Global Publishers jana ilisherehekea kutimiza miaka 11 tangu kuzaliwa kwake, ambapo sherehe hizo zilifanyika kwa staili ya ‘kujiachia’ katika Ufukwe wa Chadibwa Resort, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, picha zinakupa dokezo la jinsi ishu ilivyokuwa:

Baadhi ya ‘members’ wa Global wakibadilishana mawazo huku wakipata ‘kilaji’ ‘kufresh mind’ baada ya kazi ngumu za kila siku.

Hawa nao ni baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakipunga upepo na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali ufukweni hapo.

..kila mtu alijiachia kivyake

Wakati shamrashamra hizo zikiendelea, muda wa maakuli ulifika na wachapakazi wa Global Publishers, wakiongozwa na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Championi Jumatatu, Philip Nkini, walianza kupata misosi ya nguvu.

...Bosi Mrisho(kati) akitoa maelekezo kwa DJ ya kutoa burudani ya uhakika kwa 'vijana wake'

Baada ya kuogelea, kula na kunywa, uliwadia muda wa kujimwaga 'uwanjani'.

Vichekesho navyo vilikuwepo kutoka kwa vijana wanaojiita “Komedy” ili ‘kulegeza’ kidogo mbavu za wafanyakazi hao baada ya kazi kubwa ya kila siku ya kuhabarisha jamii.