arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 25.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» ZITO LAIBUKA
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» GLOBAL PUBLISHERS MUSIC PLA ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Mwisho wa dunia
» FROM CHINA WITH TRUE LO ...
» ANGALIA KWA MAKINI!!
» Mke wangu mtarajiwa- 13
» THE LAST HOPE (tumaini ...
» Maximo ataja 20 wa kuiu ...
» MY HEART IS BLEEDING (M ...

 

PINDA ATEMBELEA NYUMBU

photos  
PINDA ATEMBELEA NYUMBU
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride la kumkaribisha kwenye Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Nyumbu na Shirika la Nyumbu (TATC) mkoani Pwani wakati alipotembelea eneo hilo March 25, 2009.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
    (25 March 2009)
Views: 263 | Maoni (0) |

 

JK AONDOKA KWENDA VISIWA VYA COMORO

photos  
JK AONDOKA KWENDA VISIWA VYA COMORO
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais, Dr, Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, waliomsindikiza kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salam, wakati alipoondoka nchini kwenda Visiwa vya Comoro kwa ziara March 24, 2009. Kushoto kwake ni mkewe Mama Salma.

JK AONDOKA KWENDA VISIWA VYA COMORO
Rais Jakaya Kikwete akiagana na Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kundoka March 24, 2009, kwenda Visiwa vya Comoro kwa ziara.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
    (25 March 2009)
Views: 317 | Maoni (2) |

 

UWAZI FC YATOA KICHAPO KWA FREE MEDIA.

photos  
Timu ya soka inayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Championi na Ijumaa wikienda, Uwazi Fc jana ilitoa kipigo cha Mbwa mwizi, kwa timu ya Free Media, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, kwa magoli matatu kwa mbili, katika michuano ya NSSF inayoendelea katika viwanja vya TCC Chang’ombe.


UWAZI FC YATOA KICHAPO KWA FREE MEDIA.
Timu ya soka ya Uwazi FC, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuiadhibu timu ya Free Media kwa magoli 3-2.

UWAZI FC YATOA KICHAPO KWA FREE MEDIA.
Mwanamuziki mahiri wa kizazi kipya Juma Nature, akiikagua timu ya Uwazi FC, kabla ya kushuudia timu hiyo ikitoa kipigo kwa Free Media.

UWAZI FC YATOA KICHAPO KWA FREE MEDIA.
Wachezaji wa uwazi Fc, wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao wakati wa mapumziko.

UWAZI FC YATOA KICHAPO KWA FREE MEDIA.
Waandishi wa Global Publishers, wakiongozwa na Mpiga picha mahiri Issa Mnally, aliyelala chini akikung’uta Tarumbeta mara baada ya mpira kumalizika wakiwa wamewaadhibu Free Media kwa mabao 3-2.
PICHA: CHRISTOPHER LISSA/GPL.
    (25 March 2009)
Views: 247 | Maoni (0) |

 

MCHUNGAJI, SHEKHE WASEMA MASTAA HAWA WAFANYA UZINZI

risasi mchanganyiko  
MCHUNGAJI, SHEKHE WASEMA MASTAA HAWA WAFANYA UZINZI
Na Rhobi Chacha

Kwenye meza ya gazeti hili, linaloandika habari za watu maarufu nchini, imetinga ‘ishu hoti’, ambapo mastaa wanadaiwa kuvunja amri ya sita (katika vitabu vitakatifu), inayosema usizini, kutokana na kuishi pamoja bila ya kuhalalishwa kanisani ama msikitini na katika vyombo vingine husika...
    (25 March 2009)
Views: 2169 | Maoni (10) | Soma Zaidi

 

Shigongo kumvaa Rostam leo

risasi mchanganyiko  
Na Rhobi Chacha

Timu ya Uwazi Giants ya Kampuni ya Global Publishares & General Enterprises Limited, inayochapisha magazeti pendwa ya Risasi, Championi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda iliyochini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigongo leo inatarajia kuivaa timu ya New Habari Corporation Ltd iliyochini ya Mkurugenzi wake Mtendaji, Rostam Aziz katika mchezo utakaopigwa ndani ya Viwanja wa TCC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam kuwania kutinga fainali ya michuano iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)...
    (25 March 2009)
Views: 267 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Msitu wa Pande-7

hadithi za Shigongo  
Taarifa alizoziona kwenye runinga zimemshtua sana Jacob, naye anafikiria kuondoka nchini kwenda kujificha Uingereza mpaka hali itakapotulia.

Ameamua kuandika barua ya kuomba likizo, alipoimaliza tayari ni saa kumi na moja jioni, muda wa saa za kazi umekwishakupita hawezi kuiwakilisha barua yake kwa bosi mpaka siku inayofuata.

Muda huo huo anapokea simu kutoka kwa mke wake Angela ambaye anampa taarifa kuwa mtoto wao Natalia ana homa kali! Taarifa hizi zinazidi kumchanganya Jacob ambaye mara moja anaamua kwenda nyumbani, huko wanamchukua mtoto na kumpeleka hospitali ya Dk. Pandya, bingwa wa matatizo ya watoto wadogo.

Jambo la kwanza ambalo daktari huyo anafanya ni kumpima Natalia joto kabla hajaendelea na mambo mengine.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (25 March 2009)
Views: 991 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Nataka kichwa cha mwanangu-23

Mikasa ya kusisimua  
Msomaji wangu mpenzi, wiki iliyopita uliona jinsi vijana Jamali na Jamini walivyokwenda kupunga upepo katika ufukwe wa Coco, wakiwa huko Jamini anawaona wasichana wawili warembo sana wakikimbia kando ya bahari. Kutokana na uzuri wao, anashindwa kujizuia na kumuita pacha wake Jamali aliyekuwa mita chache na kumuonyesha wasichana hao ambao uzuri wao haukuwa na mfano. Jamali naye kama ilivyokuwa kwa ndugu yake, alipowaona alipagwa na uzuri wao ambapo walikubaliana kuwatongoza ili siku hiyo watoke nao.

Kama walivyopanga, hazikupita dakika nyingi, wasichana hao waliokuwa wakikimbia walirudi na kukatiza eneo walilokuwa wamesimama Jamali na ndugu yake ndipo Jamini aliwaita na kuwatongoza ambapo warembo hao walikubali. Kwa kuwa wakati huo walikuwa wamevaa mavazi ya ufukweni, waliowaomba vijana hao wawasubiri wakabadili nguo. Waliporejea wote walipanda katika gari la akina Jamali lakini jambo la kushangaza Jamini alipotaka kuliwasha halikuwa na jambo la kustajaabisha zaidi mapacha hao walipogeuka kuangalia siti ya nyuma ambayo warembo hao walikaa, hawakuwaona. Je, nini kilitokea na wale wasichana ni akina nani? Endelea kutiririka nayo…
    (25 March 2009)
Views: 853 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Kupoteza hisia za mapenzi Kupoteza hisia za mapenzi

Mahaba  
Kupoteza hisia za mapenzi Kupoteza hisia za mapenzi

...tatizo sugu linalowatesa wengi kimya kimya-2
Karibuni sana katika safu yetu bora kabisa ya Mambo ya Uhusiano. Sina shaka kuwa wote mtakuwa wazima wa afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku...
    (25 March 2009)
Views: 765 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Yanga full shangwe

champion  
Yanga full shangwe
Mashaka Baltazar, Mwanza na Adolph Balingilaki, Dar

FULL SHANGWE! Kwa mara nyingine tena, Yanga imeandika historia ya kutwaa zaidi taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya jana kufanikiwa kufanya hivyo pale ilipofanikiwa kuichapa Toto African kwa mabao 2-1 Katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa...
    (25 March 2009)
Views: 552 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

Kaduguda atoboa siri

champion  
Na Adoph Balingilaki

SI SIRI! WAKATI Yanga ikisherehekea ubingwa, Katibu Mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda amesema pangua pangua ya makocha waliyokuwa wakiifanya ndio imewafanya kukosa kombe kwa miaka miwili mfululilizo...
    (25 March 2009)
Views: 282 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jalada la E.P.A -14

hadithi za Shigongo  
Edward, Paul na Adrian ni marafiki tangu sekondari na kwa pamoja walikubaliana kusoma ili waje wawakomboe wananchi wa Taiman kutoka mikononi mwa viongozi wagandamizaji waliowaibia na kuwafanya maskini ingawa walikuwa na rasilimali za kutosha!

Walipomaliza chuo kikuu, Paul na Edward walijiunga na chuo cha Diplomasia cha Taiman ambako walisoma mambo ya Ushirikiano wa kimataifa na baadae kutumwa kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi, waliporejea nchini miaka michache baadae waligombea ubunge kwenye majimbo yao na kupata, Rais akawateua kuwa mawaziri, Edward akiwa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Paul Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mwenzao Adrian ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Taiman, mke wake Bernadetha waliyekutana tangu chuo kikuu na Edward kumtamani sababu ya uzuri wake, ni daktari katika shirika liitwalo PSI.

Baada ya kurejea nchini, Edward alianza kumfuatilia Bernadetha, alimpenda na aliona kama hakufaa kuwa mke wa Adrian, hatimaye wakakutana na kuanza kutoka kwa siri! Penzi lilipokolea Edward akataka kuchonga mzinga, alichokifanya ni kuhakikisha Adrian anaondoka nchini, mpango ukafanyika wa kutafutiwa nafasi ya masomo nje ya nchi, akaitwa ofisini kwa mkuu wa chuo na kupewa taarifa hizo, hakuzipokea kwa furaha kwa sababu hakutaka kumwacha mke wake.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
    (25 March 2009)
Views: 834 | Maoni (5) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com