arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 27.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» JE, UNGEPENDA KUPATA RAFIKI ...
» MSHANGAO!
» Rais Kabila aomba wakafungw ...
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» dalili tatu zinazoashi ...
» Jack Pemba predicted th ...
» Watoto wa miaka 12 wawe ...
» Niliishi kuzimu miaka 2 ...
» THEA, MONALISA NANI ZAI ...
» Ukihisi au ukimfuma mpe ...
» Mrembo atupa mtoto jala ...

 

MAHARAMIA WA MAGUFULI WARUDISHWA MELINI

photos  
Sakata la kesi ya maharamia walionaswa na merini wakivua samaki aina ya Jodari katika kina kirefu ndani ya Bahari ya Hindi eneo la Tanzania kinyume cha sheria leo (Ijumaa) limechukua sura mpya baada ya Mhandisi Mkuu wa meli hiyo Cai Dong Li na Msaidizi wake, Chen Rui Hai kuachiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kurudi kwenye meli hiyo.
Upande wa utetezi katika kesi hiyo uliomba wahandisi hao waachiwe kwa muda ili wakaikoe meli hiyo iliyoko katika hatari ya kuzama baada ya njia zake za kutolea maji yanayoingia kushindwa kufanya kazi baada ya kuzimwa baada ya watuhumiwa hao kukamatwa.
Wahandisi hao watakaa melini humo mpaka kazi ya kutoa maji itakapomalizika ndipo watarudishwa tena mahabusu.

MAHARAMIA WA MAGUFULI WARUDISHWA MELINI
Baadhi ya maharamia wakisubiri kusomewa kesi inayowakabili

MAHARAMIA WA MAGUFULI WARUDISHWA MELINI
Baada ya kesi hiyo maharamia wengie walirudishwa rumande mpaka Machi 31 mwaka huu.
PICHA: RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA
    (27 March 2009)
Views: 296 | Maoni (2) |

 

KIMVUA KIDOGO MAFURIKO DAR

photos  
Mvua za rasharasha zilizonyesha kwa muda mfupi jijini Dar es Salaam leo, zimesababisha kuharibika kwa miundombinu na kusababisha baadhi ya watu kusitisha safari zao.

KIMVUA KIDOGO MAFURIKO DAR
Pichani moja ya mitaa ya maeneo ya Posta Mpya jijini Dar, ukiwa umefungwa kufuatia maji kujaa na kutiririsha kinyesi.

KIMVUA KIDOGO MAFURIKO DAR
Mtaro wa kinyesi ukiwa umezibuka eneo hilo maeneo ya Posta Mpya.

KIMVUA KIDOGO MAFURIKO DAR
Wakazi wa Jiji wakivuka kwa taabu moja ya maeneo ya jiji kufuatia maji ya mvua kufurika barabarani.
PICHA:RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA /GPL
    (27 March 2009)
Views: 247 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

MZEE YUSUF: Skendo yangu kubwa ni kuoa tu!

ijumaa  
MZEE YUSUF: Skendo yangu kubwa ni kuoa tu!

HAKUNA asiyemfahamu, nadhani kila kona ukipita iwe mjini au vijijini utakuta wimbo wake unapigwa, hasa katika makabati na vituo vya kuuzia kaseti...
    (27 March 2009)
Views: 1268 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

WEMA SI TEJA TENA

ijumaa  
WEMA SI TEJA TENA
Na Imelda Mtema

Mama mzazi wa Miss Tanzania 2005-2006. Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu amesema kuwa mwanaye amerudi nyumbani, amekuwa mtiifu kitabia na hata akili yake imenyooka...
    (27 March 2009)
Views: 2274 | Maoni (24) | Soma Zaidi

 

CHANZO MUME WA MTU

ijumaa  
CHANZO MUME WA MTU
Na Mwandishi Wetu

MUDA mfupi baada ya mtangazaji mwenye jina kubwa nchini, Khadija Shaibu a.k.a Dida kukamatwa na kufanyiwa upekuzi akituhumiwa kumeza dawa za kulevya, Ijumaa limezinyaka za ndani...
    (27 March 2009)
Views: 2496 | Maoni (17) | Soma Zaidi

 

SILENT FOREVER (16)

hadithi za Shigongo  
Baada ya kuishi msituni muda mrefu na bibi Monica Lugembe, aliyekimbia kijijini kwake sababu ya tuhuma za uchawi, Dona anaamua kurejea jijini Dar es Salaam baada ya bibi huyo kufariki dunia na yeye peke yake akamzika. Ametembea kwa miguu umbali mrefu mno, ilikuwa safari ya siku mbili kutoka porini mpaka katikati ya jiji na kwenda moja kwa moja hadi eneo la Kivukoni ambako watoto wengi wa mtaani wanaishi!

Anachagua sehemu moja ufukweni na kulala mpaka asubuhi siku iliyofuata alipozinduka na kujikuta amelala karibu na kundi kubwa la watu wenye kelele, akagundua lilikuwa ni soko la samaki na hakuna mtu aliyeonekana kumjali! Je, nini kinaendelea? SONGA NAYO…
    (27 March 2009)
Views: 930 | Maoni (6) | Soma Zaidi

 

Anakusumbua sana lakini humtaki, nini cha kufanya?

Mahaba  
Anakusumbua sana lakini humtaki, nini cha kufanya?

Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa ni yeye ndiye aliyepanga tukutane tena leo katika safu yetu hii maridhawa ya Let’s Talk About Love. Hakika bila ya yeye sisi tusingekuwepo!...
    (27 March 2009)
Views: 637 | Maoni (4) | Soma Zaidi

 

Ambani hatarini kukosa Milioni 600 za Wachina

champion ijumaa  
Ambani hatarini kukosa Milioni 600 za Wachina
Na Mwandishi Wetu

HUENDA mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, Boniface Ambani akazikosa Sh. Milioni 600 kutoka klabu ya Zhejian Greentown ya China...
    (27 March 2009)
Views: 562 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Bao la Matuta lavuruga hesabu za Phiri Simba

champion ijumaa  
Na Shufaa Lyimo

BAO lililofungwa na Omari Matuta wa Mtibwa Sugar katika dakika ya 34 dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita, limezima kabisa mahesabu makali ya Kocha Patrick Phiri wa Wekundu hao wa Msimbazi ya kugusa michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani...
    (27 March 2009)
Views: 298 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Dusan Kondic atoa promosheni Yanga

champion ijumaa  
Na Adolph Balingilaki

Wakati mashabiki na wanachama wa Yanga wakiendelea kushangilia ubingwa wa Tanzania Bara walioupata mapema wiki hii katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza mgongoni kwa 'watoto wao' Toto Afrika, Kocha Mkuu wa timu hiyo Professa Dusan Kondic amebadili mfumo wa uchezaji kwa kutoa 'promotioni' kwa wachezaji waliokuwa wanakaa benchi...
    (27 March 2009)
Views: 335 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Jalada la E.P.A -15

hadithi za Shigongo  
Vijana watatu, Edward, Paul na Adrian wanakutana shuleni na kukubaliana kwamba kwa pamoja watafanya kazi kwa kushirikiana mpaka waikomboe nchi yao kutoka mikononi mwa Wagandamizaji ambao pia ni Raia wa nchi ya ya Taiman. Wanatoka katika familia tofauti, Paul na Edward wanatoka familia tajiri ambako walifundishwa na wazazi wao kwamba ni lazima katika maisha watajirike na Adrian anatoka familia masikini ambako mama yake mjane alimfundisha kwamba kiini cha maovu yote ni kupenda fedha.

Walipomaliza Chuo Kikuu, Paul na Edward wanakuwa mawaziri na Adrian anakuwa Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Taiman akiwa na mke wake Bernadetha, waliyekutana tangu enzi za sekondari! Cha kusikitisha zaidi, Edward ambaye hivi sasa ni Waziri wa Mambo ya nchi za nje ameanza kumtamani Bernadetha na anafanikiwa kumwingiza katika mtego wa mapenzi.

Ili kupata nafasi ya kufaidi mapenzi yao, unafanyika mchoro na Adrian anapata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi, nafasi ambayo awali aliikataa kwa sababu hakutaka kumwacha mke wake lakini ni mke wake huyo huyo aliyemshawishi mpaka akakubali na kuondoka nchini kwa miezi tisa.

Amerejea bila mawasiliano, sababu mke wake alikuwa hampigii simu wala kumwandikia barua, ana wasiwasi kuna kitu kinaendelea! Nyumbani kwake anakuta gari aina ya Landcruiser limeegeshwa, lina namba za serikali! Akiwa hajapata jibu gari hilo linafanya nini nyumbani kwake usiku wa saa tano, anaamua kuzunguka nyuma ya nyumba yake na kuchungulia ndani, macho yake yanagongona na taswira za watu wawili wakifanya mapenzi kitandani kwake, hao ni Edward na Bernadetha, akiwa na hasira anarejea mlangoni na kuanza kugonga.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
    (27 March 2009)
Views: 790 | Maoni (6) | Soma Zaidi
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi


Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com