzinduzi wa albamu zao mbili, ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.Albamu ya Nature inaitwa ‘Tugawane umasikini’ ambapo albamu ya Ferouz inaitwa ‘Sauti na vyombo’.

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI
Nature akikonga nyoyo za mashabiki.

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI
Ferouz akiwapagawisha mashabiki,hapa anaimba wimbo wake wa Mr.Police man.

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI
Enika alisindikiza shoo hiyo,hata hivyo kivazi chake kilionekana kuwazingua wengi.

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI
Mbunge wa Temeke Abass Mtemvu, akiwa na mbunge wa viti maalum Bi. Al-Shaimaa Kwegyir, ambao walikuwa wageni rasmi katika shoo hiyo.

JUMA NATURE ALIVYOGAWANA NA WABONGO UMASIKINI
Mtangazaji mahiri wa Redio Times FM, Tayana Amri, akiwa na msanii Mbungangari Lameck, ‘Pig Black’, wakifuatilia kwa karibu makamuzi ya TMK Wanaume halisi.
PICHA :CHRISTOPHER LISSA/GPL
    (21 March 2009)
Views: 643 | Maoni (7) |

 

KANDA BONGOMAN ANADI BAHATI NASIBU YA JISHINDIE PAJERO.

photos  
Jana jioni wakazi wa jiji la Dar es Salaam, walishuhudia mwanamuziki mkongwe kutoka nchini DRC Kongo, aishie nchini Uingereza, Kanda Bongoman, akifanya makamuzi ya kufa mtu ambayo yalienda sambamba na kuinadi bahati Nasibu ya Jishindie Pajero, ndani ya Ukumbi wa Msasani Club.
Mwanamuziki huyo leo anatarajiwa kufanya onesho lingine mkoani Morogoro.

KANDA BONGOMAN ANADI BAHATI NASIBU YA JISHINDIE PAJERO.
Kanda Bongoman na wanenguaji wake wakifanya makamuzi wakati wakiitanagaza Bahati Nasibu hiyo

KAMA HANA MFUPA
KANDA BONGOMAN ANADI BAHATI NASIBU YA JISHINDIE PAJERO.
Bongoman akijinyonganyonga jukwaani katika kuwakumbusha mashabiki wake mambo ya enzi hizo.

HAKUHOFIA VIBAKA ALIJICHANGANYA NA MASHABIKI
KANDA BONGOMAN ANADI BAHATI NASIBU YA JISHINDIE PAJERO.
Baada ya kuona mashabiki wamepandwa na mzuka Bongoman aliamua kujumuika nao.

ILIKUWA NI KUJIRUSHA TU
KANDA BONGOMAN ANADI BAHATI NASIBU YA JISHINDIE PAJERO.
Umati wa watu ukijimwaga katika onesho hilo.
PICHA: RICHARD BUKOS /GPL.
    (21 March 2009)
Views: 411 | Maoni (2) |

 

MANGE ACHEZEA KICHAPO

risasi jumamosi  
MANGE ACHEZEA KICHAPO
Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Miss na muandaaji wa mashindano ya ma-miss hapa nchini siku za nyuma, Mange Kimambi ‘MK’, amechezea kichapo, baada ya kudaiwa kuwachafua vigogo katika mtandao aliokuwa akiumiliki wa www.mangeblogspot.com, kabla ya kuufunga....
    (21 March 2009)
Views: 2356 | Maoni (14) | Soma Zaidi

 

SHIGONGO AMSAMBARATISHA MENGI

risasi jumamosi  
Na Rhobi Chacha
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, inayochapisha magazeti pendwa ya Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani na Championi, Eric James Shigongo, amemsambaratisha Mkurugenzi wa IPP, Reginal Mengi, baada ya timu yake ya Uwazi Giants kuichabanga timu ya mtani wake huyo kwa bao 10-0, katika mechi kali ndani ya Viwanja vya Sigara TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam juzi (Alhamis)....
    (21 March 2009)
Views: 656 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Mabadiliko gerezani

risasi jumamosi  
Mabadiliko gerezani

Christopher Lissa na Richard Bukos
Khadija Seleman ambaye ni mama mzazi wa Ramadhani Seleman ‘Rama mlawatu’ ambao kwa pamoja wanakabiliwa na shitaka la mauaji, ambapo Ramadhani alikamatwa maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam akila kichwa cha mtoto, imeonekana ugali wa dona katika gereza la Segerea, umemkubali kutokana na mabadiliko makubwa aliyonayo kutoka uraiani hadi sehemu hiyo baada ya kuzidi kunenepeana ovyo tofauti na alivyoingia mahabusu....
    (21 March 2009)
Views: 987 | Maoni (3) | Soma Zaidi

 

LIYUMBA ABADILISHIWA HAKIMU, ISHU YAKE BADO MBICHI

risasi jumamosi  
Richard Bukos na Christopher Lissa
Kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na mwenzake, Deus Kweka jana (Ijumaa), iliingia hatua mpya baada ya kupatiwa Hakimu mwingine kufuatia Hakimu aliyekuwa akiindesha kesi hiyo Bi. Hadija Msongo, kujitoa katika kesi hiyo...
    (21 March 2009)
Views: 385 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

MSITU WA PANDE-6

hadithi za Shigongo  
Umeibuka ugonjwa mpya katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ugonjwa huu unaitwa Chinese Encephalitis, ukienezwa na Mbu aitwaye AnophelenX, ni ugonjwa hatari ambao mpaka hivi sasa hauna tiba wala kinga na umekwishaua idadi ya watu elfu moja na mia mbili nchini Kongo. Taarifa ambazo CNN wametangaza muda mfupi uliopita ni kwamba tayari ugonjwa huo unavuka Ziwa Tanganyika kuingia Tanzania ambako unatarajiwa kuua idadi kubwa ya watu.

Hali hii imesababisha hofu kubwa na watu wengi wenye fedha zao wameanza kupanda ndege kuikimbia Tanzania wakiwaacha watu masikini wafe hii ni habari ya kusikitisha, hofu kubwa imetanda kila sehemu ya Tanzania. Jacob Steven ni mchumi wa Jiji la Dar es Salaam, mume wa Angela na wana mtoto mmoja mzuri aitwaye Natalia ambaye kila mtu aliyemwona anahisi atakuja kuchukua hata taji la Urembo wa dunia, familia yao ni yenye furaha.

Taarifa alizoziona kwenye runinga zimemshtua sana Jacob, naye anafikiria kuondoka nchini kwenda kujificha Uingereza mpaka hali itakapotulia. Ameamua kuandika barua ya kuomba likizo, alipoimaliza tayari ni saa kumi na moja jioni, saa za kazi umekwishakupita hawezi kuiwakilisha barua yake kwa bosi mpaka siku inayofuata.

Muda huo huo anapokea simu kutoka kwa mke wake Angela ambaye anampa taarifa kuwa mtoto wao Natalia ana homa kali! Taarifa hizi zinazidi kumchanganya Jacob ambaye mara moja anaamua kwenda nyumbani, huko wanamchukua mtoto na kumpeleka hospitali ya Dk. Pandya, bingwa wa matatizo ya watoto wadogo. Jambo la kwanza ambalo daktari huyo anafanya ni kumpima Natalia joto kabla hajaendelea na mambo mengine.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (21 March 2009)
Views: 800 | Maoni (7) | Soma Zaidi

 

Kupoteza hisia za mapenzi tatizo sugu linalowatesa wengi kimya kimya

Mahaba  
Uwanja wa Huba ipo tena hewani na anayekuandalia safu hii namba moja ihusuyo mambo ya mapenzi ni mimi Joseph Shaluwa, nikikukaribisha kwa moyo mkunjufu ili kujifunza mbinu mpya za mapenzi.....
    (21 March 2009)
Views: 464 | Maoni (1) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com