Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imewahimiza wananchi kuona umuhimu wa kutoa chanjo kwa watoto wao ili kuwakinga na magonjwa hatari yanayoweza kuwapata. Wito huo umetolewa leo na Dokta.Fatuma Mganga, mratibu wa uanzishwaji wa chanjo mpya inayoweza kuzuia magonjwa sita ambayo ni: kifaduro, Pepopunda, Donda koo, Kichomi, Uti wa mgongo na Homa ya ini, wakati alipokuwa akiwasilisha mada katika warsha iliyofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam. Pichani: Dk. Fatma Mganga akifafanua jambo katika warsha hiyo.
Mratibu wa ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo Dr. David Manyong akidadavua kiundani juu ya umuhimu wa kuwachanja watoto waliochini ya mwaka mmoja katika warsha hiyo.
Mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam huenda zikasababisha magonjwa ya milipuko ikiwa wananchi hawatazingatia usafi. Pichani, wafanyabiashara wa mbogamboga wamenaswa leo wakitandaza bidhaa zao chini katikati ya madimbwi ya maji na matope nje ya soko dogo la Kariakoo
MIUNDO MBINU MIBOVU... Hiii ndiyo hali halisi ya miundombinu ya maji machafu inavyofanya kazi jijini Dar es Salaam kiasi cha kuleta kero kubwa kwa wananchi. Pichani, mwananchi huyo alinaswa akijaribu kuzibua mfereji ili uweze kufanyakazi vizuri katika Mtaa wa Narung’ombe Kariakoo.
Soko Kuu la Kariakoo likiwa katikati ya bahari ya maji.
KUFA KUFAANA! Kwa upande mwingine kero ya mvua imekuwa neema kwa vijana wanaosukuma maguta. Pichani, mwananchi huyu alinaswa Barabara ya Msimbazi akiwa amepanda kitoroli ili kukwepa kero ya kuruka madimbwi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu mtambo wa kukoboa kahawa uliotengenezwa na Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) wakati alipotembelea eneo la SODO mjini Mbeya March 27, 2009. Kulia ni Meneja wa Karakana ya SIDO mkoa wa Mbeya, Charles Hingi.
Waziri Mkuu akitazama baadhi za bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia mazao mabalimbali ya kilimo na Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO), mkoa wa Mbeya wakati alipotembelea eneo la karakana ya Sido mjini Mbeya March 27, 2009.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu shamba la mahindi la Bibi Sarah Joseph lenye ukubwa wa nusu hekari wakati alipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Iganjo katika jiji la Mbeya March 27, 2009.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua shamba la mahindi la Bibi Grace Joseph wakati alipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Iganjo katika jiji la Mbeya March 27, 2009.
Waandishi wetu Mbunge wa Bariadi Mashariki, Adrew John Chenge ametiwa mbaroni na jeshi la Polisi nchini bada ya kutuhumiwa kuua kwa kuwagonga na gari wasichana wawili waliokuwa kwenye usafiri wa Bajaj. kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, ajali hiyo ilitokea saa kumi juzi usiku (Alhamisi) kwenye makutano ya Barabara ya Haile Selaise na...
Siku chache baada ya Diana Aston Villa kuwalipua baadhi ya mastaa wa Bongo akidai wako njia moja, na yeye ametumiwa ujumbe mzito kwa njia ya warakapepe akionywa kuhusu kuugua kwake...
James na Rachel wamesoma pamoja Chuo Kikuu na kuhitimu digrii ya sheria, hata siku moja ingawa walikuwa watu wa karibu, James hakuwahi kumtongoza Rachel mpaka siku ya mahafali ambapo Rachel alikataa akidai siku zote alizokuwa akimkaribia alitaka amtamkie maneno hayo lakini hakufanya, hivyo haikuwa na sababu ya kuanzisha uhusiano siku ya mwisho! Roho ya James ikaumia lakini hakuwa na la kufanya.
Wakatengana na kila mtu kurudi kwao wakiamini wasingekutana tena maishani kumbe Mungu alikuwa na mpango ambao wao hawakuufahamu, alijua wangekutana baadaye Arusha kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Kaskazini wote wakiwa waajiriwa, hapo ndipo uhusiano wao ukaanza upya na kuzaa ndoa na baadaye watoto wawili mapacha (Dona na Dana) wakiwa tayari wamekwishaacha kazi serikalini na kuanzisha kampuni yao binafsi ya Uwakili iliyoitwa James & Rachel Advocates.
Mafanikio yao yakawa makubwa maishani, wakiwashikilia wamiliki wa Migodi wote mkoani humo kama wateja wao. Wakiwa katikati ya kufurahia maisha, mara ghafla wanagundua kwamba mmoja wa watoto wao mapacha, Dana ana matatizo, ukuaji wake si mzuri, amechelewa kukaa, kusimama na hata kuongea! Zaidi ya yote anapatwa na degedege mara kwa mara, hii inawafanya wampeleke kwenye hospitali ya daktari bingwa wa watoto mjini Arusha Dk. Massawe, ambaye baada ya kumwangalia na kumfanyia vipimo aligundua kitu cha kusikitisha na kuwaita wote wawili ofisini kwake.
...tatizo sugu linalowatesa wengi kimya kimya-3 Leo ni Jumamosi na kama ilivyo katika siku kama ya leo, huwa tunakutana hapa katika Uwanja wa Huba na kupeana mawili matatu kwa ajili ya kupanuana mawazo juu ya uhusiano na mapenzi...