Hoteli tatu za kitalii za Paradise Holiday Resort (pichani juu), Oceanic View na Livingstone zilizoko mjini Bagamoyo, ambazo ziko katika ukanda wa hoteli za kitalii, zimeungua kwa moto.
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Redio One ya jijini Dar es Salaam iliyosomwa saa saba mchana, hoteli Paradise ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuungua ikifuatiwa na zile za Oceanic na Livingstone. Hali hiyo ilichangiwa na mvumo wa upepo wa bahari ambao ulieneza moto katika eneo hilo na hivyo kusambaa katika hoteli hizo. Paradise Hotel ni hotel maarufu mjini humo na mwaka jana washiriki wa shindano la kumtafuta malkia wa ulimbwende nchini, Miss Tanzania, wote waliweka kambi hapo.
UONGOZI wa Kampuni ya AFRICA MEDIA GROUP LTD, wamiliki wa Kituo cha Televisheni cha CHANNEL TEN na RADIO MAGIC FM, unapenda kuwaarifu wananchi wote kwa ujumla kuwa kuanzia sasa wanaweza kuyapata matangazo ya CHANNEL TEN kupitia SATELAITI ya INTELSAT 906 64E. MASAFA ya 3905.63MHZ, Symbol Rate 2.84835Msps na FEC 2/3 LHCP.
Aidha kwa sasa wanaweza pia kuyapata matangazo ya Radio MAGIC FM kupitia kwenye Satelaiti hiyo hiyo ya INTELSAT 906 64E. MASAFA ya 3905.63MHZ, Symbol Rate 2.84835Msps na FEC 2/3 LHCP.
Taarifa hii inawahusu wale tu wanaotumia Satelaiti Dish kupata matangazo ya CHANNEL TEN na RADIO MAGIC FM.
Kwa wanaotumia Antena za kawaida kwa Televisheni na wasikilizaji wa Redio hakutakuwa na mabadiliko yoyote.
Kwa maelezo zaidi tuandikie barua pepe kwenda technical@amgl.co.tz au tovuti yetu ya www.chten.tv au tupigie simu kwa namba zifuatazo, 0773 299219, 0787 418031, 0713 263902.
AUGUSTINO MGANGA, MKUU IDARA YA UFUNDI, CHANNEL TEN/RADIO MAGIC FM. DAR ES SALAAM.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi vya Tanzania Fishing Crew and Allied Workwers Union (WAMEUTA) na Tanzania Sea Feavers Workers Union (TASU) baada ya kuzungumza nao , Ofisini kwake jijni Dar es salaam March 20, 2009.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana , Profesa Juma Kapuya baada ya kikao kati yake na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam, March 20, 2009. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Akina dada watatu walionaswa hivi karibuni wakifanya mapenzi ya kikundi (Group Sex), wanashutumiwa kwamba tabia hiyo ni hatarishi dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU)...
Aliyekuwa Mnenguaji wa bendi mbalimbali nchini na mzazi mwenzake Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Monica ‘Diana Aston Villa’ yuko taabani kitandani akisumbuliwa na Ugonjwa wa Kifua Kikuu ‘TB’ ambao umemmaliza kiafya na kukosa nguvu...
Baada ya kuishi msituni muda mrefu na bibi Monica Lugembe, aliyekimbia kijijini kwake sababu ya tuhuma za uchawi, Dona anaamua kurejea jijini Dar es Salaam baada ya bibi huyo kufariki dunia na yeye peke yake akamzika. Ametembea kwa miguu umbali mrefu mno, ilikuwa safari ya siku mbili kutoka porini mpaka katikati ya jiji na kwenda moja kwa moja hadi eneo la Kivukoni ambako watoto wengi wa mtaani wanaishi! Anachagua sehemu moja ufukweni na kulala mpaka asubuhi siku iliyofuata alipozinduka na kujikuta amelala karibu na kundi kubwa la watu wenye kelele, akagundua lilikuwa ni soko la samaki na hakuna mtu aliyeonekana kumjali! Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
Siku hazisimami, daima zinasonga mbele kwa mbele. Mungu ambaye ndiye mfalme wa kila kilichomo mbinguni na ardhini, anawezesha mabadiliko ya kutisha ndani ya sayari ya dunia. Hakukosea Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ alipoimba Siku Hazigandi...
Zubeda Ruvanga, mwanamke mwenye umri wa miaka 38, anasimulia mateso aliyokumbana nayo tangu akiwa mtoto. Wachawi walianza kumpa tabu za maisha tangu akiwa darasa la tatu kwenye Shule ya Msingi Mwandiga Kigoma. Wiki iliyopita alikomea pale alipokuwa anamkabidhi Mfalme Dajani kifurushi chenye nyama za binadamu ambazo walizichukua na Sikuzani kutoka moja ya maiti waliomfukua kaburini. Endelea kusoma...
KLABU ya Yanga imepata pigo zito, baada ya beki wao wa kutumainiwa, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ na Kiungo, Abdi Kassim ‘Babi’, kuripotiwa kukaa nje ya dimba kwa muda kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kiafya, hivyo kuanza kwa kuikosa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Toto Africans kesho...
KATIKA kuhakikisha anakilinda kipaji cha mshambuliaji wake na Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi, Kocha Mkuu wa Timu ya soka ya Simba, Mzambia Patrick Phiri, amepanga kumweka kitako mpachika mabao huyo anayewika kwa sasa...
Timu ya Simba, imeweka hatarini tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani, baada ya jana kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro...
Marafiki watatu Adrian, Paul na Edward wanakubaliana kwa pamoja kuwa na ndoto moja ya kuikomboa nchi ya Utaiman kutoka mikononi mwa Wanasiasa wezi wanaoiba kila kitu na kujitajirisha huku wakiwaacha wananchi walio wengi wakiteseka kwa umasikini wa kutupwa! Vijana hawa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taiman, wanatoka familia zenye uwezo tofauti.
Adrian anatoka familia fukara ambako mama yake ambaye ni mjane alimfundisha kwamba kiini cha maovu yote ni kupenda fedha; kwake utajiri si kitu muhimu na anakiona dhambi! Paul na Edward wanatoka familia tajiri, ambako wazazi wao waliwafundisha kwamba maisha bila fedha hayakuwa na maana yoyote hivyo ilikuwa ni lazima maishani mwao wafanye kila kilichowezekana kujilimbikizia utajiri! Ni vijana watoto wenye ndoto moja lakini akilini mwao wakiwa na mawazo tofauti juu ya utajiri.
Wakiwa Chuo Kikuu, Adrian anapata rafiki wa kike aitwaye Bernadetha, ni msichana mrembo kweli kweli, mwanafunzi wa Chuo Kikuu pia lakini upande wa udaktari wa binadamu! Kwa tamaa zake Edward anamtamani mpenzi wa rafiki yake na kumshawishi mpaka wakaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi uliofanyika kwa siri kubwa bila Adrian kufahamu.
Jambo hili likaendelea mpaka Edward, Paul na Adrian walipomaliza Chuo Kikuu na kumwacha Bernadetha akiendelea na masomo. Adrian akaajiriwa na Chuo kama Mhadhiri na Edward na Paul wakajiunga na Chuo cha Sayansi ya Jamii ambako walisoma mambo ya Uhusiano wa Kimataifa na baadaye kupelekwa kwenye balozi za Taiman nchini Kanada na Uingereza.Waliporejea nchini waliajiriwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na baadaye ndipo Edward akakutana tena na Bernadetha ambaye hivi sasa ameajiriwa na shirika la PSI na kuamua kurejesha penzi lao.
Kwa mara ya kwanza Edward anamfuata Bernadetha mjini Kigomo alikokwenda kikazi na wanapanga katika hoteli moja, usiku mzima wanakumbushana mambo ya zamani na kulipokucha walianza kupanga mipango ya maisha. Edward akimshawishi Bernadetha aachane na Adrian ili yeye ndiye amuoe. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…