arrowSet HomePage |arrowBookMark Us
right
lines

Global Publishers Tanzania- Uwazi » Articles for 30.03.2009

Tafuta  

Tembelea...

Kalenda

Gazeti la Ijumaa

Marafiki wetu

Habari Zilizopita

Soma Magazeti Yetu...

Gazeti la Risasi Mchanganyiko
Amani
Gazeti la Ijumaa Wikienda

Bongo Celebrities ...

 
Habari Zinazotamba Habari Mchanganyiko
» Aunt Ezekiel alivyopigika k ...
» KIGOGO WA MURO NAYE KUKAMAT ...
» JERRY MURO AKOSWA RISASI
» Kigogo afanyiwa umafia
» ZITO LAIBUKA
» JERRY: NASAKWA NIUAWE!
» Waraka wa Papii watua kwa J ...
» Boban: Tunageuzwa watot ...
» Waandishi ndani ya vita ...
» MY HEART IS BLEEDING ( ...
» MALAWI YAONGOZA UMOJA W ...
» ZIFAHAMU SIFA MUHIMU Z ...
» KUTAFUTA MAISHA KUMENIF ...
» MREMBO AUA MWANAE KIKAT ...

 

KAZI KWELIKWELI!!

photos  
Kitimtim cha aina yake kilihibuka kati ya polisi mmoja wa Usalama barabarani (Trafiki) na dereva mmoja wa daladala ifanyayo safari zake kati Mwenge na Kariakoo ambaye alitaka kumgonga polisi huyo wakati akiongoza magari katika taa zilizopo Bamaga jijini Dar es Salaam.
Kitimtim hicho kilianza baada ya dereva kupita katika taa za kuongozea magari wakati taa nyekundu zikiwa zinawaka na aliposimamishwa na Trafiki huyo, alikataa kusimamisha gari lake ndipo askari huyo wa usalama barabarani alipoamua kupanda gari ndogo na kuifukuzia Daladala hiyo ambayo ilikwama kutokana na foleni za barabarani.

KAZI KWELIKWELI!!
Askari huyo wa usalama barabarani akimpeleka dereva huyo katika kituo cha Polisi ili sheria ikafuate mkondo wake.

KAZI KWELIKWELI!!
Wakionekana kwa nyuma dereva huyo akiwa amepigwa Tanganyika Jeck akielekea Polisi.

Picha: Issa Mnally /GPL
    (30 March 2009)
Views: 397 | Maoni (3) |

 

MAISHA YA BONGO HATAUFIKIRI VIPI DILI HAZIJI!

photos  
MAISHA YA BONGO HATAUFIKIRI VIPI DILI HAZIJI!
Kijana huyu alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam akiwa amejiinamia na akionekana kuwa na mawazo mengi.Hata hivyo haikueleweka mara moja masaibu yaliyomfika.

NANI KASEMA VIJANA BONGO WANAJIBWETEKA?
MAISHA YA BONGO HATAUFIKIRI VIPI DILI HAZIJI!
Mshkaji huyu ambaye anafanya biashara ya kuuza mashuka akikata mitaa kusaka wateja maeneo ya Kinondoni.

MTAJI WA MASIKINI NGUVU ZAKE MWENYEWE!
MAISHA YA BONGO HATAUFIKIRI VIPI DILI HAZIJI!
Dili kusaka Mahela! Ndiyo msemo ambao vijana wengi wanautumia ndani ya Bongo.Pichani msela akiwa amejitwisha matenga kibao ambapo haikueleweka kama anayauza au alikuwa akiyapeleka sehemu kwa ajili ya kufanyia biashara.
    (30 March 2009)
Views: 429 | Maoni (5) | Soma Zaidi

 

CHENGE APANDISHWA KORTINI

photos  
Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.
Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa, mawili ni ya kusababisha vifo na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.
Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu ambapo kigogo huyo anapeta nje kwa dhamana ya shilingi Milioni moja chini ya mdhamini mmoja.

CHENGE APANDISHWA KORTINI
Chenge akifikishwa mahakamani leo chini ya ulinzi mkali.

CHENGE APANDISHWA KORTINI
Kamishna wa usalama barabarani Mkoa maalum wa kipolisi wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam Peter Kivuyo aliongoza msafara wa kumfikisha Chenge Mahakamani hapo.

CHENGE APANDISHWA KORTINI
Mke wa Chenge akiingia Mahakamani hapo akiwa na wapambe wake.

PICHA:CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS
    (30 March 2009)
Views: 578 | Maoni (6) |

 

PINDA NA WALIMU MBEYA

photos  
PINDA NA WALIMU MBEYA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na walimu wa shule za Msingi za Mbarali baada ya kutembelea Skimu ya Southern Highlands Estate zamani ikiitwa Mabarari akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya March 28, 2009.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
    (30 March 2009)
Views: 284 | Maoni (0) |

 

TAARABU YA SIKU HIZI BWANA, MIDUME TUPU

photos  
TAARABU YA SIKU HIZI BWANA, MIDUME TUPU
Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph, (katikati) akiwajibika jukwaani leo alfajiri ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam, kulia waliokaa ni waimbaji wa kundi hilo na kushoto ni wanenguaji wa kiume wa kundi hilo.
PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL.
    (30 March 2009)
Views: 637 | Maoni (6) |

 

GARI LA MAGEREZA LAPATA AJALI

photos  
GARI LA MAGEREZA LAPATA AJALI
Gari la Askari Magereza likiwa limepinduka katika maeneo ya Tabata Bima leo asubuhi, lilikuwa likitokea Gereza la Segerea, likiongoza basi lililokua na mahabusu kwenda mahakama mbali mbali.
Picha: Makogoro oging'.
    (30 March 2009)
Views: 355 | Maoni (4) |

 

Wazee wa Masauti walivyopagawisha Msasani Club

photos  
Usiku wa kuamkia leo bendi ya Akudo Impact, 'Vijana wa Masauti' kama kawaida yao walifanya makamuzi ya nguvu katika Bonanza lao pale kwenye ufukwe wa Msasani Club jijini Dar.

Wazee wa Masauti walivyopagawisha Msasani Club
Pichani (kushoto) Rais wa Bendi hiyo, Christian Bella, akiongoza kikosi cha mashambulizi.

Wazee wa Masauti walivyopagawisha Msasani Club
Katika Bonanza hilo kiliibuka kitoto kiitwacho Jere na kufunika kwa kucheza na kuwafanya wanamuziki wa bendi hiyo kukiita jukwaani kifanye tena makamuzi.

Wazee wa Masauti walivyopagawisha Msasani Club
Mashabiki waliohudhuria Bonanza hilo, wakishangilia kwa furaha wakati dogo akifanya mavituz na wanamuzuki wabendi hiyo.
PICHA: RICHARD BUKOS GPL.
    (30 March 2009)
Views: 378 | Maoni (0) |

 

CHENGE KUUA KWA AJALI... 'NI LAANA'

ijumaa wikienda  
CHENGE KUUA KWA AJALI... 'NI LAANA'
Na Mwandishi Wetu

Tukio la Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge a.k.a Mr Vijisenti kugonga bajaji na kuua watu wawili wiki iliyopita, limeelezewa na baadhi ya watu kuwa limetokana na laana ya Watanzania walio wengi...
    (30 March 2009)
Views: 1129 | Maoni (8) | Soma Zaidi

 

Choki: Diana taja gonjwa linalokusumbua

ijumaa wikienda  
Choki: Diana taja gonjwa linalokusumbua
Na Mwandishi Wetu

Madongo yanazidi ‘kumkimbiza’ kwa nyuma aliyekuwa Mnenguaji mahiri nchini, Diana Aston Villa ambaye anaugua TB ambapo hivi karibuni mwanamuziki wa T-Respect, Ali Choki naye kupanua kinywa kumzungumzia Mnenguaji huyo...
    (30 March 2009)
Views: 3125 | Maoni (18) | Soma Zaidi

 

BONY MWAITEGE ATAJWA KUMILIKI VIUNGO VYA ALBINO

ijumaa wikienda  
BONY MWAITEGE ATAJWA KUMILIKI VIUNGO VYA ALBINO
Na Mwandishi Wetu

Muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Bony Mwaitege yumo ndani ya vinywa vya watu kufuatia kusambaa kwa habari kwamba, hivi karibuni amedakwa na ‘manjagu’ akiwa na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)...
    (30 March 2009)
Views: 1903 | Maoni (18) | Soma Zaidi

 

silent forever! -17

hadithi za Shigongo  
Dona ameondoka msituni alikoishi kwa muda mrefu na kutembea kwa miguu hadi katikati ya Jiji la Dar es Salaam baada ya bibi Monica kufariki dunia na kumzika safari iliyomchukua karibu siku nne! Jijini amefikia eneo la Kivukoni kwenye soko la samaki ambako amekutana na msichana aitwaye Joyce, huyu wameungana na kuwa marafiki na anamfundisha kazi ya kupaa samaki ambayo inakuwa chanzo cha riziki yao.

Kwa muda mrefu anaishi maisha ya kujificha akiogopa kuingia mikononi mwa wauaji waliotaka kumuua baada ya kuwaua wazazi na pacha wake Dana, baadaye yeye na Joyce wanaamua kuondoka nchini Tanzania kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine ambako mpaka sasa hawaelewi ni wapi lakini wamezamia meli iitwayo MV Sabra na kusafiri kwa siku kadhaa majini wakiwa wamejificha kwenye tundu la nanga, chakula chao kikubwa kikiwa ni mikate na maji.

Wakiamini mambo yote yamekwenda sawa, ghafla mkojo ambao wamekuwa wakikojoa ndani ya tundu hilo unaonekana kuwaponza! Mabaharia wanasikia harufu ya mkojo karibu na tundu la Nanga na kuanza kuulizana kama kuna wenzao wanakojoa sehemu hiyo badala ya kutumia choo. Hii ni hali ya hatari kwa Dona na Joyce.

Je, nini kitaendelea? Sakata hili la mkojo litaishaje? SONGA NAYO…
    (30 March 2009)
Views: 979 | Maoni (12) | Soma Zaidi

 

Niliishi kuzimu miaka ishirini Part-II-23

Mikasa ya kusisimua  
Zubeda Ruvanga, mwanamke mwenye umri wa miaka 38, anasimulia mateso aliyokumbana nayo tangu akiwa mtoto. Wachawi walianza kumpa tabu za maisha tangu akiwa darasa la tatu kwenye Shule ya Msingi Mwandiga Kigoma. Wiki iliyopita alikomea pale alipokuwa alipokuwa akishauriwa na Sikuzani, kuhusu kuwatuma watu waende duniani wakawakusanye binadamu ili walime shamba la kuzimu, wapande mbegu na kuliwekea mbolea. Endelea kusoma...
    (30 March 2009)
Views: 589 | Maoni (1) | Soma Zaidi

 

‘Tekniki’ za kutatua migogoro ya kimapenzi-2

Mahaba  
Uwezo wa Mungu ni wa ajabu mno. Amefanya mambo makubwa kunifanya mimi na wewe tuwe hapa leo na kufanya yanayoonekana sasa. Ni kupitia pointi hiyo moja tu, nitaendelea kumhimidi na kulitukuza jina lake kila siku katika maisha yangu yote...
    (30 March 2009)
Views: 379 | Maoni (0) | Soma Zaidi

 

Simba wawaa

champion  
Simba wawaa
Na Waandishi Wetu

SIMBA WAWAAA, hivyo ndivyo mashabiki wa Simba walivyokuwa wakiimba wakati timu yao ikiimudu vilivyo Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Uhuru jana na Wekundu wa Msimbazi hao kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kabla ya mechi hiyo kuahirishwa kutokana na dimba hilo kujaa maji kufuatia mvua kubwa kunyesha...
    (30 March 2009)
Views: 398 | Maoni (2) | Soma Zaidi

 

Toto Afrika yamuondoa Barasa Yanga

champion  
Na Shufaa Lyimo

KUNA kila dalili Klabu ya Yanga ikamkosa mshambuliaji wake, Mkenya Mike Barasa, kwenye mechi ya marudiano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi Al Ahly, kutokana na mchezaji huyo kusumbuliwa na Malaria pamoja na maumivu ya nyama za paja...
    (30 March 2009)
Views: 246 | Maoni (0) | Soma Zaidi
Back  <<  1 2  >>  Next Page
 

Kura Yako / Poll

Habari Katika Picha


Gazeti la Uwazi



Nani Yupo / Alikuwepo


Home Page | About Us | Regista | Picha | Bongo Celebrities | Maoni | Contact Us

 hit counter

counters

2008 © globalpublisherstz.com